Sunday, 11 May 2014

MAWE KATIKA MFUKO WA NYONGO (GALLSTONES/CHOLELITHIASIS)


Ugonjwa huu unasabishwa na kuwepo au kutengenezwa kwa aina ya mawe 
katika kibofu au mfuko 

wa nyongo. Tatizo hilo linaonekana kuongezeka kwa kasi katika nchi 

zinazoendelea ikiwamo 

Tanzania,

 lakini linazisumbua zaidi nchi zilizoendela.
Gallstones huwapata zaidi wanawake kuliko wanaume na zaidi walio na uzito 
mkubwa, wanene 

kupita kiasi wenye umri kati ya miaka 40 hadi 50 hivi.
Hii haimaanishi kwamba walio na umri chini au juu ya hapo hawawezi kupata 
ugonjwa huu au walio 

na uzito wa wastani au wembamba wanakwepa tatizo hili.

Huwapata pia watu walio na kisukari, kupoteza uzito kwa haraka, wajawazito, 
kunywa pombe, 

kuwepo na historia ya mwanafamilia wa karibu aliyepatwa na ugonjwa huu na 

kadhalika.

Ni kwa jinsi gani tatizo hili linatokea?

Ni vigumu kuelezea hapa na mtu wa kawaida akaelewa, kwani hilo ni tatizo la 

kitaaluma zaidi. 

Ingawa kwa uchache moja ya sababu ni kuganda kwa mafuta katika mfuko wa 

nyongo, au mfuko 

huo kushindwa kufanya kazi yake kama kawaida.

Dalili za ugonjwa huu ni pamoja na maumivu ya mara kwa mara upande wa juu 

kulia katika tumbo. 

Maumivu haya huweza kuwa endelevu, huelekea pia upande wa kulia mgongoni 

au kwenye bega.

Kuhisi kichefuchefu mara kwa mara na kutapika, kushindwa kula chakula chenye 

mafuta, kupata 

homa, kubadilika na kuwa wa manjano. Ni muhimu mgonjwa anapopatwa na 

maumivu makali 

yasiyovumilika na homa, akimbizwa hospitali haraka iwezekanavyo na pale mgonjwa anapokuwa 

wa manjano pia ni muhimu akaenda hospitali mapema zaidi.

Uchunguzi
Vipimo vya mwanzo, ambavyo mgonjwa atahitajika kufanya ni kuangalia uwezo wa 
ini kufanya kazi 

kupitia kwenye damu, vipimo vingine ni ultrasound ya tumbo, Ct scan, MRCP-

magnetic resonance 

cholangiopancreatography

Matibabu
 Katika kutibu ugonjwa huu, iwapo mawe mawe ni ya muda mrefu, mengi au kubwa, upasuaji wa 

kutoa mawe na mfuko wa nyongo huhitajika.
Upasuaji uhitajika pia pale mawe yanapoleta matatizo makubwa katika mwili (complications), mfano 

homa kali(acute cholecystitis, gall bladder empayema), upasuaji ndiyo njia bora ya kutibu ugonjwa wa mawe.

Kutokana na kukua kwa teknolojia, upasuaji huweza kufanywa kwa vifaa maalumu na kompyuta pia 

(laparoscopic cholecystectomy)

Pia kuna njia ya kutumia kifaa maalumu bila kupasua. Kifaa hiki 

hutoa aina fulani ya miale, ambayo hulisagasaga jiwe (extracorporeal shockwave lithotripsy) ni 

vyema ifahamike kwamba utumiaji wa teknolojia katika nchi zetu ni aghali na walio wengi katika 

nchi hizo hawawezi kuzimudu gharama hizo ikilinganishwa na upasuaji wa kawaida.

Iwapo mgonjwa hawezi kustahimili upasuaji kutokana na sababu maalumu, au jiwe ni dogo sana, 

au sababu nyingine yeyeto ile kulingana na uamuzi ya mtaalamu, basi mgonjwa huweza kupewa 

dawa maalumu kwa ajili ya kuyeyusha jiwe hilo. Hata hivyo tatizo katika dawa hizo ni kwamba kuna 

uwezekano wa mawe kurudi tena (recurrence) ndani ya mwaka mmoja kwa asilimia zaidi ya 12 na 

kwa zaidi ya asilimia 60 ndani ya miaka 10, kulingana na tafiti mbalimbali za kisayansi zilizofanyika. 

Piia kuna uwezekano mkubwa wa dawa kushindwa kufanya kazi kabisa na hivyo upasuaji kubaki 

kuwa ndiyo dawa ya mwisho.

Matatizo makubwa yayoweza kuletwa na ugonjwa wa mawe katika kibofu cha nyongo na 

kuhatarisha maisha ya mgonjwa ni kama:

• Kupata homa kali na maumivu makali ya tumbo upande wa juu –acute cholecystitis, ambapo 

hupelekea mgonjwa kulazwa hospitali, kupangiwa upasuaji.

• Jiwe kutoka katika mfuko na kuingia katika mrija mkuu wa kusafirisha nyongo kwenda katika 

utumbo mwembamba na kuuziba mrija huo, hivyo mgonjwa kupata maumivu na kubadilika kuwa wa 

manjano (common bile duct calculi abstraction), upasuaji wa haraka huhitajika, au kutumia 

teknologia bila kupasua kwa kutumia kifaa maalumu kutoa jiwe hilo-ERCP hii niteknologia ya kisasa 

(hatuna huduma hii hapa nchini).

• Mfuko wa nyongo kutunga usaha (empyema/suppurative cholecystitis), au kutoboka, au kuoza na 

kuharibika kabisa( gangrenous gall balder), huhatarisha zaidi maisha ya mgonjwa.

• Jiwe kuteleza na kuziba mrija wa kongosho, hivyo kusababisha maumivu makali- acute caliculi 

pancreatitis.

• Mawe kusababisha kuwepo kwa saratani ya mfuko wa nyongo.

3 comments:

  1. Natibu huo ugonjwa bila upasuaji ndani ya wiki moja. Unaweza kunitafuta kwenye email: riahradhey@yahoo.com

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ibrahim nahitaji matibabu ya gallstones. Nawezaje kukupata?

      Delete
  2. Nahis maumivu upande wa kulia juu ya tumbo had mgongon nlivyopiga ultrasound wakasema nyongo imejaa dat y nahis maumivu makali sa nashindwa kuelewa imejaa nini nliuliza wakasema hyo nikawaida tyu nikapewa dawa za kutumia kidgo nafuu but maumivu yako pale pale...je ni mawe yamejaa?😢😢😢😢

    ReplyDelete