Thursday, 1 May 2014

UNYWAJI POMBE KUPINDUKIA CHANZO CHA KUTOPATA / KUTOSABABISHA MIMBA.




Hii inaweza kuwa habari mbaya kwa watengenezaji au wauzaji wa vinywaji hivi au hata kwa uchumi wa Nchi, lakini huu ndio ukweli halisi.
Kwamba, tatizo la unywaji pombe kupita kiasi linaongezeka katika jamii kila siku za hivi karibuni na linawahusisha wote, vijana, watu wazima na hata wazee.

Pombe za aina mbalimbali na ujazi tofauti zimekuwa zikizalishwa viwandani au kwa njia za kienyeji kila siku na kasha kuuzwa kwa bei ndogo ya hadi sh 200 ya kitanzania ili mradi mtu aweze kuimudu.
Kwa vijana wanaotumia vileo hivyo, wengi wao hujitetea wakisema kuwa wanajiburudisha huku wengine wakisema kuwa wanatumia kinywaji husika ili kupunguza msongo wa mawazo, kupunguza au kujiepusha na ugumu wa maisha.
Hizi zote zinaweza kuwa sababu nzuri kulingana na mazingira ya mhusika mwenyewe, lakini nyuma yake kuna madhara.
Unaweza kuijuliza je, wengi wanao kunywa aina mbalimbali za 
 
pombe katika maisha yao wanafahamu kuwa unywaji huo hasa ule wa kupitiliza kiasi unaweza kuwasababishia matatizo kiafya likiwamo la kupunguza uwezo wa kupata watoto?
Utafiti uliofanywa na chuo kikuu cha SURREY cha uingereza unathibitisha suala hilo na kueleza kuwa kutokana na kuongezeka kwa matatizo ya uzazi kwa wanandoa katika miaka ya hivi karibuni, pombe imekuwa chanzo cha kuparanganyika kwa ndoa, kukosa watoto pia.
 
Kwa sababu hiyo, chuo kikuu hicho kiliamua kufanya utafiti kwa kuwahusisha wanandoa kadhaa waliokuwa wanakabiliwa na tatizo la mmoja wao kushika mimba.
Utafiti huo ulibainisha kuwa ongezeko la tatizo hilo katika miaka ya karibuni limechangiwa na kiasi kikubwa na mabadiliko ya mfum wa maisha ya binadamu, hususani katika masuala ya ulaji vyakula.
 
Utafiti huo ulonyesha kuwa wanandoa ambaowalikuwa na historia ya matatizo ya uzazi walibadilisha mfumo wao wa maisha, kwa kufuata kanuni za ulaji wa chakula na kuacha au kupunguza matumizi ya pombe walifanikiwa kwa asilimia 80 kuondokana na tatizo hilo.
Pia, utafiti huo ulibainisha kuwapo kwa uhusiano mkubwa uliopo kati  ya chakula anavyokula mtu na uwezo wake wa kuweza kuzaa.
Wataalamu wanasema kuwa unywaji wa pombe kwa kiasi Fulani 
 
huchangia katika kupunguza uwezo wa kuzaa kwa mwanamke na mwanamume
Imebainika kuwa unywaji pombe kwa kiwango chochote huunguza nusu ya uwezo wa uzazi kwa mhusika
Kwa upande wa mwanamke anayekunywa chini ya uniti 5 ambazo ni sawa na ujazo wa glasi ya milimita 175 anao uwezo mkubwa wa kupata ujauzito ndani ya kipindi cha miezi sita ukilinganisha na Yule anaye kunywa zaidi.
 
Utafiti huo unaonyesha kuwa unywaji pombe husababisha kupungua kwa idadi za mbegu za kiume kwa mwanamume na pia hupunguza kasi yake katika mwili kiasi kwamba pindi uzazi zinapotoka na kuingia sehemu za uzazi za mwanamke zinakuwa hazina nguvu na hivyo kuathiri ubora wake.
Pia, unabaini utafiti huo kuwa pombe hufanya mwili wa binadamu kushindwa kufyonza vimeng’enyo vinavyopatikana katika vyakula  kama vile madini ya zinki, ambayo ni muhimu kwa kurutubisha 
 
mbegu za mwanamume na kiandaa mwili wa mwanamke kwa ajiri ya kutunga ujauzito.
Utafiti huo unabainisha kuwa kama unajitayarisha kupata motto inabidi kuachana na matumizi ya ombe na kahawakwa kipindi cha miezi mitatu mfululizo ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kufanikiwa katika hilo.
NINI UKWELI KUHUSU MATUMIZI YA POMBE.
Daktari wa magonjwa ya kinamama kutoka Hospitali ya taifa ya muhimbili, anasema kuwa japo hakuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya pombe na viungo vya uzazi vya binadamu lakini kuna 
 
ukweli kwamba pombe huchangia katika kupunguza uwezo wa mtu kutunga mimba au kusababisha mimba.
 
Kama mtu hana tatizo lolote la kiafya linalomfanya ashindwe kupata motto, pombe inaweza ikasababisha kutokea kwa tatizo hilo kwa mtu huyo.

Suala zima la mfumo wa uzazi linaendeshwa na ubongo ilihali unywaji pombe kupita kiasi nako huathiri mfumo wa fahamu , hivyo ni lazima kwa mtu anayetumia pombe katika kiwango hicho kukumbana na tatizo hilo.
 
Hata katika hali ya kawaida ili mtu aweze kusababisha au kusika mimba ni lazima ashiriki kikamilifu katika tendo la kujamiiana na ikiwa amelewa atashindwa kushiriki kikamilifu kwani tendo hilin huhusisha akili zaidi.
Mfumo wa uzazi unaendeshwa na ubongo hivyo mtu akiwa mlevi wa kupindukia kuna uwezekano mkubwa uwezo wake wa kupata au kusababisha mimba ukawa mdogo.
 
Pia unywaji wa pombe kupindukia kwa muda mrefu kunaweza kusababisha uharibifu kwa mfumo mkuu wa neva na mfumo wa neva za pembeni na kusababisha kupoteza tamaa na kutosisimka wa mwanaume.
 
Pombe ina athari nyingi kwa mwili wa binadamu kwani pamoja na kuathiri  kondo la uzazi na mayai ya uzazi kwa mwanamke na mwanaume, Pia huleta madhara kwa viungi vingine kama figo na ini.
Kama pombe itatumiwa katika kipindi cha ujauzito inaweza kuathiri hata ukuaji wa mtoto aliyeko tumboni, kwani huyuka kizuizi cha kondo la nyuma (placenta) na inaweza kudidimiza ukuaji wa kijusi.
 
Kwa ujumla pombe ina madhara ya kiafya kwa mwili wa binadamu, hivyo kabla mtu hujaamua kuitumia inabidi  kutafakari athari na faida zake ili akinywa awe na taarifa sahihi kuhusiana na kitu gani kinaingia mwilini mwake.
‘’UNYWAJI POMBE KUPITA KIASI NI HATARI KWA AFYA YAKO

0 comments:

Post a Comment