Thursday, 1 May 2014

JINSI YA KUONGEZA UWEZEKANO WA KUPATA/KUZAA MTOTO WA KIUME.


Uchaguzi wa jinsia, au kutabiri jinsia ya mtoto atakaezaliwa ni topic yenye mkanganyiko katika kada ya afya hususani uwanja wa matabibu.
Ambapo madaktari na wataalamu wa masuala uzazi, wanawwapinga wakunga wa zamani kwa mujibu wa wao walivyokuwa wanaamini kuhusiana na hii jinsi ya kutabiri.
Baadhi ya watafiti walikuja na hoja na baadhi ya mbinu ambazo zinaongeza uwezekano wa kupata motto wa kiume au wa kike.

Dokta Shettles, alikuja na njia yake inayoitwa SHETTLE METHOD, ambayo ilifanyiwa ucchinguzi nae LANDRUM SHETTLES mnamo miaka ya 1960 na rekodi yake kuandikwa katika kitabu kilichoitwa
 “HOW TO CHOOSE THE SEX OF YOUR BABY”
Na inakadiriwa kuwa yapata asilimia 75% ya waliojaribu walifanikiwa.
Baadhi ya watafiti wengine walisema kuwa mlo na mkao wakati wa kufanya tendo la ndoa  ndio una athiri uchaguzi wa jinsia ya motto atakaezaliwa.
Katika makala hii nitaangazia juu ya jinsi ya kuongeza uwezekano wa kupata mtoto wa kiume
Hivyo, zingatia vidokezo hivo ili kuongeza uwezekano wa kupata mtoto wa KIUME.
1. ELEWA FALSAFA YA NJIA YA SHETTLES
Njia hii ina jikita katika wazo la kuwa Y-chromosomes sperm( jinsia ya kiume) ambazo ni chache, dhaifu na hutembela/kusafiri kwa haraka kuliko X chromosome sperm (jinsia ya kike)

2. UTAMBUE MUDA WA YAI KUPEVUKA/OVULATION
Kulingana na NJIA YA SHETTLES, unatakiwa kufanya tendo la ndoa KABLA, BAADA ya ovulation kutokea MASAA MACHACHE OVULATION KUTOKEA. Hii ni kwa lengo la kuongeza  uwezekano wa kupata mtoto wa kiume.
 
KUMBUKA;
·       Kuwa na chart ya kuangalia ute toka ukeni, angalia ute kila siku, kabla ya ovulation, ute unatakiwa kuwa wa kuvutika pale unapoguswa/ elastic na pia watery
·       SHETTLES ana shauri kuwa chati yako ya kuangalia ute  inabidi ifanyike kwa angalau mwezi mzima ili kuujua jinsi ute unavyo tofautiana unapokuwa unaelekea  kwenye tarehe za ovulation.
·       Pia angalia BASAL BODY TEMPERATURE/ Mabadiliko ya joto lako la Mwili, Chukua vipimo vya joto kila asubuhi kabla hujatoka kitandani, kipindi upo kwenye ovulation joto la mwili litapanda sana, hivyo kwa sababu unatakiwa kufanya mapenzi siku za karibu na ovulation iwezeanavyo ili kuweka mazingira mazuri kwa kupata mtoto wa kiume, unashauri kujua mwenendo wa joto lako angalau kwa muda wa miezi miwili ili kujua ni kipindi gani joto linakuwa juuna hivyo kujua ovulation ipo tayari.
·
3. UJUE MUDA  WA KUFANYA TENDO LA NDOA ILI KUONGEZA UWEZEKANO WA KUPATA MTOTO WA KIUME.
Fanya tendo la ndoa ama mapenzi masaa 24 kabla ya muda wa ovulation kufika na masaa 12 baada ya ovulation kutokea. Katika muda huu, ute unaoteleza toka katika cervical utaisaidia mbegu Y(kiume) toka kwa mwanaume ambayo hutembea/husafiri kwa haraka, lakini dhaifu kwa maaa kwamba hufa mapema na hivyo kuifikia mapema/haraka yai la kike ambalo ni X, ambalo X yenyewe hutembea mwendo wa pole, lakini lipo imara kwa kukaa muda mrefu.

4. FANYA TENDO LA NDOA/MAPENZI KWA MKAO/ STYLE HII HAPA.
Dr Shettles ana shauri, Uume uingie zaidi katika Uke, Huu ni mkao wowote ambao unaamini kuwa uume utaingia zaidi katika uke ambapo mbegu za kiume zitamwagwa karibia na cervix nahivyo kuweza kusafiri kwa urahisi na haraka kwa mbegu Y Kuelekea kurutubisha Yai la kike kiurahisi. Ndio maana ya mkao wa kimapenzi huo unahitajika. Mkao unaoshauriwa ni ule wa rear-entry position kwa Kiswahili unaitwa Mbuzi kagoma almaarufu doggy style
5. MWANAMKE AFIKE KILELENI/MSHINDO MAPEMA KABLA YA MWANAMME.
MwanamKe anapofanikiwa kufika kileleni/mshindo wake wakati wa tendo la Ndoa/mapenzi, mwili wake huzalisha mazingira ambayo ni ALKALINE zaidi katika UKE, ambayo ina faida kwa mbegu za kiume Y.

BORESHA ULAJI WAKO WA MLO ILI KUONGEZA UWEZEKANO WA KUPATA MTOTO WA KIUME.
1. ELEWA SABABU ZA MLO/ CHAKULA KATIKA UCHAGUZI WA JINSIA YA MTOTO.
Moja ya vitu vinavyopelekea chakula kuwa moja ya sababu katika uchaguzi wa jinsia ni kwamba  chakula na vinywaji vinaweza kubadilisha PH katika mwili ana katika UKE, ambapo inaweza kuathiri mazingira ya sperm X au Y
2. ACHA KUTUMIA/JIHADHARI NA VYAKULA VYENYE ACIDIC KWA WINGI.
Mbegu ya kiume Y inapendelea zaidi kwenye mazingira ya ALKALINE, na vyakula vyenye ACIDIC vitabadilisha mazingira ya UKE kuwa na ACIDIC.

3. KULA VYAKULA HIVI ILI KUONGEZA UWEZEKANO WA KUPATA MTOTO WA KIUME.
Wiki kadhaa/chache kabla ya zoezi zima kufanyika, kula Nyama Nyekundu kama Nyama ya ng”ombe, mayai, samaki, maharage, peazi, uyoga, mahindi, ngano, pia mkate. Vyakula hivi vitajenga mazingira zaidi ya kufanya hali ya ALKALINE pH kuwa katika kiwango kizuri katika UKE.
4. PIA, KULA KARIBIA WAKATI WOTE WA SIKU HIZO.
Kutokana na tafiti zilizofanyika  huko chuo cha Oxford na chuo kikuu cha EXETER       Nchini ENGLAND, zinasema Kiwango Kikubwa cha nishati/energy Inahitajika zaidi na pia kiwango kikubwa cha Glucose kiwe kikubwa kinahusishwa nacho katika zoezi hili la kumpata motto wa kiume.
5. INAHIMIZWA MPENZI WA KIUME KUTUMIA VINYWAJI VYENYE CAFFEIN KABLA YA TENDO LA NDOA/MAPENZI.
Inaaminika kuwa vinywaji vyenye caffeine husaidia kuifanya mbegu za kiume Y kuwa imara ZAIDI.
6. KUNYWA DAWA YA KIKOHOZI AINA YA SYRUP MASAA MACHACHE KABLA YA TENDO LA NDOA.
Baadhi ya watafiti, na wana NADHARIA wa masuala ya uchaguzi wa jinsia wanasema kuwa na kuamini dawa ya kikohozi yenye/ Iliyo na aina ya GUAIFENESIN, hufanya mazingira kuwa mazuri wa mbegu Y SPERM, Hivyo angalia dawa hiyo kwa AINA ya Ingredients na hakikisha kama imeandikwa GUAIFENESIN Kabla hujainywa.
MUHIMU;
Ili kuongeza uwezekano mkubwa wa kupata mtoto wa kiume, wanaume inahimizwa  BOXERS zenye material ya pamba zisizombana,

 Na sio zile za kubana sana zenye material ya nailon kwa sababu hizo zinazobana sana zinaongeza hali ya joto katika maeneo ya kiume hususani kwenye KORODANI na hivyo inaweza kupelekea uzalishwa hafifu wa mbegu za kiume.

0 comments:

Post a Comment