Thursday 1 May 2014

UGONJWA WA EBOLA

Ebola ni ugonjwa wa hatari
unaosababishwa na virusi vijulikanavyo
kwa lugha ya kitaalamu “Ebola
Virus”. ugonjwa wa damu
kutoganda, 
Ugonjwa huu ni miongoni mwa
magonjwa yajulikanayo kwa ujumla kama
Homa za Virusi zinaazosababisha kutokwa
na Damu mwilini,(Viral Haemorrhagic
Fevers) Chanzo kamili cha virusi vya ugonjwa
huu hakijulikani. Katika orodha ya watu 10
waliopata kirusi cha Ebola, basi wastani
kati ya watano au tisa hufa.
 Hali inayosababisha
mlipuko wake pia haijulikani.Ugonjwa
huu pia hauna tiba wala chanjo.Hata dawa
za jadi hazijathibitika kutibu ugonjwa huu.

Dalili za Ebola
Pale watu wanapopata Ebola, dalili zake za
kwanza ni kuonekana kama magonjwa
mengine
Dalili za ugonjwa huu ni:-
Homa kali, inayoambatana na kutokwa damu
katika matundu yote ya mwili kama pua,njia
ya haja kubwa na
dogo, mdomoni, masikioni, machoni n.k.
· Kutapika damu
· Kuharisha damu
· Fizi kuvuja damu
· Kutokwa na damu na kuvujia chini ya
ngozi. Kwasababu ya kutokwa na damu
sehemu za haja kubwa na ndogo, choo
na mkojo pia vitaonekanakuwa na damu.

Kuenea kwa Ebola.
Ugonjwa huu unaenea kwa urahisi sana
na haraka kutoka mtu mmoja hadi mtu
mwingine kupita njia mbali mbali.
Njia hizi ni:-
· Kuingia mwilini au kugusana na:-
· Mate
· Damu
· Mkojo
· Machozi
· Kamasi
majimaji mengine ya mwili, ikiwa ni pamoja na
jasho.
kugusa mtu aliyekufa kwa ugojnwa wa Ebola
kushika/kugusana na wanyama jamii ya nyani.
· Kuchomwa na sindano au vifaa ambavyo
havikutakaswa
Ugonjwa huu pia huambukizwa kwa njia ya
kujamiiana.
kugusa taka ngumu au maji taka yaliyotokana
na kumhudumia mgonjwa Ebola.

Athari za ebola

· Unasambaa kwa haraka sana
· Unasababisha vifo vingi kwa muda mfupi
· Jamii huingiwa na hofu na wasi wasi na
kushindwa kufanya shughuli zao za
kawaida
ni gharama kuwahudumia/kutibu wagonjwa.
· Mipaka inaweza kufungwa na watu
wakashindwa kusafiri kutoka eneo/nchi
moja hadi nyingine.

Tiba ya Ebola
Hakuna tiba maalumu ya homa ya Ebola.
Lakini ikiwa watu wanapata huduma
bora kutoka kwa madaktari na wauguzi,
wengi wao huishi.
 
Kinga ya Ebola
Ugonjwa wa Ebola unaweza kuzuilika.Ni
muhimu kwa kila mmoja kuwajibika
Njia kuu za kujikinga na ugonjwa huu:-

 Kuepuka kugusa au kuingiwa na
mate, damu, mkojo, jasho, kinyesi, machozi na
maji maji mengine yanayotoka mwilini mwa
mwenye dalili za ugonjwa wa Ebola.
Kwa kuwa ugonjwa huu pia huambukizwa
kwa njia ya kujamiiana, epuka kuwa na
mpenzi zaidi ya mmoja.

 Kutoa taarifa mapema kwa viongozi wa
serikali na wa huduma za Afya katika ngazi
zote pale anapotokea mtu mwenye dalili za
Ebola

uwahi katika vituo vya huduma za Afya pale
mtu anapoona dalili za ugonjwa huu.

· Wananchi wana tahadharishwa kuepuka
kushughulikia maiti ya mtu aliyekufa kwa
Ebola;badala yake watoe taarifa kwa
uongozi wa kituo cha huduma za Afya kwa
ushauri. 
ufanya ufatiliaji madhubuti wa ugonjwa huu.

· Wananchi waepuke mila na desturi
zinazoweza kuchelewesha kupata huduma
muhimu na kuzidi kueneza ugonjwa wa
Ebola
Wagonjwa wa Ebola
hutengenishwa na wagonjwa wengine ili
wasipate kuambukizwa.

Zingatia usafi wa mwili na tabia.

KUMBUKA
Ugonjwa wa Ebola ni hatari sana.
Unasambaa haraka na unasababisha
Madhara na vifo vingi.
Epukana nao.

0 comments:

Post a Comment