DALILI ZA MSHITUKO WA MOYO
Baadhi ya wakati mshituko wa moyo
hutokea kwa dalili zilizo wazi na kwa haraka sana. Lakini mara nyingi mshituko
wa moyo hutokea polepole huku mtu akipata maumivu ya wastani na kutokujisikia
vyema.
Mara nyingi watu wanaopatwa na hali
kama hiyo huwa hawana uhakika na kile kinachotokea na husubiri kwa muda mrefu
kabla ya kuomba msaada au kumuona daktari.
Zifuatazo ni dalili ambazo hutokea
pale mtu anapopatwa na mshituko wa moyo.
1) Maumivu katika kifua: Mara
nyingi mtu anapopatwa na mshituko wa moyo huhisi maumivu sehemu za kifua hasa
sehemu za katikati ya kifua ambayo huisha baada ya dakika kadhaa au mara
nyingine maumivu hayo huisha na kurudi tena. Mtu huhisi kana kwamba kifua
kinambana, kimejaa na kinauma.
2) Maumivu katika sehemu za juu za
kiwiliwili: Mtu huhisi maumivu sehemu za mikono, mgongo, shingo, taya na tumbo.
3) Kukosa pumzi au kushindwa
kupumua: Hali hii huweza kutokea ikichanganyika na maumivu ya kifua au bila
maumivu hayo. Dalili nyinginezo ni pamoja na kutoka kijasho chembemba (cha
baridi), kujisikia kichefuchefu pamoja na kichwa kuwa chepesi na
kizunguzungu.
Moyo kwenda mbio au kwa ibara nyingine mapigo ya moyo kutokea kwa kasi zaidi
kuliko kawaida.
Unashauriwa iwapo utajisikia mumivu ya kifua, hasa pamoja na mchanganyiko wa moja ya dalili tulizozitaja, usisubiri na haraka wasiliana na kituo cha afya ili upatiwe msaada, au elekea haraka
Unashauriwa iwapo utajisikia mumivu ya kifua, hasa pamoja na mchanganyiko wa moja ya dalili tulizozitaja, usisubiri na haraka wasiliana na kituo cha afya ili upatiwe msaada, au elekea haraka
hospitali mwenyewe. Muda unaofaa wa
kutibiwa mshituko wa moyo ni saa moja tangu wakati wa kutokea hali hiyo.
Kutibiwa mapema dalili za mshituko wa moyo hupunguza hatari ya kuharibika seli
za moyo. Hata kama huna uhakika dalili unazohisi ni za mshituko wa moyo au la,
ni bora umuone daktari na ufanyiwe uchunguzi.
Utafiti waliofanyiwa wanawake 515
ambao walipata mshituko wa moyo umeonyesha kuwa, wengi wao waliripotiwa kuwa na
dalili za kujihisi kuchoka, kutolala vyema, kushindwa kupumua, kujisikia
maumivu baada ya kula na wasiwasi.
Asilimia 70 ya wanawake hao
walihisi dalili zaidi ya moja kabla ya kupatwa na mshituko wa moyo.
Karibu theluthi moja ya kesi za
ugonjwa wa mshtuko wa moyo hutokea kimya kimya, bila maumivu ya kifua wala
dalili nyinginezo. Kesi kama hizo hugunduliwa baadaye katika vipimo. Kesi kama
hizo hutokea zaidi kwa wazee, wagonjwa wa kisukari na baada ya kuunganishwa
moyo au heart transplant.
VIPIMO VYA MSHITUKO WA MOYO.
Kwa kawaida madaktari hufahamu kuwa
mtu amepatwa na mshituko wa moyo au anaelekea kupatwa na mshituko huo kutokana
na dalili alizonazo na anavyojisikia.
Pia kwa kutegemea historia ya
kifamilia na ya kitiba ya mgonjwa pamoja na vipimo.
Kipimo kikuu kinachotumika kupima
iwapo mtu amepatwa na mshituko wa moyo ni EKG. Hicho ni kipimo kinachoonyesha
na kurekodi mwendo na harakati ya moyo. Kipimo hicho huonesha moyo unakwenda
kwa kasi ya kiasi gani, mapigo ya moyo na mdundo wake.
Kwa hakika kipimo cha EKG huonyesha
dalili za kuharibika moyo kutokana na matatizo ya mishipa ya moyo ya ugonjwa wa
coronary heart disease na pia dalili za mshituko wa moyo uliotokea huko nyuma
na unaotokea hivi sasa.
Kipimo kingine ni cha damu ambacho
huonesha protini zinazoonekana kwenye damu zinazotokana na seli za misuli za
moyo zilizokufa.
Basi tuangalia utafiti uliosema
kwamba mshituko wa moyo mara nyingi hutokea saa tatu asubuhi.
Wataalamu wa magonjwa ya moyo
wamesema kuwa hatari ya kupatwa na mshituko wa moyo hutokea zaidi mapema
asubuhi, hasa saa tatu asubuhi.
Utafiti huo uliotangazwa katika Kongress ya 4 ya magonjwa ya moyo ya Mashariki ya Kati umeonyesha kuwa, watu wanaokabiliwa na hatari ya kupatwa na mshituko wa moyo, hutokewa na ugonjwa huo mapema asubuhi kwa sababu ya mabadiliko ya homoni, ambayo huongeza hitajio la oksijeni la mishipa ya moyo katika wakati huo, na kusababisha mshituko wa moyo.
Utafiti huo uliotangazwa katika Kongress ya 4 ya magonjwa ya moyo ya Mashariki ya Kati umeonyesha kuwa, watu wanaokabiliwa na hatari ya kupatwa na mshituko wa moyo, hutokewa na ugonjwa huo mapema asubuhi kwa sababu ya mabadiliko ya homoni, ambayo huongeza hitajio la oksijeni la mishipa ya moyo katika wakati huo, na kusababisha mshituko wa moyo.
Uchunguzi huo umeeleza pia kuwa, ripoti
zinaonyesha ongezeko la matukio ya mshituko wa moyo katika siku za Jumatatu,
suala ambalo huenda likawa linachangiwa na kiasi kikubwa na kula kupita kiasi
siku za wikiendi.
Wataalamu hao pia wamesema kuwa,
mishipa ya juu ya mwili huwa inasinyaa msimu wa baridi, hali ambayo ni kinyume
na utendaji wa mishipa ya moyo na husababisha kupungua kiwango cha oksijeni
inayohitajiwa na misuli ya moyo.
Wamesema hii ndio sababu, watu
hupata mishtuko wa moyo kwa wingi wakati wa mapukutiko (fall) na baridi
(winter).
NAMNA YA KUTIBU MSHITUKO WA MOYO
Mshituko wa moyo unahitaji
kushughulikiwa haraka. Kama unamshuhudia mtu akipatwa na mshituko wa moyo
unapaswa kuomba msaada haraka au kumfikisha kituo cha afya haraka iwezekanavyo.
Kama mtu aliyepatwa na mshituko wa
moyo amepoteza fahamu, baada ya kuomba msaada kituo cha afya cha karibu,
unapaswa kumfanyia CPR mara moja kama unajua kufanya hivyo.
CPR ni kitendo ambacho husaidia
kufikisha hewa ya oksijeni katika ubongo. Kwanza hakikisha njia za hewa za mgonjwa
ziko wazi, yaani hakikisha mdomoni na puani kwake hakuna kitu kinachozuia hewa
kupita na msaidie kwa hewa kila baada ya kumkandamiza kifuani au (chest
compress) mara 30.
Kama hujui CPR pia unapaswa kuanza
kumkandamiza kifuani mgonjwa aliyepoteza fahamu kutokana na mshituko wa moyo,
kwani kufanya hivyo huenda kukaokoa maisha yake.
Nitaelekeza hapa jinsi ya
kumkandamiza kifuani mgonjwa aliyepatwa na mshituko wa moyo na aliyepoteza
fahamu.
Weka kiganja cha mkono wako mmoja
katika mfupa wa kifua (chestbone) katikati ya matiti na kiganja cha pili juu ya
cha kwanza, na kandamiza kwa kiasi cha inchi mbili au sentimeta 5 kuelekea
chini.
Endelea kukandamiza na kuachia mara
30. Kama unajua namna ya kufanya CPR mfanyie mgonjwa na kama hujui endele
kumkandamiza sehemu hiyo ya kifua hadi msaada utakapowasili au hadi mgonjwa
atakapopata fahamu au kuonyesha dalili za kupumua.
Matibabu ya ugonjwa wa mshituko wa
moyo hufanyika hospitali kwa njia tofauti kulingana na hali ya mgonjwa. Kila
dakika inavyopita baada ya kutokea mshituko wa moyo, ndivyo tishu ya moyo
inavyopoteza oksijeni na kuharibika au kufa.
Njia kuu ya kuzuia moyo usiharibike
ni kurejesha tena haraka mzunguko wa damu. Mgonjwa wa mshituko wa moyo huweza
kutibiwa kwa dawa au njia nyinginezo za tiba kwa kutegemea jinsi gani tishu ya
moyo ilivyoharibika.
Dawa tofauti zinazotumika kutibu
mshituko wa moyo ni kama aspirin, dawa zinazoyeyusha damu ili kuondoa damu
iliyoganda ambazo huitwa kitaalamu kama clot buster, dawa aina ya heparin na
nyinginezo ambazo hutofautiana kutokana na utendaji wake mwilini.
Baadhi ya wakati athari za mshituko
wa moyo huwa kubwa ambapo mgonjwa hutibiwa kwa njia inayoitwa Angioplasty. Hiyo
siyo operesheni bali ni matibabu ya kufungua mishipa ya damu iliyoziba au
kudhoofika na kusabisha mshituko wa moyo.
Mara nyingine wagonjwa wa heart
attack hutibiwa kwa upasuaji unaoitwa bypass surgery.
Baada ya kujua namna ya kutibu
mshituko wa moyo.
JINSI GANI TUNAWEZA KUJIEPUSHA NA
UGONJWA HUO WENYE MADHARA MAKUBWA KWA MIILI YETU.
Kwa wale ambao tayari wameshapatwa
na ugonjwa huu pia wanashauriwa kuendelea kutumia dawa walizopewa hospitalini
lakini pia kubadilisha mienendo ya maisha yao ili kuzuia kupatwa tena na
mshituko wa moyo katika siku zijazo.
Kwa wale ambao mshituko wao wa moyo
umesababishwa na
magonjwa mengineyo waliyonayo kama matatizo mengine katika
moyo au maradhi tofauti, wanatakiwa kutibiwa maradhi hayo.
Lakini kwa ujumla tunaweza
kujiepusha kupatwa na ugonjwa huo kwa kutovuta sigara, kudhibiti hali
nyinginezo kama shinikizo la damu, ongezeko la mafuta ya kolestroli mwilini na
kisukari.
Suala jingine linaloweza kuzuia
kupatwa na shinikizo la damu ni kuushughulisha mwili kila mara na kufanya
mazoezi, kupata lishe bora, kupunguza uzito uliopindukia wa mwili na kupunguza
ua kujiepusha na wasiwasi pamoja na msongo wa mawazo.
Kama wewe ni mvutaji wa sigara,
tafadhali acha kuvuta sigara ili ujiepushe kupatwa na heart attack na kama
unaishi katika mazingira ambayo kuna mtu au watu wanaovuta sigara, basi
washauri wenzako waache kuvuta sigara kwani sio tu tabia hiyo huathiri afya zao
bali yako wewe pia. Vile vile matumizi ya tumbaku yana taathira kama ya sigara
kwenye moyo.
Tunashauriwa kufanya mazoezi kwa uchache dakika 30 kwa wiki ili
kujiepusha na ugonjwa wa moyo.
Mazoezi hayo yanaweza kuwa ya aina
yoyote hata kutembea kwa mguu. Hii ni katika hali ambayo, lishe ina nafasi
muhimu katika kuwaepusha watu kuwa na unene wa kupindukia na hivyo kutokupata
mshituko wa moyo.
Dakta Linda Van Horn mtaalamu wa
lishe na mjumbe wa Kamati ya Lishe ya Jumuiya ya Moyo ya Marekani ambaye pia ni
mhadhiri wa tiba ya kuzuia maradhi katika Chuo Kikuu cha Tiba cha Northwestern
huko Chicago anashauri kuwa, ili kujikinga na mshituko wa moyo tunapaswa kula
vyakula vyenye ufumwele kwa wingi na visivyokuwa na mafuta mengi ili kuimarisha
afya ya mioyo yetu.
Wataalamu wanasema kuwa, mafuta
yasiyo na madhara au unsaturated fats kama vile fati asidi za omega 3 na mafuta
ya zaituni huweza kusaidia kupunguza kiwango cha mafuta yenye madhara katika
miili yetu, kuzuia damu kuganda na pia kufanya chembe za mafuta zisigande
katika mishipa ya damu.
Lishe iliyo na ufumwele ambayo mara
nyingi hupatikana katika nafaka, baadhi ya matunda na mboga, husaidia kupunguza
kolestroli aina ya LDL ambayo ni hatari kwa miili yetu.
Baadhi ya vyakula vyenye uwezo wa
kuimarisha afya ya mioyo yetu ni samaki hasa aina ya sardine na salmon. Samaki
hao wana kiwango kikubwa cha omega 3 pamoja na calcium na niacin ambazo ni
virutubisho muhimu kwa afya zetu. Chakula kingine ni shayiri yenye ufumwele kwa
wingi na pia huupatia mwili nguvu kwa haraka na kuzuia njaa kwa muda mrefu.
Utafiti umeonyesha kwamba kunywa
kikombe kimoja tu cha kahawa kwa siku kunapunguza hatari ya kupatwa na mshituko
wa moyo.
Utafiti huo uliotolewa katika
Kongamano la Jumuiya ya Mshituko wa Moyo la Kimataifa nchini Marekani, umeeleza
kwamba kunywa kikombe kimoja cha kahawa ya kawaida na isiyokuwa na kafeini kila
siku huzuia kupatwa na mshituko wa moyo kwa asilimia 30.
Hata hivyo wataalamu wameonya kuwa
kutumia sana kinywaji hicho matokeo yake yanaweza kuwa kinyume. Utafiti
mwingine umeonosha kuwa, kufanya mazoezi kwa muda mrefu hakuhusiana na kuongeza
hatari ya kupata ugonjwa wa moyo.
Huko nyuma kulikuwepo tafiti
zilizoonesha wasiwasi wa afya ya mishipa ya moyo kwa baadhi ya wanamichezo wa
Olimpiki.
Tafiti hizo zilisema kwamba,
kupanuka kwa mioyo ya wanamichezo kunakoitwa kitaalamu "athlete's
heart" huufanya moyo kuwa dhaifu sana na kushindwa kuvumilia mazoezi
mazito. Lakini kwa mujibu wa uchunguzi uliochapishwa kwenye jarida la Marekani la
Kitengo cha Magonjwa ya Moyo, mazoezi mazito hayana hatari kwa afya ya moyo.
Kiwango cha damu inayosukumwa
katika miili ya wanamichezo hakibadiliki wakati wa mazoezi. Mbali na kupanuka
kidogo baadhi ya sehemu za moyo, misuli ya moyo hubakia sawa wakati wa mazoezi.
Wanasayansi wamehitimisha kwamba,
mioyo ya wanamichezo ina afya nzuri na inaweza kuvumilia kirahisi mazoezi ya
kiwango cha juu. Pia wamesema kwamba, baadhi ya dawa kama vile
erythropoietin
(EPO) zinazotumiwa na wanamichezo hao ili kuzipa nguvu chembe chembe nyekundu
za damu, kunaufanya utendaji kazi wa moyo udhoofu, suala ambalo limekuwa
likiwaathiri wanamichezo hao na wala sio mazoezi mazito ya mwili wanayoyafanya.
Sio vibaya ukijua kuwa,
moyo ulioko katika kifua cha
mwanadamu hupiga mara 100,000 kwa siku,
husukuma galoni mbili za damu kwa
dakika,
galoni 120 kwa saa na hufanya hivyo
kwa masaa 24 kwa siku, miezi na miaka yote mwanadamu anayoishi duniani.
Mfumo wa mishipa ya damu ambayo
husafirisha damu katika mwili wa binadamu ina urefu wa maili 60,000. Ukubwa huo ni mara mbili zaidi ya mzunguko wa dunia!
husafirisha damu katika mwili wa binadamu ina urefu wa maili 60,000. Ukubwa huo ni mara mbili zaidi ya mzunguko wa dunia!
Suala la kustaajabisha zaidi na unalopaswa kujua kuhusiana na kiungo hiki muhimu katika mwili wa binadamu ni kwamba moyo huanza kupiga katika mwili wa mtoto mchanga pale anapoumbwa tumboni, hata kabla ubongo haujaumbwa.
Moyo huanza kupiga kabla hata ya
mfumo wa fahamu wa kati kuumbwa!
Kuna nadharia maarufu kwamba mfumo
wa kati wa fahamu (CNS) hudhibiti na kusimamia vitendo vyote vya mwanadamu
kuanzia kwenye ubongo lakini utafiti umeonesha kwamba mfumo wa fahamu
hauanzishi mapigo ya moyo.
Kiuhakika mapigo ya moyo huanza yenyewe na kuna
wanaosema kuwa bado haijafahamika mapigo ya moyo huanzishwa na nini.
Wataalamu wanasema kuwa moyo ni
kituo cha ufahamu (consciousness) na wala sio ubongo kama wengi tunavyodhani.
0 comments:
Post a Comment