Thursday 8 May 2014

MAWE KATIKA KIBOFU CHA MKOJO



Tatizo la mawe katika kibofu cha mkojo (Gallstones),

linazidi kushika kasi kwa kuwasumbua watu wengi kuliko ilivyokuwa awali. Vitu kama mitindo ya

maisha na vyakula tunavyokula, vinatajwa kuwa chanzo kikuu cha tatizo hili. Kwa kuzingatia hilo, makala haya yameandaliwa kujaribu kuchambua Gallstones ni nini, husababishwa na nini na matibabua yake.Gallstones ni nini?

Gallstones
ni vimawe vidogovidogo vinavyopatikana kwenye kibofu cha mkojo au kwenye nyongo ambavyo humsababishia mgonjwa maumivu makali. Vimawe hivi vinaweza kugawanywa katika makundi makuu matatu.

Cholestrol Gallstones (Mawe ya Lehemu)
Haya husababishwa na ulaji uliokithiri wa vyakula vyenye Cholesrtol ambapo ikiingia kwenye mzunguko wa damu, hujikusanya na kisha kuganda kwenye kibofu ambapo baada ya muda hubadilika na kuwa vimawe vigumu.


Black Pigment ( Pigmenti nyeusi)
Haya husababishwa na kuharibiwa kwa kiwango kikubwa cha chembe nyekundu za damu (red blood cell) ambapo mabaki ya seli hizo hujikusanya kwenye kibofu na kuganda, kisha kutengeneza vimawe vigumu vyenye rangi nyeusi.


Brown Pigment (Pigmenti za Kahawia)
Haya husababishwa na kurundikana kwa uchafu katika kibofu cha mkojo. Wanywaji wa pombe na wavutaji wa sigara wapo katika hatari kubwa ya kupata aina hii ya mawe kwenye kibofu.Uwepo wa mawe haya kwenye kibofu husababisha maumivu kama ya moto kuwaka tumboni, tumbo kujaa gesi na kunguruma, mwili kukosa nguvu, homa kali na kama mgonjwa asipotibiwa, husababisha kifo.


DALILI ZA TATIZO
Tatizo hili linapoanza, huwa hakuna dalili za moja kwa moja, na mtu anaweza kukaa na mawe hayo kwa miaka kadhaa bila kuhisi chochote. Dalili huanza kuonekana yanapoongezeka ukubwa na kufikia kiwango cha milimita 8. Dalili za awali huwa ni kuhisi maumivu makali upande wa kulia, juu ya tumbo.Maumivu haya huambatana na


kichefuchefu cha mara kwa mara na kutapika mfululizo. Dalili nyingine ni maumivu makali katikati ya mabega, upande wa mgongoni hasa nyakati za usiku.Pia kushindwa kula vyakula vyenye mafuta ni dalili nyingine ya tatizo hili. Mtu mwenye mawe kwenye kibofu, anapokula chakula chenye mafuta, hata kwa kiwango kidogo, hupatwa na kichefuchefu, tumbo hujaa gesi na wakati mwingine hutapika nyongo.


MADHARA
Uwepo wa mawe katika kibofu, husababisha ugonjwa uitwao Cholecystitis ambao huendana na kurundikana kwa nyongo katika kongosho, hali ambayo husababisha tatizo lingine la utumbo kushambuliwa na bakteria hususan Escherichia coli au Bacteroides.


Mawe haya husababisha madhara zaidi kwa kuziba mirija mbalimbali ndani ya mwili, ikiwemo mirija ya mkojo, hali ambayo kitaalam huitwa Cholangitis au Pancreatitis. Hali hizi huwa hatari sana kwa uahi na husababisha kifo kwa mgonjwa endapo atachelewa kupatiwa matibabu


.UCHUNGUZI WA TATIZO
Ugonjwa wa mawe katika kibofu au nyongo, hupimwa kwa kutumia mbinu za kitaalam ambazo ni:
Ultrasound: Mionzi maalum hutumika kuangalia viungo vya ndani ya tumbo, hasa kibofu na nyongo kuangalia kama kuna vitu visivyo vya kawaida. Majibu ya Ultrasound pekee hayatoshi kutoa majibu ya mwisho, bali daktari atayaunganisha na majibu ya vipimo vingine.


Oral Cholecystogram (OCG): 
Hii ni mbinu ambayo mgonjwa anapewa vidonge maalum ambavyo vikigusana na mawe ndani ya tumbo, hubadilika rangi na kufanya iwe rahisi kwa mawe hayo kuonekana kwenye kipimo cha tatu, X- Ray.

X Ray: Baada ya mgonjwa kumeza vidonge, picha za X Ray zikipigwa huonesha mahali mawe yalipo, ukubwa na jinsi yalivyokaa.
Baada ya vipimo hivi, daktari anaweza pia kushauri mgonjwa apimwe damu ili kupata taarifa kamili juu ya afya yake.

MATIBABU
Hakuna matibabu ya moja kwa moja ya tatizo hili. Baada ya uchunguzi wa tatizo, daktari na mgonjwa wataamua mbinu ya matibabu inayofaa lakini kama hali ya mgonjwa ni mbaya, hakuna mbinu nyingine inayoweza kufaa zaidi ya upasuaji ambapo kifuko cha nyongo hukatwa na kutolewa kabisa 


(Cholecystectomy).
Kama mgonjwa ana hali ya kawaida, tiba mbadala kama kufunga (fasting), kunywa maji na juisi kwa wingi, kuepuka vyakula vyenye mafuta na sukari kwa wingi, husaidia sana kupunguza athari za ugonjwa huo.
Dawa za Acetaminophen pia hupunguza maumivu ingawa ni kwa muda.

0 comments:

Post a Comment