Wednesday, 7 May 2014

SIRI YA PAPAI KATIKA UREMBO WAKO

TUNDA la papai lina vitamini C na E,  lina siri kubwa ya urembo na hutumika kutengeneza facial za aina mbalimbali.
Papai limekuwa likitumiwa kama tunda kwa kula lakini pia kwa kupaka na humfanya mtu awe na ngozi ya asili.
Bidhaa ambazo 
zimekuwa zikitengenezwa kwa kutumia tunda la papai ni pamoja na sabuni, losheni, tona, moisturiza, ‘facial peels’ na nyingine nyingi. Ukitumia facial mask ya papai utakuwa na sura nzuri ya asili na kukupa muonekano mzuri wa uso wako.
Facial mask 
hii huweza hutumika kwa watu wa umri na aina yoyote ya ngozi. Facial mask ya papai ina nguvu ya kung’arisha uso wako.
Mask ya mchanganyiko wa papai na yai ni nzuri katika kuhakikisha kuwa unakuwa na ngozi nzuri na nyororo. Njia hii pia husaidia hata wale wenye nyuso za mafuta ambao wamekuwa wakisumbuliwa na chunusi mara kwa mara kwa kufanya ngozi kuwa kavu.
Utengenezaji:
Chukua papai, likate kisha toa mbegu na ulisage kwa kutumia blenda au pondaponda kwa kinu kisha weka mchanganyiko huo kwenye chombo ulichokichagua kama kikombe au bakuli.
Vunja yai na koroga kuhakikisha kuwa mchanganyiko huo umechanganyika vizuri. Safisha uso wako kwa kutumia cleanser au maji ya vuguvugu na uondoe uchafu wote ulioganda usoni.
Kisha paka mask kuzunguka uso 
wako na unapopaka hakikisha kuwa, mchanganyiko huo haugusi macho yako. Osha uso wako baada ya dakika 15 kwa kutumia maji ya vuguvugu. Jifute kwa kutumia taulo safi.
Unaweza kupaka losheni unayotumia baada ya hapo. Husaidia kutunza ngozi na kuondoa vipele na uchafu ulioganda usoni.

0 comments:

Post a Comment