Sunday, 11 May 2014

SARATANI YA NGOZI AINA YA MELANOMA NI HATARI KIASI GANI?



Tangu tuanze 
kuichambua mada hii ya maradhi ya saratani ya ngozi, tumeangazia mambo

mbalimbali ikiwamo saratani ni nini, aina za saratani, makundi ya watu yanayoathiriwa zaidi na

saratani hii ya ngozi.
Saratani si tu  kwamba ni ugonjwa  hatari lakini pia ni ugonjwa unaompa mwanadamu mateso

makali. Haijalishi ni saratani ya ngozi, ya tumbo au ya kizazi.
 Vilevile ni ugonjwa ambao matibabu yake yanahitaji gharama kubwa mno. Inasemekana kuwa

mgonjwa mmoja wa saratani 

ambaye saratani yake imechelewa kugundulika, huhitaji kiasi cha Sh

300,000 kwa ajili ya matibabu.
 Tatizo jingine ni kuwa kutokana na elimu duni, Watanzania wengi hushindwa kupima saratani na

kuigundua mapema hivyo hugundulika katika hatua za mwisho.
Leo tutachambua kwa undani ukubwa wa tatizo hili kwa kuangalia ni ugonjwa wa hatari kiasi gani.
Melanoma ni saratani ya hatari sana kwa maisha ya mwanadamu. Ni mara chache sana saratani

hii hushambulia watu lakini inapotokea mtu akapata saratani hii basi maisha yake yanakuwa

hatarini sana.
Saratani hii si rahisi kuigundua ukilinganisha na saratani nyingine za ngozi nilizokwisha taja hapo juu.
Siyo tu kwamba saratani hii ni ngumu kidogo kuitambua lakini pia husambaa haraka zaidi kuliko

Saratani nyingine za ngozi.
Melanoma huweza kusambaa na kushambulia viungo vingine zaidi ya ngozi kama mifupa na

ubongo. Inapofikia hatua hii saratani hii inakuwa ngumu sana kutibika.

Dalili za Melanoma
Dalili ya kwanza kabisa ambayo inabidi kila mtu afahamu ni kubadilika kwa ukubwa, rangi au ule

muundo wa alama ya ngozi ambayo umekuwa nayo kwa muda mrefu au umezaliwa nayo. Alama hii

ni ile ambayo ina rangi nyeusi zaidi ukilinganisha na maeneo mengine ya ngozi.

Mabadiliko haya si lazima yawe yanatokea haraka haraka yanaweza kuwa yanatokea taratibu

katika kipindi cha miezi lakini cha muhimu ni kuwa unaona kabisa mabadiliko kwenye alama hiyo ya

ngozi.

Ni muhimu sana kutambua mabadiliko haya. Mabadiliko mengine ni kama yafuatayo
Pamoja na mabadiliko niliyokwisha taja hapo juu alama hii inaweza kuwa inavimba,

kingo zake zinapoteza mzingo wake wa kawaida,

alama inakua zaidi kwa eneo (mfano kutoka mzingo wa 4 mm inakuwa kubwa na kuzidi 6 mm).

Alama inaweza kuanza kuwasha kama mgonjwa atachelewa kugundua tatizo basi dalili zifuatazo

huonekana:

Alama ya kwenye ngozi kupasuka na kufanya kidonda

Alama kutoa damu

Kuwa na maumivu kwenye alama

Kama matibabu hayatofanyika basi saratani hii husambaa na dalili zifuatazo huweza

kuonekana :

Tezi za mwili kuvimba (hususan zilizo kwenye makwapa na kwenye nyonga)

Uvimbe kwenye ngozi

Kupoteza uzito kwa kasi bila kujua sababu

Kikohozi kisichoisha

Kupoteza fahamu (Kifafa)

Kichwa kuuma

Related Posts:

  • SARATANI YA TEZI YA THYROID (THYROID CANCER) Hii ni aina ya saratani inayokumba tezi ya thyroid. Ikumbukwe kuwa tezi ya thyroid ipo sehemu ya mbele ya shingo ya mwanadamu ikiwa na sehemu mbili (lobes) moja kila upande wa shingo.Visababishi na ukubwa tatizoSaratani … Read More
  • HIVI NDIVYO FANGASI WANAVYOSHAMBULIA SEHEMU ZA SIRI!! LEO tuangalie fangasi wanaoshambulia sehemu za siri, yaani Tinea cruris. Aina hii ya fangasi ndiyo inayofahamika na Watanzania wengi zaidi ya aina nyinginezo na waathirika huwashwa sana sehemu za siri. Dalili zake… Read More
  • UGONJWA WA SARATANI YA NGOZI (MELANOMA) LEO tutachambua kwa undani saratani ya ngozi iitwayo Melanoma kwani saratani si tu kwamba ni ugonjwa hatari lakini pia ni ugonjwa unaompa mwanadamu mateso makali kutokana na maumivu anayoyapata. Maumivu hayo huyapata… Read More
  • MARADHI YA UGONJWA WA KIMETA ( ANTHRAX) Kimeta ni ugonjwa wa hatari unasababishwa na vimelea vya bacteria. Bacteria hawa hujulikana kama  Bacillus anthracis,bacteria ambao wana uwezo wa kufanya mbengu.Mbegu hizi ni seli ambazo huweza kukaa kwa miaka kadh… Read More
  • UGONJWA WA NGOZI TUTUKO ZOSTA HERPES ZOSTER Tutuko zosta "Zoster" inaelekezwa hapa. Kwa the ancient Greek article of dress, tazama Zoster (costume). "Shingles" inaelekezwa hapa. Kwa matumizi mengine, tazama Shingle (disambiguation). Herpes zost… Read More

0 comments:

Post a Comment