Huu ni
ugonjwa unaothiri sehemu inayofunika ubongo na uti wa mgongo, yaani utandu.
Ubongo unafunikwa na sehemu au tandu tatu nyembamba za seli ili kuitengenisha
na fugu la kichwa. Tandu hizi zinaweza kuathirika na kusababisha hali
inayojulikana kama uvimbe wa utandu wa ubongo na uti wa mgongo.
Kwa
sababu tandu zilizoathirika ziko karibu na ubongo, uvimbe wa utandu wa ubongo
huwa na athari kwenye ubongo na hata kazi zake kama vile kuona, kusikia,
kukumbuka, uwezo wa kutembea, uwezo wa kuzungumza na uwezo wa kukumbuka.
NI NINI HUSABABISHA
UGONJWA HUU?
Aghalabu
husababishwa na bacteria, lakini pia huweza kusababishwa na viumbehai kama
virusi na fungi Bakteria hii hupumuliwa ndani na hupenya kupitia damu na
kuathiri ubongo na uti wa mgongo. Huambukiza haraka sana/husambaa haraka sana
katika maeneo ambapo kuna msongamano mkubwa na hii inaweza kugeuka kuwa mlipuko
wa magonjwa.
MLIPUKO NI NINI?
Mlipuko
ni ugonjwa unaoambukiza haraka na huathiri watu wengi kwa wakati mfupi sana.
Mlipuko, aghalabu hutokea katika sehemu/maeneo makubwa ambapo huishi kariby
sana hususan karibu na kambi za wanajeshi, kambi za wakimbizi, katika shule za
bweni na kadhalika. Milipuko ya magonjwa hutokea mara moja moja miongoni mwa
jamii mbalimbali/tofauti tofauti kwa wakati tufauti tofauti kwa mwaka.
NI NANI ALIYE KATIKA
HATARI YA KUPATA UGONJWA HUU?
Kila
mtu hupo katika hali ya hatari kuambuwa na kuugua wakati wa mlipuko/mkurupuko
huu. Huambuza kirahisi na harka kutoka kwa mtu mmoja hadi mwengine.
Ilivyo
kwenye magonjwa yote, ugonjwa wa utandu wa ubongo huathiri sana watoto walio
chini ya miaka 5 pamoja na wakongwe. Wale walio na kinga duni k.v wale wanougua
ugonjwa wa sukari, saratani, ukimwi, pia wapo katika hali ya kupata ugonjwa wa
utandu wa ubongo na uti wa mgongo.
NITAJIZUIA VIPI ILI
NISIPATE UGONJWA HUU?
Uzuiaji
nzuri ni kupitia chanjo. Lazima watoto wote wachanjwe ili kupunguza hatari ya
kuugua ugonjwa wa utandu wa ubongo.
Hata
wakati wa mkurupuko wakati mwingine kuna chanjo ya kizuia maambuzi ya ugonjwa
huu.
Kwa
sababu ugonjwa huu huambukiza kutoka na kukaribiana kwa watu, ni muhimu
kuzingatia usafi na kuwa mbali na waathiriwa wa ugonjwa wakati wa kuwatazama,
kuwajulia hali ama kuwaliwaza.
Msongamano
wa watu ndicho chanzo muhimu cha kuenea na kusambaa kwa ugonjwa huu kutoka kwa
mtu mmoja hadi mwengine. Katika kupunguza msongamano karibu na wewe, pia
unahitajika kupunguza uwezo wa kuzuia magonjwa mengine mbali na utandu wa
ubongo.
NITATAMBUAJE NINAPOUGUA
UGONJWA HUU? (DALILI NA ISHARA)
Ugonjwa
huu huwa na joto la hali ya juu, shida ya kuona au kuepuka mwangaza, basi ni
bora uende kwenye hospitali iliyo karibu nawe haraka iwezekanavyo. Hii ni muhim
sana panapokuwa na mlipuko wa utandu wa ubongo na utu wa ubongo. Hii ni kwa sababu
ugonjwa huu huambuza kwa kasi sana.
Usikawie
ni vema kuwa na afya badala ya kujuta.
JE, KUNA TIBA YA UGONJWA
HUU?
Ndiyo:
huu ni ugonjwa unaosababishwa na bacteria na kuna dawa za kupambana na magonjwa
yababishwayo na hewa katika hospitali zote, ambayo yanaweza kutiba ugonjwa wa
utandu wa ubongo kabisa. Dawa hizi hutumiwa kupitia sindano mara nyingi kwa
siku na lazima sindano hizi ziendelee kwa kipindi cha wiki/majuma mawili hadi
matatu.
Iwapo
kuna kukawia kufika hospitalini, dawa hiyo haiwezi kusaidia kutibu mgonjwa
ambaye amezidiwa na ugonjwa huu. Haitafanya kazi kwa vyovyote vile. Kwa hivyo
ni muhimu kuenda hospitalini kwa wakati unaofaa dalili zinapoonekana.
KUTAKUWA NA UBAYA GANI
IWAPO SIPATI MSAADA? (MATATIZO)
Ugonjwa
wa utandu wa ubongo huambukiza haraka na kwa sababu ni hatari, husabisha kifo
iwapo hautibiwi. Wagonjwa wote wa utandu wa ubongo lazima walazwe hospitalini
kwa sababu huzingatiwa kuwa dharura ya kimatibabu. Aghalabu, hili hujiri
mgonjwa anapoenda hospitalini akichelewa ili kupata matibabu.
Madhara
hufungamana na utendakazi wa ukongo na huhusisha upofu, usiwi na kutoweza
kutumia mikono na miguu vizuri, kutozungumza kwa ufasaha and nafuu siyo nzuri.
NITAMTUNZA VIPI MTU
AMBAYE ANAUGUA UGONJWA HUU (UTANZAJI WA NYUMBANI)?
Haushauriwi
kumtunzia mgonjwa wa utandu wa ubongo nyumbani. Hii ni dharura ya kimatibabu
inayostahili kutatuliwa hospitalini kati ya wiki 2-3. Iwapo unashuku kwamba
Fulani wanaugua ugonjwa huu, wapeleke hospitalini haraka iwezekanavyo.
Wanapokuwa
kwenya matibabu na sasa wamerudi nyumbani, husalia kuwa wanyonge. Kwa Hivyo
vema kwao kutunzwa. Sharti chakula chao kiwe chepesi chenye na virutubishi wape
kiasi kidogo kila baada ya saa mbili. Hii ni kwa sababu hamu yao ya chakula
imerudi chini. Watie moyo wagonjwa ambao wana madhara kutokana na ugonjwa huu.
HOJA MUHIMU KUHUSU
UGONJWA WA UTANDU WA UBONGO
·
Utandu ni ugonjwa wa ubongo na uti wa mgongo unaotibika.
Husambaa haraka sana katika maeneo palipona msongamano na iwapo hautatibiwa.
·
Huathiri sana sana watoto an wakongwe lakini wakati wa
mlipuko/mkumpuko huathiri vijana wanaume na wanawake wape watoto kinga kupitia
chanjo.
·
Dalili za ugonjwa wa utandu, joto la hali ya juu, kutapika,
kuumwa kichwa na kuepuka mwangaza. Kupitia kwa shingo huwa dalili ya mwisho.
Watoto walio chini ya miaka 2 wanaweza kuwa na joto tu pamoja na kulia.
·
Ugonjwa wa utandu unaweza kuua kati ya saa au siku chache. Iwapo
unaushuku, mkimbize mtoto au mtu mzima hospitalini kwa ajili ya kupimwa.
Wanaweza kulazwa kwa ajili ya matibabu.
0 comments:
Post a Comment