Thursday 8 May 2014

MAGONJWA NA TIBA YA FANGASI WANAOSHAMBULIA SIRINI ( TINEA CRURIS)


Kabla ya kueleza tiba tufafanue kwamba kuna baadhi ya mambo yanayosababisha watu kuwashwa sehemu hizo nyeti kama vile kuwa na fangasi tuliowataja hapo juu.

Wengine huwashwa kutokana na kutumia dawa za antibayotiki kwa muda mrefu.
Kutumia dawa hizo husababisha fangasi kwani huua wadudu wote wanaolinda mwili na kuacha sehemu ya siri kukiwa hakuna kinga.
Dawa za antibayotiki ni kama, ampicillini amoxyclini, ciproflaxine, doxylline, erythromycine, gentamcycine na nyingine nyingi hivyo basi, jamii isitumie ovyo dawa hizi bila ushauri wa daktari.

Sababu nyingine ni unene kupita kiasi. Mtu akinenepa anaweza kupata fangasi kwa sababu unene husababisha jasho sehemu za siri na kuongeza unyevunyevu sehemu hizo pia michubuko kutokana na kubanwa na chupi.
Sababu zingine ni utumiaji wa dawa ya jamii ya steroid, dawa hizi ni kama prednisoline, hydrocortisone, dexameltasone na nyingine nyingi. Hizi nazo hupunguza kinga ya mwili na kusababisha fangasi kuzaliana kwa wingi sehemu nyeti.

Pia kuna magonjwa yanayosababisha kupungua kwa kinga nayo ni kisukari, Ukimwi na magonjwa mengine yanayopunguza kinga ya mwili na kusababisha fangasi.
Kuwepo na joto kupita kiasi na kuvaa nguo za ndani ambazo hazijakauka pia husababisha fangasi sehemu za siri.

Dalili
Dalili kwa maradhi ya fangasi hutofautiana kati ya mtu na mtu ila dalili kubwa ni kutokwa na majimaji meupe wakati mwingine kama mgando wenye rangi ya njano ukiwa umeambatana na muwasho  sehemu za ndani au kwenye mashavu  ya sehemu za nje za siri za mwanamke.
Nje ya sehemu hizi za siri hutokea wekundu na maumivu wakati wa kukojoa au wakati wa tendo la ndoa pia mgonjwa atajikuta akikojoa mara kwa mara.

Tiba na ushauri
Fangasi hutibika vizuri na mgonjwa kupona ila ni vizuri akaenda hospitali na kufanyiwa kipimo cha mkojo ambapo chembechembe za yeast huonwa vizuri kwenye darubini.
Daktari akigundua mgonjwa ana maradhi haya ataweza kumpa dawa zenye uhakika.Usinunue dawa hovyo na kutumia utasababisha usugu wa fangasi, hivyo kutopona.
Mgonjwa ahakikishe sehemu iliyoathirika 
inakuwa kavu masaa 24 na apake poda yoyote ya kutibu fangasi asubuhi na usiku kwa wiki 4 mfululizo.
Mgonjwa, kwa ushauri wa daktari atameza dawa za antibayotiki kama vile cloxacillin 250mg (2 x 3 siku 5) kama sehemu yenyewe imekuwa kama kidonda ili iweze kukausha haraka, anashauriwa asivae boxer/chupi bali avae bukta 

yenye kuruhusu hewa kupita na ajikaushe vizuri baada ya kuoga.
Ushauri pia unatolewa kwa mgonjwa asitumie sabuni zenye dawa kwani zitamsaidia kwa muda lakini zitafanya ngozi kupoteza uwezo wake wa asili wa 

kujilinda dhidi ya vijidudu na ahakikishe anabadili nguo ya ndani kila siku na iwe safi iliyopigwa pasi.
Kwa ushauri wa daktari 
mgonjwa anaweza kutumia ‘cream’ iliyo kwenye tyubu inayoitwa Quadrimerm  au fluocinonide cream kwa wiki mbili kwa kupaka sehemu iliyoathirika ikiwa kavu na akae dakika 30 kabla ya kuvaa nguo.

0 comments:

Post a Comment