HAPA hutokea hali ambayo nyama zinaota na kukua kama tabaka au ukuta mwingine juu ya misuli ya kizazi ‘Ectopic Glandular tissues’.
Awali tatizo hili liliitwa kitaalamu ‘Endometriosis Interna ingawa tatizo hili kwa kiasi kikubwa linatofautiana na ile hali ya tabaka ya ndani ya kizazi kuwa nje. Endometriosis.
Mwanamke mwenye tatizo hili
hutokewa na hali tofauti kama tutakavyokuja kuona na husababisha awe mgumba kabisa kwa kupoteza kabisa uwezo wa kuzaa kama hapo awali hajawahi kuzaa.
Tatizo huwapata zaidi wanawake
walio na umri wa kati ya miaka 35 hadi 50. Ingawa katika hali isiyo ya kawaida hutokea katika umri wa chini ya miaka 35.
Mwanamke ambaye hajawahi kushika ujauzito hadi kufika umri huo ana nafasi kubwa ya kupata tatizo hili tofauti na mwanamke ambaye ameshawahi kuzaa chini ya umri wa miaka 35.
Hali hii ya kuvimba kwa kizazi inapotokea huambatana na kutokwa na damu nyingi wakati wa hedhi na kupata maumivu makali unapokuwa katika hedhi.
Maumivu huongezeka zaidi
pale lile tabaka la ndani la kizazi linapojikita katikakati ya misuli ya kizazi kwa hiyo unaweza kupata maumivu makali ya tumbo chini ya kitovu muda wote pasipo kupata damu ya hedhi hata kama tarehe za kupata damu zinafika. Vilevile damu ya hedhi inaweza kutoka kwa wingi.
Katika tatizo hili,
kizazi kinaendelea kuvimba kutokana na tabaka la ndani ‘Basal Endometrium’ kujipenyeza ndani ya misuli ya kizazi hivyo kusababisha kila siku kizazi kiendelee kukua kama una ujauzito na huwa kigumu.
Tatizo hili ni tofauti sana na kuwa na uvimbe wa fibroid.
Kizazi kinapoendelea kukua mwanamke uhisi ujauzito ukielemea upande wa chini wa nyonga kama tutakavyokuja kuona.
Dalili za ugonjwa
Wanawake wengine wemye tatizo hili huwa wahaonyeshi dalili zozote huku kizazi kikizidi kuvimba na wengine uhisi maumivu makali ya kizazi muda wote au wakati wa hedhi.
Chembechembe
za tabaka la ndani la kizazi zinapojikita katika misuli ya kizazi, huendelea kutoa damu hivyo kusababisha damu kuvuja ndani kwa ndani ya tabaka la kizazi bila damu hiyo kutoka kwa nje.
Mwanamke uhisi kama anapata uchungu wa uzazi na kama kuna kitu kinashuka ukeni kwa kuhisi shinikizo ukeni kama kuna kitu kinasukumwa.
Dalili nyingine
ambazo humuathiri mwanamke mwenye tatizo hili kuwa na maumivu chini ya tumbo muda wote na kila akienda katika zahanati huambiwa ana yutiai kitu ambacho siyo sahihi na kila akitumia dawa tatizo linabaki palepale au anapata nafuu ya muda mfupi.
Maumivu pia huwa makali
pale mwanamke anapokuwa katika kipindi cha upevushaji mayai ‘ovulation au anapokuwa katika hedhi.
Wakati wa hedhi hupata maumivu makali sana huku tumbo likibana au
kukaza hali iitwayo ‘Abdominal eramps’ na muda wote hutamani aendelee kuinama tu.
Uhisi mkojo kila wakati kutokana na kibofu kugandamizwa kunaposababishwa na shinikizo la kizazi.
Maumivu husambaa kuanzia mapajani kushuka chini hadi miguuni. Damu hutoka kwa wingi sana na wakati mwingine hata pedi hazitoshi.
Damu hutoka kwa mabonge mabonge na huendelea tu kutoka kwa siku nane hadi kumi na nne, aidha taratibu au kwa wingi hadi kusababisha alazwe hospitali.
Chanzo cha tatizo
Chanzo halisi cha tatizo hili kusababisha tabaka la ndani la kizazi kujikita katika misuli ya kizazi bado hakijulikani, ingawa kwa misuli ya kizazi ‘Uterine trauma’ huchangia hali hii kwa kuondoa ukingo wa tabaka la ndani la kizazi kuelekea katika misuli ya kizazi.
Hali ya kuumia kizazi hutokea wakati wa upasuaji wa uzazi ‘Siza,’ wakati wa kufunga kizazi kwa kukata mirija, utoaji wa mimba na kusafisha kizazi au endapo utakuwa mjamzito huku tatizo la mabadiliko ya tabaka la ndani litakuwa limeanza.
Uchunguzi na tiba
Hufanyika katika kliniki za magonjwa ya kinamama kwenye hospitali za mikoa na wilaya.
Vipimo kama Ultrasound na ikibidi MRI kitafanyika ili kuthibitisha tatizo.
Matibabu inaweza kuwa dawa hasa dawa za homoni kutegemea na
ukubwa wa tatizo. Tiba nyingine ni upasuaji hasa wa kuondoa kizazi.
Endapo mwanamke atapata ujauzito ikiwa tayari tatizo hili linaanza basi mimba inaweza kutoka na akapata uchungu mapema kabla ya muda wake.
0 comments:
Post a Comment