Thursday, 1 May 2014

KUJIPUMZISHA MCHANA KUNAIMARISHA AKILI.


Uchunguzi mpya umeonyesha kuwa kulala
kidogo wakati wa mchana huimarisha ubongo
na kuimarisha uwezo wa kufahamu mambo
mapya.

Profesa Matthew P. Walker wa Kitengo
cha Saikolojia na Sayansi ya ubongo cha Chuo
Kikuu cha Calfornia aliyeongoza uchunguzi
 
huo anasema kwamba, unahitaji kulala kabla
ya kujifunza, ili kuutayarisha ubongo wako ili
uwe kama sponchi kavu linalosubiri kunyonya
taarifa mpya.
 
Akielezea umuhimu wa
kujipumzisha mchana hasa kwa wale
wanaosoma na kujifunza Profesa Walker
anasema kwamba, usingizi sio tu huondoa
 
uchovu na kufuta makosa yanayotokana na
kuwa macho muda mrefu, bali pia
humrejesha mtu pale alipokuwepo kabla ya
 
kulala. Wataalamu wanasema kuwa, kila mtu
anapoongeza masaa ya kukaa macho ndivyo
hivyo hivyo uwezo wa ubongo wake wa
kuelewa mambo unavyopungua.
Professa
Walker akitoa mfano ili kufahamisha zaidi
umuhimu wa kupumzisha ubongo ili
kuongeza uwezo wa kujifunza,
 
anaufananisha ubongo na sanduku la barua
pepe na kusema kwamba iwapo sanduku hilo
litajaa basi hutoweza kupata barua pepe
 
mpya hadi pale utakapoondoa barua pepe
zisizotakiwa au kuzipelekea katika folder
jipya, na kulala nako huusaidia ubongo hivyo
hivyo.

Uchunguzi huo unaunga mkono utafiti wa
huko nyuma unaosema kwamba, kukaa
macho muda mrefu usiku hupunguza uwezo
wa mtu wa kuelewa mambo mapya kwa
 
karibu asilimia 40, kwani baadhi ya sehemu
za ubongo hufunga baada ya kukosa usingizi
kwa muda mrefu.

0 comments:

Post a Comment