Thursday, 1 May 2014

JINSI YA KUISHI NA VIDONDA VYA TUMBO




Kama una vidonda vya tumbo, matibabu
yako yatategemea sababu ya vidonda vya
tumbo. Kama ni bakteria H.pylori, dawa za
kuua na kuondoa bakteria hutumiwa.

Kama ni Non-Steroidal Anti-Inflamantory
Drugs 'NSAIDS' mfano Aspirin & Ibuprofen
utapaswa kutumia Proton Pump Inhibitor
'PPI' mfano Omeprazole & Esomeprazole.
Ingawa matibabu ya siku hizi husisitiza
kuchanganya dawa za kuua bakteria na
Proton Pump Inihibitors 'PPI'.
Mambo yafuatayo yatakusaidia kuishi vizuri
ukiwa na 'Vidonda Vya Tumbo':-
1.     Acha kutumia kahawa na chai, kwa
maana vitu hivi huongeza kiwango cha
asidi kinachotengenezwa na tumbo lako.
Unaweza tumia chai ya mitishamba 'Herbal
tea' kama mbadala.

2.      Kunywa maziwa na ule vitokanavyo na
maziwa kama maziwa mgando 'Yoghurt',
jibini 'Cheese'. Maziwa hufikiriwa kufunika
utumbo na kupunguza athari za asidi ya
tumboni.
3.      Jitahidi kupunguza uzito kama uzito
umezidi na hauendani na kimo chako.
4.      Kula walau kidogo mara kwa mara. Hii
itasaidia kupunguza athari za asidi
inayotengenezwa na tumbo.
5.      Acha au kunywa vileo siku maalumu tu
kwa maana unywaji wa pombe mara kwa
mara hutonesha kwenye vidonda vya
tumbo vinavyotaka kupona.

6.      Epuka matumizi ya viungo vya vyakula
kwa maana hufanya hali kuwa mbaya zaidi.
7.      Acha kuvuta sigara/tumbaku/bangi.
Uvutaji wa sigara utakuweka kwenye hatari
zaidi ya kuanza vidonda vipya na kuzuia
vidonda vingine visipone.

Related Posts:

  • MATATIZO KATIKA NJIA YA HAJA KUBWA TATIZO hili huwapata wanaume na wanawake. Matatizo haya hujitokeza katika hali ya tofauti kutegemea na chanzo halisi. Mfumo wa haja kubwa ni pamoja na mfuko wa kuhifadhia haja kubwa ‘rectum’ na sehemu haja inapokea ‘anu… Read More
  • MAUMIVU CHINI YA KITOVU KWA WANAWAKE NA WANAUME-2 Wiki iliyopita nilianza mada hii ambayo leo nitahitimisha. Maumivu chini ya kitovu hutokea kama ifuatavyo: Yapo yale ya chini ya kitovu katikati, kushoto na kulia. Kwa wanawake maumivu ya kushoto na kulia yapo ya ai… Read More
  • MAUMIVU CHINI YA KITOVU KWA WANAWAKE NA WANAUME TATIZO hili huwakumba watu wengi kwenye jamii lakini kwa bahati mbaya wengi huchukulia ni jambo la kawaida kitu ambacho baadaye husababisha baadhi kuingia kwenye matatizo makubwa ya kiafya hasa kwenye mfumo wa uzazi… Read More
  • MAUMIVU CHINI YA KITOVU KWA WANAWAKE NA WANAUME-3 WIKI iliyopita niliishia kwenye maelezo kuwa secondary dysmenorhea huwakumba akina mama ambao tayari wameshajifungua mtoto mmoja au zaidi lakini wanapatwa na maumivu makali wakati wa hedhi jambo ambalo hawakuwa nalo… Read More
  • SARATANI YA MATITI NA NAMNA YA KUJICHUNGUZA MWENYEWE Saratani ya matiti ni ugonjwa ambao huwapata wanawake na unatokana na athari za chembe ndogo ama seli kwenye matiti na matokeo yake ni kwamba hubadili mfumo wa kawaida wa kukua na kuongezeka. Mabadiliko haya huanza pol… Read More

0 comments:

Post a Comment