Kutumia
maziwa ya mama
Mama
aliyeamua kuchagua kutumia maziwa yake ana njia kuu tatu ambazo anaweza
kuamua
ni ipi itakayomfaa yeye na mtoto wake. Njia hizi ni:
· Kunyonyesha maziwa ya mama pekee tangu mtoto anapozaliwa
hadi miezi sita;
· Kunyonyesha maziwa ya mama kwa muda mfupi (chini ya miezi
sita);
· Kutumia maziwa ya mama yaliyokamuliwa na kuchemshwa.
Kunyonyesha maziwa ya mama pekee tangu mtoto anapozaliwa
hadi miezi 6
Tafiti
zimeonyesha kuwa kumnyonyesha mtoto maziwa ya mama pekee kunapunguza
uwezekano
wa mtoto kupata uambukizo wa virusi vya UKIMWI kutoka kwa mama
yake
ukilinganisha na kumnyonyesha mtoto na wakati huo huo kumpa maziwa
mengine, vinywaji au vyakula vingine. Iwapo mama atachagua
njia hii anashauriwa:
·
Kumnyonyesha mtoto wake
maziwa yake pekee kwa miezi sita ya mwanzo bila ya
kumpa mtoto kitu kingine chochote hata maji. Kumpa mtoto
maziwa mbadala,
vinywaji au vyakula vingine huweza kuongeza hatari ya
uambukizo wa virusi vya
UKIMWI kwa mtoto. Vinywaji au vyakula hivyo huweza
kusababisha michubuko
Kwenye utumbo wa mtoto na hivyo kuruhusu virusi vya UKIMWI
kupenya kwa
urahisi;
·
Kuhakikisha mtoto
ananyonyeshwa kila anapohitaji, usiku na mchana;
·
Kumpakata na kumweka
mtoto vizuri kwenye titi ili kuzuia matatizo ya matiti
yanayoweza kujitokeza, kama chuchu kupata mipasuko au
michubuko. Matatizo
hayo huongeza hatari ya uambukizo wa virusi vya UKIMWI
kutoka kwa mama
kwenda kwa mtoto.
·
Kuacha kabisa kumnyonyesha mtoto baada ya miezi sita. Wakati
huo mama
anaweza kukamua na kuchemsha maziwa yake akampa mtoto, huku
akimpatia vinywaji na vyakula vingine.
Kunyonyesha maziwa ya mama kwa muda
mfupi.
Kumwachisha mtoto kunyonya maziwa ya mama yake mapema
husaidia kupunguza
uwezekano wa mtoto kuambukizwa virusi vya UKIMWI kupitia
maziwa. Kwa
kufanya hivyo muda wa mtoto kuwa kwenye hatari ya uambukizo
wa virusi vya
UKIMWI hupungua.
Iwapo mama mwenye virusi vya UKIMWI atachagua njia hii
anashauriwa kuacha
kumnyonyesha mtoto wake mapema iwezekanavyo kabla ya miezi
sita. Muda
halisi wa kuacha kumnyonyesha mtoto utaamuliwa na mama
mwenyewe kwa kuzingatia uwezekano wa kupata maziwa mbadala na uwezo wa
kuyatumia
ipasavyo.
Mama akumbuke kumnyonyesha mtoto maziwa yake pekee bila
kumpa maziwa
mbadala, vinywaji au vyakula vingine vyovyote. Uchanganyaji
wa maziwa ya
mama na maziwa mbadala, vinywaji au vyakula vingine huongeza
hatari ya
uambukizo wa virusi vya UKIMWI kwa mtoto. Mama anashauriwa
kumpakata na
kumweka mtoto vizuri kwenye titi ili kuzuia matatizo ya
matiti yanayoweza
kujitokeza.
Mama
anapoamua kuacha kumnyonyesha mtoto wake ashauriwe kufanya hivyo
katika
muda mfupi. Ili kuweza kuzuia hatari ambazo zinaweza kujitokeza katika
kipindi
hicho cha mpito au kutokana na mabadiliko ya ghafla, mama ashauriwe
kuanza
kukamua maziwa yake katika wiki mbili kabla ya kumwachisha mtoto na
kumnywesha
mtoto maziwa hayo kwa kutumia kikombe. Hii itamwezesha mtoto
kuweza
kuzoea kutumia kikombe.
Mtoto aliyeachishwa kunyonya maziwa ya mama yake kabla ya
miezi sita apewe
maziwa mbadala au mama akamue maziwa yake na kuyachemsha
kabla ya kumpa
mtoto. Mtoto anyweshwe maziwa hayo mara tano au zaidi kwa
siku, akizingatia
kipimo cha mililita 150 kwa kila kilo ya uzito wake kwa
siku.
Mama anayeamua kuacha kumnyonyesha mtoto wake mapema
anapaswa
kusaidiwa kufanya hivyo kwa ufanisi na usalama ili kuepusha
madhara yoyote
yanayoweza kutokea kwa mtoto.
Mama akiwa na hali mbaya, hasa anapopata magonjwa nyemelezi
na akawa
mgonjwa sana ni vyema aache kunyonyesha.
Kutumia maziwa ya mama yaliyokamuliwa
na kuchemshwa
Virusi vya UKIMWI vilivyoko kwenye maziwa ya mama vinaweza
kuharibiwa kwa
kuchemsha maziwa hayo yaliyokamuliwa. Tafiti zimeonyesha
kuwa virusi hivyo hufa
bila kuharibu kingamwili zilizopo kwenye maziwa iwapo
yatapashwa moto kati ya
nyuzi joto 56°C – 63°C kwa muda wa dakika 20. Lakini katika
mazingira ya kawaida
sio rahisi kupima nyuzi joto hizo hivyo inashauriwa kuacha
maziwa hayo mpaka
yachemke. Mara tu yakichemka yaipuliwe. Kwa kuchemsha maziwa
hayo baadhi ya
kingamwili na virutubishi vilivyomo hupungua. Ni muhimu mama
apate ushauri wa
daktari au mtaalamu wa afya kuhusu virutubishi vya nyongeza
vya kumpa mtoto.
Iwapo
mama ataamua kutumia maziwa yake aliyoyakamua na kuyachemsha yafuatayo
ni
muhimu.
·
Mama aelekezwe njia sahihi
ya kukamua maziwa yake bila ya kusababisha maumivu ya titi lake;
·
Maziwa hayo yachemshwe na
yaipuliwe pindi tu yanapoanza kuchemka;
·
Maziwa hayo yapoozwe kwa
haraka aidha kwa kutumbukiza chombo chenye
·
maziwa ndani ya maji
baridi au kuweka ndani ya jokofu;
·
Mtoto anyweshwe maziwa
hayo kwa kutumia kikombe;
·
Maziwa yachemshwe kiasi cha kutosha mlo mmoja tu.
Maziwa
yaliyochemshwa yasihifadhiwe kwa matumizi ya mlo unaofuata.
·
Mama anapochagua njia hii kama ilivyo kwa njia nyingine
anapaswa kupata unasihi na kusaidiwa.
Kutumia maziwa mbadala
Maziwa
mbadala yanaweza kutumika kumlisha mtoto aliyezaliwa na mama mwenye
virusi
vya UKIMWI. Maziwa mbadala ni pamoja na maziwa yaliyotengenezwa
maalumu
kwa watoto wachanga, maziwa yanayotayarishwa nyumbani kutokana na
maziwa
ya wanyama kama ng’ombe au mbuzi, maziwa ya unga yenye mafuta (dried full
cream milk) au maziwa yaliyochevushwa
(evaporated milk).
0 comments:
Post a Comment