Uambukizo wa virusi vya UKIMWI kutoka kwa mama
kwenda kwa mtoto
Kwa kawaida sio wanawake wote wenye virusi vya
UKIMWI
huwaambukiza watoto
wao. Inakadiriwa kuwa kiasi cha asilimia 60 hadi 70 ya
watoto wanaozaliwa na
wanawake wenye virusi vya UKIMWI hawaambukizwi
kabisa hata kama hakuna hatua
zozote zilizochukuliwa kupunguza uwezekano wa
uambukizo. Inakadiriwa asilimia 30
hadi 40 ya watoto huambukizwa virusi vya UKIMWI ambapo:
·
Asilimia 5 – 10 ya watoto wanaambukizwa wakati wa ujauzito
·
Asilimia 10 – 20 wanaambukizwa wakati wa uchungu na
kujifungua
·
Asilimia 5 – 20 wanaambukizwa wakati wa
kunyonyeshwa
Mambo yanayochangia kuongeza hatari ya uambukizo wa
virusi vya UKIMWI
kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto:
·
Mama kuambukizwa virusi vya UKIMWI wakati wa
ujauzito au wakati wa kunyonyesha. Wakati mama
anapoambukizwa, huwa na virusi vingi mwilini kwa hiyo
uwezekano wa kumwambukiza mtoto ni mkubwa zaidi.
·
Mama kuwa na UKIMWI.
Uwezekano wa kumwambukiza
mtoto ni mkubwa kwani mama atakuwa na virusi vya
UKIMWI vingi mwilini mwake.
·
Mama kuwa na maambukizo ya magonjwa ya ngono wakati
wa ujauzito. Magonjwa ya ngono husababisha
michubuko ukeni ambayo huongeza hatari ya uambukizo wa
virusi vya UKIMWI iwapo mama hafanyi ngono salama.
·
Taratibu zinazotumika wakati mama anapojifungua. Kwa
mfano kuongeza njia ya uzazi, uchanaji mapema wa utandu,
mtoto kunyonywa uchafu baada ya kuzaliwa.
·
Hali ya lishe ya mama. Mama mwenye hali nzuri ya lishe
huwa na mfumo thabiti wa kinga ambao huchelewesha mama
huyo kupata UKIMWI.
·
Hali ya matiti ya mama.
Matiti yenye vidonda au
michubuko, chuchu zinazotoa damu na majipu ya titi
·
Ulishaji wa kuchanganya maziwa ya mama na vinywaji
au vyakula vingine. Vyakula na vinywaji kama maziwa
Ulishaji wa kuchanganya maziwa ya mama na vinywaji
au vyakula vingine. Vyakula na vinywaji kama maziwa
mbadala, maji, chai, uji, maji ya matunda, n.k. huweza
kusababisha michubuko kwenye utumbo wa mtoto na hivyo
kutoa mwanya kwa uambukizo wa virusi vya UKIMWI.
·
Muda wa kunyonyesha.
Kadiri kipindi cha kunyonyesha
kinavyokuwa kirefu, ndivyo uwezekano wa kumwambukiza
mtoto unavyoongezeka. Hatari huongezeka zaidi iwapo
mama mwenye virusi vya UKIMWI atamnyonyesha mtoto
wake kwa zaidi ya miezi sita kwani wakati huo mtoto
hupewa vyakula vingine.
·
Hali ya kinywa cha mtoto.
Vidonda vya kinywani au kooni na
utandu mweupe kinywani kwa mtoto huweza kuongeza
hatari ya uambukizo wa virusi vya UKIMWI kupitia
sehemu hizo zenye vidonda.
utandu mweupe kinywani kwa mtoto huweza kuongeza
hatari ya uambukizo wa virusi vya UKIMWI kupitia
sehemu hizo zenye vidonda.
“Ikumbukwe kuwa njia kuu ya kuzuia mtoto kupata virusi
vya UKIMWI ni wazazi kuzuia wasiambukizwe virusi hivyo.
Jukumu hilo ni la baba na mama.”
Kumlisha mtoto mchanga aliyezaliwa na mama
mwenye virusi vya UKIMWI (miezi 6 ya
mwanzo)
Tamko rasmi lililotolewa na mashirika ya kimataifa
(WHO/UNAIDS/UNICEF)
linasisitiza mambo muhimu yafuatayo:
• Mama mwenye virusi vya UKIMWI aelekezwe kikamilifu
kuhusu hatari ya
kuambukizwa mtoto kupitia maziwa ya mama na njia
nyingine;
• Wanawake wahimizwe na wapewe huduma za ushauri
nasaha na kupima virusi vya
UKIMWI kwa hiari (VCT);
• Mwanamke mwenye virusi vya UKIMWI apewe taarifa
muhimu na zilizo sahihi,
kumwezesha kufanya uamuzi sahihi wa njia ya kumlisha
mtoto wake, iwe ni
kunyonyesha kwa maziwa yake au kutumia maziwa mbadala.
KUMBUKA
Ni muhimu kuhakikisha kwamba wanawake ambao
hawajaambukizwa virusi vya
UKIMWI na wale wasiojua hali zao za uambukizo
wanaendelea kushauriwa
kunyonyesha maziwa yao, na wasishawishike kutumia
maziwa mbadala kwa
kuwaona
wengine walioshauriwa na kuamua kutumia maziwa hayo.
Njia zinazoweza kutumika kumlisha mtoto
mchanga tangu anapozaliwa
mpaka miezi sita kwa mama anayeishi na
virusi vya UKIMWI
Kumbuka kuwa katika miezi sita ya mwanzo ya maisha ya
mtoto yeyote, maziwa ndiyo
chakula pekee na muhimu sana. Maziwa hayo yanaweza
kuwa ya mama au maziwa
mengine. Ikiwa mtoto hanyonyeshwi maziwa ya mama basi
apate maziwa mengine
kiasi cha mililita (ml.) 150 za maziwa kwa kila kilo moja ya
uzito wake kwa siku. Kwa
mfano mtoto mchanga mwenye kilo tano anahitaji mililita
(ml.) 750 za ujazo za maziwa
(yaani ml. 150 x kilo 5) kwa siku, kiasi hiki kinaweza
kugawanywa katika milo mitano
au zaidi kwa siku. Ni muhimu kutumia kikombe kumlisha
mtoto badala ya chupa ya
kunyonya.
Hii
hupunguza hatari ya maradhi ya kuhara kwani ni rahisi kusafishakikombe kuliko
chupa.
Kuna njia kuu mbili zinazoweza kutumika kumlisha
mtoto
aliyezaliwa na mama
mwenye virusi vya UKIMWI. Njia hizi ni kutumia
maziwa ya mama na kutumia
maziwa mbadala.
inaendelea sehemu ya pili ..
0 comments:
Post a Comment