Thursday, 1 May 2014

FAIDA ZA KUNYWA MTINDI HUIMARISHA KINGA YA MWILI NA KUREFUSHA MAISHA



MTINDI
Mtindi unaorodheshwa kuwa miongoni mwa vyakula bora kutokana na kuwa na virutubisho vingi vya aina mbalimbali ambavyo vina faida nyingi katika mwili wa binadamu.

Vikitajwa kwa uchache virutubisho hivyo, imethibitika kuwa mtindi ni chanzo kizuri cha ‘Calcium’, ‘Phosphorus’, ‘Riboflavin (vitamin B2), ‘Iodine’, ‘vitamin B12’, ‘Pantothenic acid (vitamin B5) ‘Zinc’, ‘Potassium’ na ‘Molybdenum’. Mbali ya virutubisho hivyo, ndani ya mtindi kuna ‘bakteria hai’ ambao ni muhimu kiafya katika mwili.

HUREFUSHA MAISHA

Utafiti unaonesha kuwa unywaji wa mtindi mara kwa mara, hasa katika kundi la wazee, uwezo wa mwili wa kupambana na magonjwa mbalimbali umeonesha kuongezeka na kufanya mfumo wa kinga ya mwili kuwa imara zaidi.


Katika utafiti mmoja, walichaguliwa wazee 162 ambao walipewa utaratibu wa kunywa mtindi na maziwa zaidi ya mara 3 kwa wiki na kufuatiliwa maendeleo yao kwa muda wa miaka mitano. Baadaye utafiti huo ulionesha kuwa idadi ya vifo vya wazee hao ilipungua kwa asilimia 38 ukilinganisha na kundi la wazee wasiotumia au waliotumia mtindi kiasi kidogo sana.

KINGA KWA KINA MAMA

Aidha, mtindi umeonesha kuwa na uwezo mkubwa wa kutoa kinga dhidi ya maradhi ya kuambukiza ukeni (vaginal infections). Katika utafiti mmoja uliohusisha wanawake wenye magonjwa ya kuambukiza sehemu za siri, baada ya kutumia mtindi kiasi cha paketi moja kila siku kwa muda wa miezi sita, maambukizi waliyokuwanayo wanawake hao kabla yalitoweka.

KINGA YA MWILI
Utafiti uliofanywa kwa wanyama, wakiwemo panya na kuchapishwa kwenye jarida moja la masuala ya virutubisho nchini Marekani (Journal Of Nutrition), umeonesha kuwa unywaji wa mtindi kila siku, huamsha na kuupa nguvu mfumo wa kinga ya mwili kupambana na magonjwa kadhaa ya maambukizi, ikiwemo saratani ya utumbo.

HUONDOA LEHEMU MBAYA MWILINI

Katika hatua nyingine, mtindi umeonekana kuwa na uwezo wa kupunguza kiwango cha lehemu mbaya mwilini (LDL (bad) cholesterol) na wakati huo huo kupandisha kiwango cha lehemu nzuri mwilini (HDL (good) cholesterol). Kwa maana nyingine, ikiwa mtindi unaondoa lehemu mbaya, mtumiaji anajiepusha pia na hatari ya kupatwa na tatizo la shinikizo la damu.

KUPUNGUZA UZITO
Mbali ya faida hizo, mtindi pia umeonekana kupunguza mafuta (fat) mwilini na kwa maana hiyo una uwezo wa kupunguza unene unaotokana na mafuta mengi mwilini.

MUHIMU KUZINGATIA
Jambo muhimu la kuzingatia ni unywaji wa mtindi halisi uliotengenezwa kutokana na maziwa halisi ya ng’ombe, siyo mtindi uliotengenezwa kutokana na maziwa ya unga. Siri kubwa iliyomo kwenye mtindi ni ule uchachu unaotokana na ‘bakteria hai’ wanaopatikana baada ya maziwa kuganda na kuchachuka.

Related Posts:

  • FAIDA YA UNYWAJI WA KAHAWA Kikombe kimoja cha kahawa kwa siku chapunguza hatari ya ugonjwa wa moyo Mbali na faida kemkem tunazozijua zinazopatikana kwenye kahawa, utafiti mpya umesema kwamba kunywa kikombe kimoja tu cha kahawa kwa siku … Read More
  • IJUE ASILI YA VIDONGE VYA LISHE   WENGI wetu tungependa kujua historia ya vidonge vya lishe au lishetiba au Food Supplement kama inavyojulikana kitaalamu na nani aliyeanzisha utaratibu huu duniani wa kukigeuza kidonge kuwa chakula. Kabla ya … Read More
  • FAIDA ZA KIAFYA ZA MAFUTA YA NAZI Mafuta  ya nazi  yana faida  nyingi kwa mwanadamu. Ni kusudio  langu kushare  na wewe  msomaji wangu  taar… Read More
  • FAIDA ZIPATIKANAZO KIAFYA KWA ULAJI WA SAMAKI -Huendesha mfumo wa kinga ya mwili -Huzuia saratani -Hutoa ahueni kwa wenye pumu - Hupambana na dalili za awali za ugonjwa wa figo -Huongeza nishati ya ubongo -Huyeyusha damu, huifanya kuwa nyepesi - … Read More
  • ZIJUWE VYAKULA BORA NA FAIDA ZAKE MWILINI TUNAAMBIWA kuwa kuishi vizuri ni pamoja na kula chakula bora na sahihi. Pia, mtu anayeishi vizuri ni yule ambaye hasumbuliwi na maradhi hatari na njia pekee ya kuulinda mwili dhidi ya maradhi hatari ni kujua ipas… Read More

1 comments:

  1. Asante sana kwa andiko zuri lenye ugha ya kueleweka.Mungu akubariki sana, akupe uhai mrefu, uzidi kutuelimisha.

    ReplyDelete