Tuesday 20 May 2014

CANCER OF SAC EGGS OF A WOMAN SARATANI YA KIFUKO CHA MAYAI YA UZAZI CHA MWANAMKE

Saratani ya kifuko cha mayai ya uzazi cha mwanamke. 

Vifuko hivi ni viwili vidogo vilivyo kila upande wa mji wa mimba. Saratani hii huwaambukiza wanawake walio zidi umri wa miaka 50. Ni vigumu kuitambua kwa hivyo ni muhimu kumtembelea daktari wako kila mwaka kwa uchunguzi wa fupanyonga bila kujali miaka yako. 

Baadhi ya mambo yanayowatia wanawake hatarini kupata saratani ya kifuko cha mayai ni:
  • Ikiwa mtu yeyote wakike katika familia (mama,dada,nyanya) amewahi kua nao huu.
  • Umri kuzidi miaka 50.
  • Ukiwa tasa.
  • Ikiwa umewahi kuwa na saratani ya matiti au utumbo mpaua

Wanawake hutambua ungonjwa huu kama umeshaenea sana.

Ishara zengine ni kama:
  • Maumivu tumboni kama uliyejawa na hewa tumboni.
  • Kuendesha au kufunga choo
  • Kutohisi njaa au kutokula vizuri
  • Kupoteza au kuongeza uzito bila kisababu
  • Kuvuja damu wakati haupo katika hedhi.

Dalili hizi zaweza kuwa kitu kingine, lakini ni vyema kuongea na daktari unapoziona.

Saratani ya tezi kibofu cha mkojo (Prostate) Saratani ya mamalia dume (tezi kibofu) 

huwa kati ya wanaume. Huweza kutibiwa inapogunduliwa mapema. Ugonjwa huu huwaambukiza wanaume walio na umri wa miaka 55 na zaidi. Mamalia dume hutengeza manii ambayo mbegu za kiume hupatikana. Huambukiza chini ya kibofu cha mikojo.

Wanaume wengine wamo hatarini kupata saratani ya mamalia dume:
  • Walio na umri wa miaka 55 na zaidi
  • Wanaume ambao wamekuwa na jamaa kama baba au kaka ambao washauguwa ugonjwa huu.
  • Wanaume weusi.
  • Kula vyakula vingi vya mafuta, nyama nyekundu, siagi na maziwa.

Dalili ya saratani ya mamalia dume:
  • Kukojoakojoa kila mara hasa wakati wa siku.
  • Kuwa na shida za kuanza kukojoa au kusitiri mikojo.
  • Kukojoa kwa matone matone.
  • Kuhisi uchungu au moto unapokojoa
  • Kuwa na shida kusimika.
  • Kuhisi uchungu unapomwaga manii.
  • Kukojoa mikojo iliyochanganyika na damu.
  • Maumivu ya kila mara hasa sehemu za mgongo,nyonga au mapajani sehemu za juu.

Daktari wako anaweza kukufanyia uchunguzi kutambua kama una saratani ya mamalia dume.Kwa kutumia kemikali ya “Prostate specific antigen” au PSA katika damu yako, ikiwa una idadi ya juu ya PSA , waweza kuwa na ugonjwa huu.

Saratani ya Ngozi Watu wengine wamo hatarini zaidi kupata saratani ya ngozi: 

  • Walio weupe, na macho na ngozi ilio parara.
  • Walio na mabakabaka mwilini.
  • Wanaoishi sehemu ambayo kuna jua jingi.
  • Walio na maturuturu kutokana na miale ya jua.

Dalili za Saratani ya Ngozi ni nini?
  • Uvimbe au mabaka katika ngozi
  • Uvimbe katika ngozi usiopona
  • Katika hatua za mwisho unahisi mwasho, ngozi inayowaka moto na kutokwa damu.

Saratani ya ngozi inaweza kutibika ikitambulikana mapema. Hata wale wasiokuwa hatarini ya kupata saratani ya ngozi lazima watumie mafuta ya kujipaka ili kuzuia miale ya jua hasa kati ya saa 4 asubuhi na saa 9 mchana.

Saratani ya Makodo (Testicular) Saratani ya makodo au mapumbu ndio inayojulikana sana hasa kwa vijana barubaru wa kati ya miaka 15 hadi 35. Habari njema ni kuwa saratani ya makodo ni haba sana na inatibika. 

Licha ya kutoa mbegu za uzazi, makodo pia hutengeza homoni za kiume. Makodo ni laini, mviringo na ngumu. Wanaume wanahitaji kujikagua wenyewe mara kwa mara kila mwezi kutambua mabadiliko.

Wanaume wengine wamo hatarini zaidi mwa kupata saratani ya makodo:

  • Watoto wa kiume waliozaliwa na makodo isiyo ning’inia chini.
  • Wanaume ambao makodo yao hayakumea kawaida.
  • Wanaume waliozaliwa na Klinefelter’s Syndrome (Hali ya mvulana kuzaliwa na chromosome zaidi ya 46 iliyo kawaida. Akikua mwili wake una dalili za uke kama vile matiti na kutokuwa na nywele usoni)

Dalili za Saratani ya Makodo
  • Uvimbe usiyo na uchungu kwa kodo
  • Uchungu ndani ya kodo
  • Kodo kuwa ngumu na kubadilika kwa saizi. (Kuvimba au kurudi). Kuhisi uzito kwa mapumbu (mfuko wa makodo)
  • Uchungu usio mkali kwa manena na sehemu ya chini ya tumbo.
  • Matiti kuwa makubwa au kuuma.

Hizi pia zinaweza kuwa dalili za magonjwa mengine ambayo si saratani. Ukihisi dalili yoyote ya hizi, muone daktari.

1 comments:

  1. Greatest thanks to Dr Oyagu for his herbal drugs that he prepared for me and when i start using it in just 2weeks i was completely cured and that ended my HERPES SIMPLEX 1&2 DISEASE i am so happy and grateful to Dr Oyagu . after reading about him on a testimony of Jason Cash on a blogger. i knew suddenly Dr Oyagu was the right Doctor to cure my HERPES SIMPLEX 1&2 DISEASE. i discuss with Dr Oyagu and he prepared a herbal medicine for me and when it got sent to me in south korean . i used the herbal medicine and 2weeks and i went to check up again. after 15years of suffering from HERPES SIMPLEX 1&2 at last i am smiling once again. Dr Oyagu also has remedy to others disease like COLD SORES,HIV/AIDS,DIABETES.CANCER,HIGH BLOOD PRESSURE AND MANY MORE. I oblige everyone to contact this powerful herbalist Dr Oyagu and be free from your suffering. contact his WhatsApp line:+2348101755322 or his Email via dr.Oyaguherbalhome@gmail.com

    ReplyDelete