Sunday, 20 April 2014

TIBA YA UGONJWA WA MALARIA






Ugonjwa wa malaria umekuwa na tiba za asili nyingi ambazo baadhi tumeshaziandika na zimewasaidia wengi, leo tunawaletea tiba nyingine inayomaliza kabisa maradhi hayo.
  • BAMIA
Chukua mbegu za bamia uzikaange, uzisage mpaka ziwe unga.
Chemsha nusu kikombe cha unga huo katika glasi 2 za maji kisha chuja.

DOZI
Wakubwa kikombe 1 x 3 kwa siku kila baada ya mlo.
Miaka (7-12 ) anywe nusu kikombe x 3 kwa siku kila baada ya mlo. Huruhusiwi kuchemsha na kuweka bali fanya hivyo kila unapotaka kunywa.
Miaka (2-6) robo kikombe x 3 kwa siku.
Kwa watoto wachanga kijiko kikubwa 1 x 3, mpatie baada ya kunyonya au kunywa maziwa na kushiba.

  • PAPAI
Chukua mbegu za papai zikaushe kivulini, baada ya hapo zisage ziwe unga laini.

DOZI
Weka kijiko kimoja cha chai kwenye uji, kama huwezi kutumia uji unaweza kuweka kwenye chai lakini muhimu sana kwenye uji.
Kwa siku tumia mara tatu.
Kwa mtoto miaka 5-10 unaweza kumgawia nusu ya mtu mzima.
Kwa mtoto wa miaka 3-5 unaweza kumgawia ¼ wote x 3 kutwa.


  • ALIZETI
Chemsha kilo moja ya majani ya alizeti katika lita 2½ za maji kwa dakika 15. 

DOZI
Kunywa nusu glasi x 3 kwa siku, tumia tiba hii kwa muda wa siku 5.
Miaka (7-12) ¼ glasi x 3 kwa siku.

Miaka (2-6) kijiko 1 x 3 kwa siku.

0 comments:

Post a Comment