Ukigundua una tatizo hili, hakikisha unasafisha miguu yako mara kwa mara ukiiacha mikavu muda wote ili kuepusha unyevunyevu.
Miguu kutoa harufu mbaya ni tatizo sugu linalowakabili baadhi ya watu katika jamii, wengi wakiwa wanaume.
Katika nyakati hizi za mvua, tatizo hili linaonekana kuzidi kuwa sugu,
hali inayosababisha kuwepo na harufu mbaya hasa kwenye mikusanyiko ya
watu kama vile kwenye daladala.
Lakini watu wengi wenye tatizo
hili huwa wagumu kukubaliana na hali yao hata kutafuta tiba mahususi
inaweza kuwaondolea kero hiyo.
Licha ya kuwepo sababu mbalimbali
zinazochangia kutokea hali hiyo, ukweli utabaki kuwa uchafu ndiyo chanzo
kikuu cha miguu kutoa harufu.
Kwa kiasi kikubwa uchafu huo ndio
unasababisha kuzaliwa kwa vijidudu vinavyoleta harufu mbaya kwenye miguu
na kuwakera wanaokumbana na harufu hiyo.
Pamoja na tiba nyingine
za kitaalamu ambazo mtu mwenye tatizo hili anaweza kupata, usafi ni
jambo kubwa analopaswa kuzingatia zaidi hasa kipindi hiki cha mvua.
Ukigundua una tatizo hili, hakikisha unasafisha miguu yako mara kwa mara ukiiacha mikavu muda wote ili kuepusha unyevunyevu.
Kila unapovaa viatu vya kufunika, hakikisha unavaa soksi safi na kavu.
Epuka kurudia soksi au kuvaa ambazo hazijakauka vyema kwani zinaweza
kusababisha miguu kunuka mara dufu.
Usivae viatu vilivyoloa na
endapo ikatokea umenyeshewa, hakikisha unavianika kwenye hewa ili
vikauke kupunguza uwezekano wa kutokea harufu.
Kama utahisi
tatizo ni kubwa zaidi ni vyema utumie sabuni zenye dawa za kuua vijidudu
pamoja na mafuta maalumu yanayoweza kutumika miguuni. Ikishindikana,
nenda kwa wataalamu wa afya.
Kwa Ushauri wa Maswali na Matibabu ta
Maradhi yoyote yale wasiliana na mimi Kwa njia ya email Baruwa ya pepe
Email Address yangu hii hapa fewgoodman@hotmail.com Au waweza kuni Add kwenye Whats Up yako namba yangu hii hapa +905344508169
0 comments:
Post a Comment