Wednesday, 23 April 2014
MAAJABU YA ASALI MBICHI NA KARANGA KWA NGOZI YA BINADAMU
. Karanga ni mojawapo ya nafaka muhimu kwa afya ya binadamu. Huweza kutumika kama chakula, mafuta, kiungo na hata kwa ajili ya urembo.
Zao hilo huweza vile vile kufanya maajabu katika ngozi. Bila kubagua jinsia, matumizi ya karanga husaidi katika kuondoa makunyanzi na kulainisha ngozi.
MAHITAJI
Kwa kazi hii ya ngozi, karanga zinazohitajika ni zile mbichi. Kitu kinachohitajika ni kuchukua karanga mbichi ambazo hazijakaangwa kiasi kidogo kama kikombe kidogo cha chai.
MATAYARISHO
Zianike karanga juani kwa muda ili ziweze kumenyeka kwa urahisi bila kukaanga. Saga karanga zako kwa kutumia blenda au kitu chochote kitakachoweza kuzilainisha na kuwa unga laini.
Chukua unga wako wa karanga na uuchanganye na asali mbichi kiasi kidogo, kisha acha kwa muda wa dakika 10 ili vichanganyike.
MATUMIZI
Chukua mchanganyiko wako, kisha paka usoni hasa zile sehemu unazoziona kuwa na mikunjo zaidi.
Subiri kwa dakika kama 10, kisha osha uso wako na sabuni isiyo na kemikali baada ya hapo futa uso wako na kitambaa kisafi na kikavu. Subiri tena kwa dakika 5 halafu paka mafuta au losheni. Unashauriwa kufanya hivi mara moja kwa wiki.
Kiasili njia hii imekuwa ikitumiwa na Wanyamwezi wa Tabora kama kipodozi kwa ajili ya mabinti wadogo pindi wanapokaribia kufanyiwa sherehe maalum.
Unaweza pia kusugua taratibu uso kwa kutumia mchanganyiko wako ili kuondoa takataka katika mwili wako ambapo baada ya kumaliza zoezi hilo unaweza kujipodoa kwa kupaka aina nyingine za vipodozi.
Kwa kuwa hazina madhara, unaweza kufanya hivi kila siku na utafurahia matokeo yake.
Shukrani sana kwa darasa zuri
ReplyDeleteNingesauri pia uruhusu right-click kwenye mada zako maana iko disabled ie mtu hawezi ku-right click
Ukitaka kusoma Messege zangu ubonyeze mahali palipo nadikwa hivi (Read More) unaweza kusoma ukitaka kukopi niambie nitakupatia unayotaka.
ReplyDelete