USIOYAJUA-magadi soda si chakula tu.
Leo asubuhi Dada yangu alinichekesha
sana,alifanya siku yangu ianze vizuri pale aliponiletea kibao kichafu
cha kukatia nyama alichobeba kutoka nyumbani kwake ili nimsaidie
kukisafisha.Nilicheka sana kwani kila mara najitaidi kumfundisha mbinu
mbalimbali za jikoni lakini hasikilizi.sasa leo yalipomfika,na kufikia
hatua ya kutaka kukitupa kibao hicho ndipo alipokumbuka kua niliwai
mfundisha namna ya kukisafisha.Akaamua kujibeba yeye na kibao chake
akanifata.Na ndipo hapo nilipomuweka kwenye darasa la vitendo kwa
makubaliano kwamba siku nyingine sitamsaidia.
Najua wengi mnaifaham Baking soda au
Bicarbonate of soda kwa lugha ya Kiswahili huitwa magadi soda ,kwa wale
msioifahamu,Baking soda au bicarbonate of soda ni hitaji la kawaida
kabisa jikoni,hutumika sana katika vyakula vya kuhoka kama keki na
mikatepia hutumika katika maandazi,pan cakes,chapatti na vyakula vingine
vingi.Hata ivyo Baking soda wakati mwingine hutumika kulainisha vyakula
ambavyo ni vigumu kuiva au visivyolainika haraka vinapopikwa kama
mahindi yasiokobolewa,mboga za majani za kienyeji kama mgagani,
msusa,majani ya kunde yaliyo komaa na kadhalika.Hapa nchini Baking soda
ya jina kubwa na kufaamika kwa wengi inaitwa SIMBA.
Baking soda hupatikana kwa wingi
madukani na hata sokoni.kuna ile ambayo imepita kiwandani na kusindikwa
kitaalam na kuna ile ya kienyeji ambayo iko kiasili zaidi.
Siri kubwa ambayo wengi hawajui kuhusu
baking soda,Ni ambavyo huweza kutumika kufanya shughuli nyingi za
usafi.Uwepo wa alkalini ndani ya baking soda huipa uwezo wa kuondoa
uchafu wenye asili ya asidi.
1.Kusafisha kibao cha kukatia nyama au mboga.
Kwa wale mnaotumia kibao cha plastiki au
mbao kukata nyama mnajua ambavyo kibao hushika uchafu na hata
kubadilika rangi,hata baada ya kukiosha.Kutatua tatizo hilo na kufanya
kibao chako kiwe safi na cheupe tena,Nyunyuzi baking soda ya kutosha
kisha sugua na dodoki adi kibao kiwe safi,kama ni uchafu wa muda mrefu
loanisha kibao na maji kisha nyunyuzi baking soda na uache kwa dakika 15
ndipo usugue na dodoki
2.Kuzibua sinki la jikoni.
Sinki la jikoni mara nyingi huziba na
kugoma kupitisha maji machafu kwasababu ya mafuta na uchafu wa
chakula.Mwaga kikombe kimoja cha baking soda kwenye tundu la sinki,kisha
mwaga vikombe vitatu vya maji ya moto sana.Acha kwa angalao masaa manne
kabla hujatumia sinki.Ni vyema ukafany ivyo usiku unapoenda kulala
kwani sinki halitatumika adi asubuhi.
3.Kukata harufu ya mkojo chooni.
Kama unasafisha choo lakini bado kuna
harufu mbaya ya mkojo.Chukua nusu kikombe cha baking soda changanya na
nusu kikombe cha vinegar nyeupe kisha mwaga ndani ya choo na unyunyuze
kwenye sakafu ,na baada ya nusu saa unaweza kudeki sakafu ili pabaki
safi.
4.Kusafisha na kung’arisha sinki,bathtab na tiles.
Ingawa wengi hupenda kuweka
tiles,masinki na Bathtubs kwenye nyumba zao,utakubaliana na mimi
nikisema wengi hawajui namna ya kuzifanyia usafi,unakuta sinki au tiles
nyeupe zimegeuka na kua za rangi ya njano kwa uchafu.
Chukua nusu kikombe cha baking soda
changanya na nusu kikombe cha sabuni ya majichanganya vizuri ili kupata
kama uji mzito.Kisha tumia kusugua sinki,tiles au bathtub.
5.Kusafisha Oven
Kawaida unapohoka vyakula kama
nyama,samaki,mboga za majani na matunda kama nanasi,mchuzi au umajimaji
kutoka kwenye vyakula hivi humwagika ndani ya oven.Wakati mwingine unapo
rost vyakula ndani ya mafuta kwenye grill,mafuta huruka na kuchafua
oven.Kwa kawaida uchafu wa aina hii Uganda haraka sana ndani ya oven.
Ili kusafisha .weka baking soda
yakutosha kwenye sehem ya chini kabisa ya oven,kisha iloanishe na
maji,usiweke maji mengi,kiasi tu cha kutosha kuloanisha baking
soda.Fanya hivi usiku kabla ya kulala na ifikapo asubui uchafu wote
ulioganda utakua umelainika,tumia dodoki kusafisha.
6.Kukata /Kuondoa harufu mbaya ndani ya friji.
Kutokana na uwekaji wa vyakula iana
mbalimbali vyenye harufu tofauti tofauti mara nyingi friji huwa na
harufu isioeleweka.Kwa sisi yunaoishi Tanzania na kukabiliwa na tatizo
la umeme,umeme unapokatika kwa muda mrefu friji hutoa harufu.
Chukua boksi la baking soda,lifungue na
kisha fungua mfuko wa plastiki uliobeba baking soda ili ukae wazi,kisha
weka baking soda hiyo kwenye sehem ya chini ya friji yako,itanyonya
harufu yote ndani ya friji na kuiacha ikiwa fresh.Ukiweka boksi lenye
baking soda kidogo utendaji wake huwa wataratibu sana,hivyo ni vyema
ukaweka boksi jipya.
7.Kukata harufu kwenye nguo mpya
Mara nyingi unaponunua nguo mpya inakua
na harufu ya upya na ndio maana watu wengi hufua nguo mpya kabla
hawajavaa.Nguo za mtumba nazo hua na harufu kali inayolazimu kufua kabla
hujavaa,hizi zote ni harufu za kemikali zilizotumika katika
utengenezaji wa nguo,na kwa nguo za mitumba ni harufu ya madawa yenye
kemikali zinazotumika kuhifadhi nguo.
Ili kuondoa harufu hizo,pima kikombe
kimoja cha baking soda changanya kwenye maji lita tano ,kisha loweka
nguo kwenye maji hayo kwa masaa matatu au zaidi,suuza na uanike.
Kwakua baking soda inaweza fanya yote
haya,unakila sababu ya kua nayo jikoni kwako,hasa kwa ajili ya
kusafishia kibao cha kukatia Nyama na mboga,pamoja na kuzibua sinki lako
la jikoni.Ukweli ni kwamba,kibao cha kukatia nyama kikiwa kichafu,au
kimebadilika rangi na mabaki ya nyama yamenata au kuganda kwenye kibao
hicho,inatia kinyaa na pia ni hatari kwa afya ya familia yako.Sinki la
jikoni nalo likiziba na kuacha kupitisha maji machafu ndio mwanzo wa
kurundika viombo vichafu na kua na maji machafu kwenye beseni kila
wakati,chanzo kikubwa cha inzi jikoni na magonjwa ya tumbo.
Kama kawaida,naboresha maisha ya familia yako,Kazi yangu ni kukuelimisha tu,utendaji ni juu yako.
Jali afya ya familia yako.
Am Lisa by name, i was diagnosed with Herpes for 3years ago i lived in pain with the knowledge that i wasn't going to ever be well again i contacted so many herbal doctors on this issue and wasted a large sum of money but my. condition never got better i was determined to get my life back so one day i saw mr Brown post on how Dr Aba saved him from the VIRUS with herbal medicine i contacted Dr Aba on his email address dr.abaherbalhome@gmail.com we spoke on the issue i told him all that i went through and he told me not to worry that everything will be fine again so he prepared the medicine and send it to me through courier service and told me how to use it,after 14days of usage I went to see the doctor for test ,then the result was negative,am the happiest woman on earth now. this testimony is real.thanks to Dr Aba God bless you. you can also reach him on his whatsApp number +2348107155060
ReplyDelete