Wednesday 30 April 2014

JE! UNAJUA KWAMBA, UNGA WA MKAA NI TIBA YA MAGONJWA NA MATATIZO MBALIMBALI YA KIAFYA?



Mkaratusi

Watu  wengi  hawajui  kuwa, unga  ama  vumbi  vumbi  la  mkaa  linaweza  kutumika  kama  tiba  ya  magonjwa  na  matatizo  mbalimbali  ya  kiafya. Fuatana  name  hadi  mwisho  wa  makala  haya  upate  kujua  namna  ambavyo  unga  wa  mkaa  unaweza  kutumika  kama  tiba  ya  magonjwa  na  matatizo  mbalimbali  ya  kiafya  :
JINSI  YA  KUUPATA  UNGA WA MKAA :
Unga  wa  Mkaa
Unaweza kupata  unga  wa  mkaa kutoka kwenye mti wa mkuyu, kifuu cha nazi, msonobari au  mkaratusi.  Hivyo  basi  unga  wa  mkaa  unao  zungumziwa  hapa  ni  ule  unaotokana  na   eidha kifuu  cha  nazi, mti  wa  msonobari  au  mkaratusi.
MAGONJWA  YANAYO  TIBIWA  NA  UNGA  WA  MKAA
Unga  wa  mkaa  umethibitika  kuwa  na  uwezo  wa   kutibu magonjwa   matatizo  mbalimbali  kama  vile; Kuumwa na nyoka Kiungulia ,Kusaga  chakula, Uvimbe, Kutapika , Kuhara damu, kuharisha ,Vidonda vya tumbo ,  Macho , Dawa  kwa  mtu  aliye  kunywa  sumu  au  vitu  vyenye  kemikali n.k
JINSI   YA  KUTAYARISHA  UNGA  WA  MKAA  WA  KIFUU  CHA  NAZI, MSONOBARI  AU  MKARATUSI.
Choma kifuu cha nazi hadi kiwe  kama  mkaa  kasha saga kupata  unga  unga  wake.
Kwa   mti  wa  msonobari tumia magome yake  kwa  kuyachoma  hadi  yawe  mkaa  kasha  yasage  kupata  unga  unga.
MATAYARISHO  YA  DAWA
Chukua kijiko 1 kikubwa cha mkaa (unga) changanya na maji safi ya kunywa ya uvuguvugu uwe kama uji uji.

MATUMIZI   YA  DAWA
Kunywa kikombe kimoja cha mchanganyiko huo kabla ya kula.

MATUMIZI   YA  DAWA  HII  KWA  MTU   ALIYE UMWA NA NYOKA :
Shona kifuko cha kitambaa cheupe, chota mkaa kijiko kikubwa, weka ndani ya kifuko na maji kidogo, funga sehemu iliyoumwa, kisha fungua baada ya saa1, fungia nyingine hadi ufikapo hospitalini. Pia endelea kumpa  dawa hiyo hiyo ya kunywa, iliyokorogwa na kuwa kama uji mzito baada ya saa1 ufikapo hospitalini sumu yaweza kuwa imekwisha .
MATUMIZI  YA  DAWA  HII  KWA  MTU  ALIYEKUNYWA  SUMU
Kwa mtu aliyekunywa sumu   tumia njia hiyo ya kunywa. Inafaa kuwa na dawa hii nyumbani mwako kila wakati.

KWA   MTU  MWENYE  MATATIZO  YA  MACHO
Kwa   mtu  mwenye  matatizo  ya  macho, weka katika kifuko cha kitambaa kama hapo juu, fungia au weka kwenye jicho. Funga kwa siku 3 mfululizo wakati wa usiku.

0 comments:

Post a Comment