NI mpapai! Mara nyingi nimekuwa nikiongea kuwa Tanzania tuna miti
mingi sana kiasi kwamba bado hata robo yake hatujaijua majina yake,
achilia mbali kitu muhimu kama kujua matumizi.
Mungu alipomuumba binadamu na kumleta duniani, alihakikisha hapatwi na maradhi kama fangasi, madonda tumbo, ukurutu, mapunye n.k, kwa kuumba na mpapai. Mungu hakuumba hata zahanati pale Bustani ya Eden, badala yake bustani ile iliumbwa ili wakila vilivyomo basi iwe ni hoteli washibe, hospitali wajitibie, saluni wawe warembo n.k.
Mpapai ulikuwepo. Mpapai toka mizizi, mti wake, matunda, majani mpaka
maua yake yanabeba maji na utomvu ambao nakuhakikishia msomajikama utayadondoshea maji hayo katika sehemu iliyoshambuliwa na maradhi
niliyotaja hapo juu, basi hutarudia kupaka tena maji hayo maana kesho
yake tu utaona mambo yamekuwa sawa.
VIDONDA VYA TUMBO:
Kula kipande cha papai kisichoiva vizuri kila siku alfajiri, ukimaliza shushia na mbegu moja tu ya kitunguu swaumu. Hakikisha unazidisha kiwango cha kunywa maji siku zote utakazo jitibia vidonda hivyo, na ikifika siku 13 hadi 16 utanipigia simu kunitaarifu kuwa vidonda vimepona.
Kula kipande cha papai kisichoiva vizuri kila siku alfajiri, ukimaliza shushia na mbegu moja tu ya kitunguu swaumu. Hakikisha unazidisha kiwango cha kunywa maji siku zote utakazo jitibia vidonda hivyo, na ikifika siku 13 hadi 16 utanipigia simu kunitaarifu kuwa vidonda vimepona.
Kama kipato chako ni kidogo na kupata papai kila siku
ni gharama, basi usikonde. Chuma majani mawili ya mpapai kisha katakata
kama mboga ya kupikwa, tia katika chupa kubwa ya lita mbili za maji na
kunywa kutwa nzima kidogo kidogo hadi yaishe. Waweza kutia vipande vya mapapai machanga yaliyokatwakatwa pia badala ya majani.
FANGASI NA MAPUNYE
Hili ndiyo tatizo la watu wengi hapa Dar na popote kwenye joto kali. Kama umeshindwa kuvaa viatu kwa sababu ya fangasi na mapunye wala usikonde.
Fua soksi zako, suuza na maji safi,
chuma majani ya mpapai mawili au matatu fikicha pamoja na soksi kabla
hujazikamua.
Zikishafikichika na majani basi anika hivyo hivyo.
Zikikauka, pukuta majani kisha vaa soksi zako endelea na
shughuli zako maana kama fangasi wote watakufa na wala soksi hazitatoa
harufu tena.
MAPUNYE KICHWANI
Huu ni ugonjwa wa
watoto zaidi. Watoto wanasumbuliwa sana na mapunye, ukurutu, vipele na
fangasi kwapani na kichwani. Chuma papai changa, mpake mtoto utomvu
katika mapunye mara moja tu yataisha. Yasipoisha,rudia hata
mara tatu lakini ukiona hayakauki, basi naomba unitafute nikuelekeze la
kufanya maana maradhi mengine huja na matatizo hayo hivyo atakuwa
anaumwa zaidi ya mapunye na fangasi na atahitaji tiba kali zaidi.
Angalia. Kama mtoto ni mdogo wa miaka mitatu kushuka chini basi
usimpake utomvu, badala yake mpake masalia ya maganda ya papai bivu
maana utomvu huponyesha haraka lakini ni mkali na unaleta maumivu ambayo
mtoto mdogo hatavumilia.
Mpapai umeumbwa na unaishi na binadamu
kwa ajili ya kazi hii tu. Tuweke akilini kuwa mimea ni viumbe hai
visivyotembea lakini vipo kwa ajili yetu hivyo tuvipende na kuvithamini
viumbe hivi.
Tuviulize majina yao, tuulize pia kila mmea una
kazi gani hapa duniani n.k. Mpapai umeumbwa mahususi kuwa sabuni ya
mwili nje na ndani. Ukiwa na tatizo lolote la shambulio la ngozi
basi kimbia, chuma mpapai fikicha utoe majimaji hapo kwenye tatizo na
mara moja utaona mafanikio tena kwa haraka mno.
0 comments:
Post a Comment