Saturday 3 May 2014

VIJUE VIKWAZO KATIKA UZAZI WA MPANGO VINAVYO IKABILI JAMII



WANAWAKE wengi nchini wana elimu ya
kutosha kuhusu uzazi wa mpango.
Wanajua kutokana kwa kuambiwa na rafiki
zao, kujifunza kwa wazazi, kliniki na kwa
 
kusoma kutoka vitabuni na mahali pengine.
Wanajifunza kwamba uzazi si kitu cha
bahati mbaya. Kinasababishwa. Baadhi ya
 
akina mama hawa wanataka kuepuka
mimba zisizotarajiwa, wanaona hali mbaya
ya uchumi, kipato duni na kazi ngumu ya
kulea watoto wengi.


Wanawake wengi wanajifunza aina
mbalimbali za kupanga uzazi, mfano za vijiti,
vitanzi, sindano, kondomu, vidonge na
nyingine za asili za kufuata kalenda ya mwili
ama wenzi wao wa kiume ‘kuishia nje’.
 
Ukizungumza na wanawake wengi, wasomi
na wasio wasomi, wanasema kila njia ni
nzuri kwa mtumiaji maadam ameona inafaa.
 
Kwani njia moja inaweza kumfaa na
mwingine isimfae. Hata hivyo, wapo baadhi
ya watafiti wanaosema kwamba njia nyingi
za uzazi wa mpango mbali na zile za asili
 
zina madhara haya na yale. Katika kampeni
yao ya kupanga uzazi, wanawake wengi
wanapambana na vigingi viwili vikubwa.


Kimoja ni uhaba wa wataalamu wa
kuelekeza utumiaji wa njia salama za uzazi
wa mpango na kuadimika kwa njia hizo za
 
kupanga uzazi. Kutokana na vikwazo hivyo,
wanawake wengi wamejikuta ama
 
kulazimika kutumia njia za uzazi ambazo
hawazipendi, ama zisizo salama na zenye
kuwaletea madhara.


Wengine wamejikuta, wakitumia njia
ambazo, wanashindwa kuzifuata na
hatimaye wanatumbukia kwenye mimba
zisizotarajiwa na kuamua kuzitoa.



Bingwa wa Masuala ya Wanawake katika

Hospitali, anasema,
wanawake wengi wamekuwa wakishindwa
kufuata mpango wa uzazi kutokana na
kukosa huduma wanazotaka au kukosa
wataalamu wa kuelekeza njia mbalimbali za
uzazi.


 
wanawake wanaotumia njia za kisasa za
uzazi wa mpango wameanza kuongezeka
katika kipindi cha miaka miwili iliyopita.
 
Anasema ukizungumza na wanawake,
wanakubali kwamba wanatumia njia
 
mbalimbali za kuzuia mimba, kupanga uzazi
na kuzuia maradhi kwa lengo la kupata
muda wa kutosha kufanya shughuli za
ujasiriamali.


zahanati nyingi hazitoi huduma zote za
kupanga uzazi na kwamba zipo baadhi
zinatoa njia moja tu kati ya hizi; sindano,
vidonge, vitanzi, vijiti, kondomu na kalenda
ya mwili.

Ukienda vijijini/kijijini, kutokana na
kukosekana kwa mtaalamu katika zahanati
nyingi karibu zinashindwa kuendelea na njia yake
ya sindano, watu wengi wanamua kuchukua vidonge tena pasipo maelekezo ya mtaalamu.


maeneo mengi au watu wengi hawana

elimu ya
kutosha kuhusu vidonge, wakati mwingine
alisahau kutumia vidonge, akajikuta
amepata mimba ambayo hakupangilia.
 
Matatizo kama hayo yanawakumba
wanawake wengi, japo idadi ya hospitali,
vituo vya afya na zahanati ni nyingi nchini,
lakini hakuna huduma ya kuaminika ya uzazi
wa mpango.


Takwimu za Wizara ya Afya na Ustawi wa
Jamii za 2006 zinaonesha kwamba kulikuwa
na hospitali 219, vituo vya afya 481 na
 
zahanati 4,679, ambavyo vingi vina uhaba
wa wataalamu wa afya na hasa inayohusu
uzazi. Kumekuwa na matatizo katika
 
hospitali na vituo vingi vya afya na hata
zahanati za kupata huduma hizo, kutokana
na wanawake wengi kukosa uchaguzi wa
aina ya njia wanazoona zinawafaa katika
kupanga uzazi.


Wanawake wamekuwa wakifika hospitalini,
vituo vya afya au zahanati na kulazimishwa
kutumia sindano au kondomu, wakati wao
wamezoea vijiti au vidonge.

Binti mmoja nilimuuliza

anasema, alipoenda zahanati moja
aliambiwa kuwa mtaalamu wa kuweka vijiti
amesafiri hivyo asubiri hadi atakaporudi au
atumie vidonge.
 
Kwa kupatikana huduma za vidonge tu,
Binti huyo alikuwa na wakati mgumu na hivyo
kwa hofu ya kupata ujauzito asiopangilia,
akaamua kuanza kutumia vidonge ambavyo haikuwa chaguo lake

0 comments:

Post a Comment