1. Kama unahitaji kumtibia mtu aliyerogwa uchawi
usiotibika kirahisi au amezunguka sana kutafuta
matibabu mbalimbali basi utakwenda katika mti huu kwa kufuata adabu za kuchukua mti kitiba kisha
utachukua majani yake kisha
utakwenda
kuyapondaponda majani hayo kisha utachanganya
katika maji yako ya kuoga na majani mengine utatia
katika maji ambayo utakuwa unakunywa kiasi cha
kikombe kimoja asubuhi na jioni,pia utakuwa
unakoga maji hayo asubuhi na jioni kwa muda wa
siku saba hadi 14.Kama kupata majani mabichi ya mti
huo itakuwa ni vigumu basi utachuma majani mengi
kisha utayaanika alafu uyasage upate unga
wake,kisha unga huo utakuwa unachanganya katika
maji yako ya kuoga na unga mwingine utakuwa
unaweka katika maji ya vugu vugu au katika uji wako
kisha unakunywa.Hakika utakwenda kupona maradhi
hayo.
KUFUKUZA NA KUONDOA MAJINI WA KICHAWI KATIKA MWILI
2. Kama unahitaji kufukuza majini wachafu katika
mwili utachemsha majani ya mti huu kisha utatumia
kumpigia nyungu mgonjwa anayesumbuliwa na
majini wachafu katika mwili wake,tumia dawa hii
asubuhi na jioni kwa muda wa siku saba
mfululizo.Inshaalla majini hao wataondoka haraka
sana.
KUTIBU TATIZO LA KIFUA AU UGONJWA WA PUMU
3. Kama unahitaji kujitibu au kumtibu mtu
anayesumbuliwa na tatizo la kifua au pumu
utakwenda katika mti huu kisha utachimba mizizi
zake kisha utakwenda kuitwanga mizizi hiyo upate
unga wake.Unga huo utatumia kiasi cha kijiko kimoja
cha chai kuchanganya katika juisi ya asali(zile za
kienyeji na sio za viwandani) au ataweka katika
kikombe cha uji kisha utatumia kunywa kikombe
kimoja asubuhi na jioni kwa muda wa siku 7-21.
0 comments:
Post a Comment