Saturday, 15 April 2023

FAIDA YA KULA MAGANDA YA NDIZI MBIVU KIAFYA.

 




Watu Hula Maganda ya Ndizi. 

Wewe Unazijua Faida Zake?

How healthy are bananas? Bananas are rich in Vitamin B6 and a good source of fiber, vitamin c, magnesium and potassium. 

Bila shaka hujawahi kuona mtu akila maganda ya ndizi kutokana na ukweli kwamba kinacholiwa ni kilicho ndani na kutupa ganda. 

Hata hivyo katika nchi za Asia, kama vile India, watu wamekuwa wakila ndizi na maganda yake kwa miaka mingi sasa.

Tofauti na ndizi yenyewe, ganda lake huwa gumu kidogo na lina uchungu ambao si rahisi mtu kupenda kula na ndiyo sababu watu wengi hawawezi kula maganda ya ndizi. 

Lakini pamoja na uchungu wake, kuna virutubisho muhimu sana ndani yake ambavyo tutakupa siri na sababu kwa nini uwe unakula na maganda ya ndizi pia.

Utafiti uliofanyika umebaini kuwa, Maganda ya ndizi mbivu yana kiwango kingi zaidi cha Vitamin B6 na B12 pamoja na madini ya Manganizi (Magnesium) na Potasia (Potassium) kuliko ndizi yenyewe. 

Hivyo unapokula ndizi na kutupa maganda yake unakuwa umetupa virutubisho vingi zaidi kuliko ulivyokula.

Aidha, utafiti unaonesha ndizi ina asilimia 8 ya kiwango cha madini ya Manganizi kinachohitajika kila siku na mwili, madini haya ni muhimu kwa kurekebisha kiwango cha sukari mwilini na shinikizo la damu.

Kiwango cha madini ya potasia kilichomo kwenye ndizi ni asilimia 12 ya mahitaji ya kila siku ya mwili ambayo ni muhimu katika ukuaji wa seli za mwili.

Asilimia 17 ya mahitaji ya mwili ya kila siku kwa upande wa kamba lishe (fiber) utaipata kwa kula ndizi. 

Kirutubisho hiki ni muhimu katika usagaji wa chakula na kupunguza hatari ya mtu kupatwa na kisukari.

Kwa upande wa vitamin B6 na B12, ndizi inatoa kiasi cha asilimia 20 ya mahitaji ya kila siku ya mwili wa binadamu.

 Vitamini hizi ni muhimu katika zoezi la kugeuza chakula tunachokula kuwa nishati inayohitajika mwilini.

Ili kupata faida za kutosha za ndizi mbivu, inashauriwa kula ndizi iliyoiva kama tulivyoona wiki iliyopita na pia ule na maganda yake ambayo huwa laini kutafuna na matamu kadri ndizi inavyoiva zaidi. 

Kama hutaweza kula ganda zima, basi angalau hakikisha unalamba nyama na nyuzi nyuzi zote zinazobaki kwenye ganda baada ya kumenya, kwani hivyo ni virutubisho muhimu sana katika mwili wako

Related Posts:

  • VIUNGO NA MATUMIZI YAKE KWA KILA SIKU KWA AFYA YAKO PART 2 Leo nimeona tuangalie baadhi ya viungo, matumizi yake na faida zake kwa afya zetu. Viungo vimekua vikitumika sana kuleta ladha katika chakula au vinywaji mbalimbali,lakini pia huleta afya katika miili yetu.Endelea kusom… Read More
  • CHOROKO HUIMARISHA AFYA YAKO Je wewe ni miongoni mwa wapenzi wa choroko? Kama unatumia utakuwa miongoni mwa wanaofaidika na virutubisho muhimu kwa afya mwilini. Wataalamu waliofanya uchunguzi kuhusu choroko ambayo ni jamii ya kunde, wanasema utam… Read More
  • UWEZO WA AJABU WA JUISI YA KITUNGUU Kuna magonjwa mengine yakikupata hujui hata namna ya kujitibu. Lakini kwa kutumia vyakula na matunda unaweza ukashangaa namna ambavyo unaweza kuliondoa tatizo ambalo pengine ulidhani halina tiba. Katika makala haya ya l… Read More
  • VIUNGO NA MATUMIZI YAKE KWA KILA SIKU KWA AFYA YAKO. Viungo ni kitu muhimu kwenye chakula na huleta ladha ya kufanya  chakula kiwe na hamu zaidi ya kuliwa. Lakini viungo ni si tu huleta  ladha katika chakula lakini pia ni muhimu kwa afya. Leo tuangalie baadhi y… Read More
  • UWEZO WA AJABU WA JUISI YA KITUNGUU-2 leo tunaendelea kufafanua faida zake hasa kwa nywele za binadamu. Jambo muhimu la kuzingatia wakati wa usiku ni muda wa kumaliza kula na kunywa juisi hiyo. Hakikisha unakunywa juisi yako angalau masaa mawili baada ya kul… Read More

0 comments:

Post a Comment