Thursday 31 December 2015

FAIDA ZA MCHAICHAI KWA AFYA YAKO



UJUE MCHAICHAI
Ni wengi wanaoutumia na
kuufahamu mchaichai kama
kiungo cha chakula jikoni na
wengine hutumia kama dawa ya
mbu.
Lakini, je unafahamu kuwa
majani haya yana faida kubwa
kiafya . Mafuta ya mchachai
hutumika katika viwanda
vinavyotengeneza pafyumu na
sabuni.
Tafiti kadhaa zinaonyesha kuwa
mchaichai una vichocheo
muhimu vinavyoweza
kupambana na athari kadha wa
kadha tumboni, kwenye mkojo
na hata kwenye vidonda. Watu
wengine huamini kuwa
mchaichai unaweza kutibu
baadhi ya maradhi kama vile
homa ya matumbo, matatizo ya
ngozi, madhara yanayotokana
na ulaji wa chakula chenye
uchafu na pia hutibu maradhi
ya kichwa na hata misuli.
Mchaichai pia unatajwa kuwa
kinywaji kinachoweza
kupunguza joto. Chai ya
mchaichai inasaidia kupunguza
joto kwa mgonjwa wa homa.
Faida nyingine za mchaichai
kiafya ni pamoja na:
KINGA DHIDI YA SARATANI
Tafiti mbalimbali zimeonyesha
kuwa kwenye kila gram 100 ya
mchaichai, kuna viondosha
sumu ambavyo vina uwezo wa
kuukinda mwili dhidi ya
ugonjwa wa saratani. Mwaka
2006, timu ya watafiti kutoka
Chuo kikuu cha Gurion, Israel
waligundua mchaichai una
uwezo wa kuua seli zinaweza
kusababisha saratani.
MMENG'ENYO WA CHAKULA
-Husaidia umeng’enyaji wa
chakula
Chai ya mchaichai hurahisisha
utaratibu wa mmeng’enyo wa
chakula na pia hutibu
magonjwa ya kuhara na
maumivu ya tumbo ikiwamo
kujaa gesi.
Hurahisisha utaratibu wa
kuondoa uchafu mwilini
Katika matibabu,
unatibu magonjwa
mengi ikiwemo
kushusha joto, hasa kwa
wagonjwa wanaosumbuliwa na
malaria kali.
KUSAFISHA FIGO NA MKOJO
Mchaichai pia una kazi ya
kusafisha figo ambayo kazi yake
kubwa ni kusafisha damu
mwilini, kuondoa mafuta
mabaya mwilini ambayo mengi
yanatengenezwa na kemikali
kiwandani na hivyo mwili
kushindwa kuziondoa na
baadaye kusasababisha
magonjwa mbalimbali ikiwemo
saratani.
Figo inapokuwa safi na imara,
hata kazi nyingine kama
kusafisha mkojo zinafanyika
kirahisi kwani mkojo unapozidi
kuwa mchafu mtu hujikuta
akivimba mwili na wakati
mwingine kufikia hata hatua ya
kupoteza maisha.
MAUMIVU WAKATI WA HEDHI
Mchaichai pia huwasaidia kina
mama ambao wanaumwa na
tumbo kipindi cha hedhi, ambao
wengi wao huchukulia kama
chango.
“Unapokunywa mchaichai,
unawezesha kusafisha mirija ya
uzazi na hivyo kuwezesha damu
kupita kwa urahisi,”
MAJIPU NA MCHAFUKO WA DAMU
vilevile mchaichai una
kazi ya kusafisha damu, hasa
kwa watu ambao wamekuwa na
tabia ya kupata magonjwa ya
ngozi kama mapele na kutoka
majipu
KUZUIA KUHARISHA
Mchaichai pia unaelezwa kuwa
ni dawa ya kuzuia kuharisha
ambapo una uwezo wa
kupambana na mdudu aina ya
protozoa anayesababisha
ugonjwa huo.
MAMA WAJAWAZITO
Endapo mjamzito atatumia
majani ya mmea huu kwa muda
mrefu, ataweza kujiepusha
kujifungua kwa njia ya upasuaji
kwani husaidia katika kulegeza
nyonga ambazo hubana katika
kipindi cha ujauzito na kufanya
njia kuwa ndogo kuwezesha
mtoto kupita,
WENYE VIDONDA VYA TUMBO
Hata hivyo kwa wagonjwa
wanaosumbuliwa hasa na
vidonda vya tumbo, mchaichai husaidia
kuondoa gesi ambazo huwapata
mara kwa mara.
HUONGEZA CD4
Kwa wagonjwa wa ukimwi,
mchaichai unaelezwa kuwa
huongeza CD4 na inashauriwa
kuwa ni vyema mgonjwa wa
aina hiyo akapendelea kutumia
zaidi mchaichai kuliko majani
ya chai.

2 comments: