Thursday 12 March 2015

VYAKULA MAARUFU KWA KUZUIA UVIMBE MWILINI


Vyanzo vinavyoweza kusababisha mlipuko wowote wa uvimbe mwilini na magonjwa mengini ya aina hiyo ni vingi, kutokana na aina ya vyakula tunavyokula, mazingira tunayoishi na hata msongo wa mawazo unaosababishwa na kazi tunazozifanya.
Kwa kawaida mwili umeumbwa kujikinga  wenyewe na kuwa na uwezo wa kupambana na kuzuia maambukizi ya maradhi na milipuko kama hiyo. Ili mwili uwe na uwezo huo, unahitaji uupe uwezo kwa kula vyakula vinavyoongeza kinga mwilini, hasa kinga ya kuzuia uvimbe, miongoni mwa hivyo ni pamoja na hivi vifuatavyo:
MAHARAGE
Jamii yote ya maharage, ikiwemo na soya, inaaminika kuwa na kiasi kingi cha protini na virutubisho vingine vingi vinavyohitajika mwilini kuzuia magonjwa ya mlipuko na uvimbe. Pia vyakula hivi vinafaa kwa wagonjwa wa moyo.SAMAKI NA MAFUTA YAKE
Ulaji wa samaki, hasa aina ya jodari, ni muhimu sana, kwani samaki hawa wana kiwango kingi cha virutubisho aina Omega-3 na 6. Ukiweza, pendelea kula samaki kila mara katika mlo wako wa kila siku. Halikadhalika, utumiaji wa mafuta ya samaki, kiasi cha kijiko kimoja au viwili kwa siku ni muhimu ili kuimarisha kinga ya mwili.
VIUNGO
Katika mlo wako wa kila siku, usipuuzie viungo vya mboga vyenye asili ya miti, kama vile bizari, mdalasini, tangawizi na hiriki. Miti hii ina kiwango kikubwa cha virutubisho vyenye uwezo wa kupambana na kutoa kinga dhidi ya magonjwa ya uvimbe. Hivyo hakikisha kwenye mapishi yako, unaangalia namna ya kuchanganya viungo hivi.
VIAZI VITAMU
Viazi vitamu vina kiwango kikubwa pia cha virutubisho vyenye uwezo wa kung’arisha ngozi, kuimarisha kinga ya mwili na pia afya ya moyo. Kwa upande wa kuzuia magonjwa ya uvimbe, viazi pia vimetajwa kuwa na uwezo mkubwa sana. Mbali ya viazi, pia hata maboga na karoti nazo zina virutubisho vingi vya kuimarisha kinga ya mwili.
CHAI
Unaweza kupamba na magonjwa ya uvimbe na kuupa mwili wako kinga ya mwili dhidi ya magonjwa hayo hata kwa kunywa chai, hasa ya majani ya kijani (green tea), ambayo utafiti wa kitabibu unaonesha kuwa na kiwango kingi cha virutubisho vya kuongeza kinga ya mwili.Kwa ujumla, ni vyema kuwa na kawaida ya kula vyakula asili vya aina mbalimbali na bila kusahau mboga za majani ya aina mbalimbali pamoja na matunda ili kujenga kinga ya mwili imara ambayo itakuwa tayari kupambana, siyo tu na magonjwa ya uvimbe mwilini, bali hata magonjwa mengine hatari.

0 comments:

Post a Comment