Thursday 5 March 2015

FAIDA ZIPATIKANAZO KWA KUTUMIA PILIPILIPI HOHO KIAFYA. Health Benefits of Capsicum (Bell Pepper)



Pilipili hoho Iwe za njano, nyekundu ama kijani, pilipili hoho zinatajwa kuwa mboga yenye vitamin zaidi ya 30. Kila vitamin ina kazi yake katika mwili wa binadamu lakini kubwa zaidi ni pale,

aina hii ya mboga inavyoweza kutumika kama kinga kwa ajili ya baadhi ya magonjwa yanayomkumba binadamu.Pamoja na kuwa na virutubisho vya jumla, vipo vya nyongeza vinavyopatikana na rangi zake.


Watalaamu wa afya kutoka mtandao healthyliving, wanaeleza pilipili hoho ya njano kuwa ni mboga yenye faida nyingi zaidi kiafya. Wanasema licha ya kuwa na ladha ya kipekee, ina uwezo mkubwa ya kuboresha mifumo mbalimbali mwilini. Aina hii yah hoho zina virutubisho vyenye uwezo wa kuongeza kinga ya mwili, kupambana na maradhi ya saratani, moyo na husaidia kuongeza uwezo wa macho kuona.


Wataalamu hao wa afya wanafafanua kuwa, hoho za rangi ya njano ni chanzo kizuri cha virutubisho aina ya lutein na zeaxanthin zinazolinda misuli hususani ya macho.

Kimsingi, hoho za njano ndio mboga pekee yenye zeaxanthin kwa wingi kuliko mboga yeyote. Mahindi ndio yanashika nafasi ya pili nyuma yake.
Virutubisho vingine ni pamoja na vitamin A inayotajwa kuwa muhimu kwa kuongeza uwezo wa kuona wakati wa usiku. Pia vitamin C yenye uwezo wa kuukinga mwili dhidi ya saratani ya utumbo mpana, magonjwa ya tumbo na pia huuwezesha mwili kuponya majeraha kwa haraka zaidi.

0 comments:

Post a Comment