Msongo wa mawazo unaweza kukufanya ushindwe kufanya shughuli zako za kila siku kwa ufanisi. Jambo la kufurahisha ni kuwa msongo wa mawazi unaepukika, leo nimechambua baadhi ya mambo ambayo yanaweza kukuwezesha kuepuka kupata msongo wa mawazo.
1. Usiweke Malengo ambayo Hayafikiki
Kila mtu ana uwezo na vipawa vyake tofauti na mtu mwingine, unapoweka malengo yako hakikisha unazingatia uwezo, vipawa na muda ulionao ili kuweza kuyafanikisha. Usiweke malengo sababu watu wengine wameweka hayo,au ukaweka muda kiasi fulani sababu watu wote wameweka hivyo, daima zingatia uwezo wako ili malengo yako yaweze kufanikiwa na kuepuka kupata ‘stress’.
2. Jifunze Kukubali Changamoto
Katika maisha huwa tunakutana na mambo ambayo hatukutaka kukutana nayo na pia tunashindwa kupata yale tuliyoyataka, karibu kila mtu huwa anapitia hali hii kwa namna moja au nyingine. Jifunze kukabili changamoto na sio kusikitika kwa nini mambo hayajawa kama ulivyotaka na kubaki ukisononeka. Jaribu kukubali mambo kwa busara zaidi, na utulivu huku ukitafakari nini cha kufanya ili kulipata lile ulilo kusudia. Changamoto iwe ni chachu ya wewe kuzidi kukazana na kujaribu zaidi.
3. Fanya Maamuzi Pale Unapopaswa
Kutokufanya maamuzi katika muda sahihi hyleta wasiwasi hofu na msongo wa mawazo. Uwe na ujasiri wa kuamua mara baada ya kutafakari pande zote kwa makini na kuona faida na hasara za kila upande. Usihofu sana juu ya kuweza kufanya makosa hadi ukaishia kupata msongo wa mawazo, mara nyingine watu hujifunza kutokana na makosa.
4. Kuwa na Mipango
Hili nimeshaliongelea sana, angalia hapa . Kutokuwa na mipango ni sababu moja kubwa sana inayoweza kukuletea msongo wa mawazo.
5. Usiweke Jambo Linalokusumbua Moyoni
Pale unapokutana na jambo ambalo umeshindwa kulitatua ni vyema ukamshirikisha mzazi wako au mlezi, rafiki wa karibu, mume au hata mshauri. Jifunze kutokuweka mambo yanayokuumiza moyoni maana katika hali hiyo ni rahisi sana kupata msongo wa mawazo. Uwe na tabia ya kupeleka wasiwasi na hofu zako zote mbele za Mungu kwa maombi na pia kuongea na mtu ambaye unajua atakuwa msaada kwako.
6. Jali Mwili Wako
mara nyingi tunakuwa na shughuli nyingi kiasi cha kuusahau mwili na kuuchukulia tu kwa juu juu. Ni muhimu sana mwili wako uwe katika hali nzuri na afya bora ili uweze kufanya kazi zako vizuri na kwa wepesi. Hakikisha unakula chakula chenye virutubisho bora na pia unakunywa maji ya kutosha. Fanya mazoezi ya viungo mara kwa mara na pata muda wa kutosha wa kupumzika kila siku.
Mungu akubariki sana.
Friday, 2 January 2015
KUKABILIANA NA MSONGO WA MAWAZO NA NAMNA YA KUEPUKANA NA (STRESS)
Related Posts:
MAMBO MATANO YA KUFANYA PINDI UNAPOKUTANA NA MPENZI WAKO ULIYE ACHANA NAE KWA MUDA Dakika chache za kwanza tunapokutana na wapenzi wetu baada ya kuachana kwa kitambo kifupi zinaumuhimu sana.Kitambo hiki ni kile ambacho labda mpenzi wako alikuwa kazini au safarini, umepita muda fulani hamjaonana, yamkini… Read More
NJIA 7 ZA KUHUISHA KUMBUKUMBU KWA UMRI WOWOTE NI jambo la wazi kwamba tunapozidi kuwa wazee huwa tunaanza kugundua mabadiliko kadhaa katika uwezo wetu wa kukumbuka mambo.Hali hii ni kama kujikuta uko jikoni lakini hukumbuki ni kwa nini ulikwenda humo, au kutoweza kuk… Read More
DALILI ZA KUMGUNDUWA MPENZI MKOROFI, MGOMVI. Dalili hizi zitakupa kujihadhari mapema mara utakapoziona zinajitokeza mara kwa mara katika mahusiano yenu. Kusudi la makala hii ni kuwasadia wale wenyematarajio yakuingia katika mahusiano ya kushi pamoja kwa sabab… Read More
NAMNA YA KUISHUGHULIKIA NA KUISHINDA HOFU-3-4 Usijiogopeshe kwa vitu ambavyo hutokea kwa nadra sana.Njia bora ya kuyatengeneza mawazo yetu yanayofikiri sana juu ya hatari ambazo hutokea kwa nadra sana ni kwa kuwaza kuwa wewe hautakuwepo pale hatari hiyo itakapo tokea… Read More
NAMNA YA KUISHUGHULIKIA NA KUISHINDA HOFU Hofu na mashaka ndiyo adui namba moja anayefilisi nguvu au nishati ya mwili wa mwanadamu kwa haraka kuliko kitu kingine chochote. Wengi wameathiriwa katika maisha yao ya kielimu, kiafya, kijamii, kikazi na hata kiuchum… Read More
0 comments:
Post a Comment