Saturday 13 December 2014

VYAKULA VYA KUDHIBITI UGONJWA WA GAUTI (GOUT)



Juisi za mboga na matunda

Mboga zina nafasi kubwa sana katika kupambana na maradhi yanayomkabili mwanadamu na huwa ndiyo kinga ya mwili wakati wote zinapotumiwa. Katika kutibu tatizo la Gauti, juisi ya mchanganyiko wa karoti, tango na Kiazisukari (Carrot, Cucumber & Beet) huweza kusaidia sana.

Tengeneza juisi ya tango na kiazi sukari ya ujazo wa mili lita 100 kila moja, kisha tengeneza juisi ya karoti ya ujazo wa mililita 300, halafu changanya juisi zote tatu ili upate mililita 500 (lita moja) ya juisi yeye mchanganyiko wa mboga hizo tatu na unywe kiasi kila siku.

Kwa upande wa matunda yanayoweza kukupa ahueni na kinga dhidi ya ugonjwa huu ni pamoja na maepo (apple). Tunda hili linajulikana kwa ubora wake katika kutibu Gauti kutokana na kuwa ‘malic acid’ ambayo ina uwezo wa kuiyeyusha ‘uric acid’ inayoleta madhara mwilini. Ili kupata faida ya tunda hili, mgonjwa anashauriwa kula epo moja kila baada ya mlo wake wa kila siku.

Ukiacha Apple,(Tufaha) ndizi nayo imo katika orodha ya matunda yanayoleta ahueni kwa wagonjwa wa Gauti. Dayati ya kula ndizi pekee kwa muda wa siku tatu ama nne, itaweza kumpa ahueni mgonjwa. Ili kupata ahueni kwa kutumia ndizi mbivu, mgonjwa anashauriwa kula ndizi pekee kati ya nane na tisa kila siku kwa siku hizo zilizotajwa hapo juu, na asile tunda lingine.

Limau nalo lina faida kubwa kwa wagonjwa wa Gauti. Kwa mujibu wa utafiti wa kisayansi, Vitamin C, ambayo inapatikana kwa wingi kwenye limau, ina uwezo wa kukinga na kutibu maumivu ya viungo kwa kuimarisha tishu za mwili. ‘Citric Acid’ iliyomo kwenye limau, ina uwezo wa kuyeyusha ‘Uric Acid’ ambayo ndiyo chanzo cha tatizo. Ili kutumia limau kama dawa, kamua nusu limau kwenye glasi na kunywa mara mbili kwa siku.
DAYATI YA MGONJWA WA GAUTI

Ukishajijua kwamba una Gauti, unashauriwa kuzingatia sana vitu unavyopaswa kula na vile ambavyo hupaswi kula. Kwa wagonjwa wenye hali mbaya, wanashauriwa kufanya funga ya kunywa juisi ya machungwa na maji tu kwa siku tatu ama nne, hii ina maana kwamba katika siku hizo, kitu pekee utakachokula kutwa nzima ni juisi ama maji tu.

Baada ya funga hiyo, utaona nafuu kwenye tatizo lako na unashauriwa kufanya funga nyingine ya kula matunda pekee kwa siku tatu ama nne mfululizo. Baada ya hapo, mgonjwa anashauriwa kupendelea kula vyakula vya asili huku akitilia mkazo matunda na mboga mboga.

Epuka ulaji wa nyama, mayai, samaki, chai, kahawa, sukari, vyakula vitokanavyo na unga mweupe (ukiwemo mkate mweupe), vyakula vya kwenye makopo na vya kukaanga.

Mwisho, mgonjwa anashauriwa kukaa sehemu za wazi ili kupata hewa safi na afanye mazoezi ya viungo mara kwa mara na kuacha kuwaza ili kuepuka mfadhaiko wa akili ambao tumeona kuwa unachangia ugonjwa huu

0 comments:

Post a Comment