Thursday 11 December 2014

KUPUNGUA NGUVU ZA KIUME NA MATIBABU YAKE


Tatizo la kupungua au kuishiwa nguvu za kiume linawakabili wanaume wengi mno katika zama za leo, zama za maendeleo makubwa ya sayansi na teknolojia.


Kwa bahati nzuri, matatizo mengi ya nguvu za kiume hutibika, kama matibabu sahihi yatapatikana. Lakini kabla ya kujitibu, ni muhimu kwanza ujue chanzo cha tatizo lako la kuishiwa nguvu za kiume. Watu wengi hukurupuka tu na dawa, hii ndiyo maana wamekuwa hawaponi licha ya kubugia chungu ya dawa, na pia wamekuwa wakipoteza pesa nyingi katika matibabu hayo ya kubahatisha.


Sababu nyingi zinazochangia kupungua kwa nguvu za kiume zinaepukika. Hivyo katika e-mail hii nakusudia kukusaidia jinsi ya kujikinga na jinsi ya kutibu matatizo hayo kama tayari unayo.


Katika e-mail hii leo nitazungumzia sababu za kupungua nguvu za kiume na matibabu yake ya uhakika. Fuatana nami mpaka mwisho.
UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME NI NINI?

Upungufu wa nguvu za kiume ni jina la jumla lenye mjumuiko wa vipengele vingi:
• Kuwahi kufika kileleni au kucheleawa sana kufika kileleni.
• Uume kutosimama vizuri (kusimama kwa ulegevu au kutodumu kusimama).
• Kukosa hamu ya tendo la ndoa.
• Kushindwa kurudia raundi ya pili.
• Kuchukua muda mrefu sana kurudia tendo la ndoa baada ya raundi ya kwanza au kushindwa kabisa kurudia.
• Maumivu wakati wa tendo la ndoa au baada ya tendo la ndoa.
Kukumbwa na moja ya vipengele hivyo au zaidi, tayari wewe ni mwanachama wa

UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME.

SABABU ZA KUPUNGUA NGUVU ZA KIUME
Kusimama kwa uume, kudumu kusimama na kufika kileleni kwa muda mzuri wa kufurahia tendo la ndoa ni mfuatano wa matukio ya matendo kadhaa mwilini. Kudhurika au kuvurugwa kwa tukio lolote la kitendo husababisha kupungua nguvu za kiume.
Nukta muhimu hapa ni kwamba, mtu anayepungua nguvu za kiume, ina maana kuna kiungo au viungo ndani ya mwili wake (tofauti na uume), kimeshindwa kufanya kazi katika utaratibu wake wa kawaida. Baadhi ya maradhi, mtindo wa maisha mbaya na lishe mbovu huweza kusababisha kiungo, au viungo, au mfumo fulani wa mwili kushindwa kufanya kazi.
Matukio ya vitendo hujumuisha mpwito neva (nerve impulses) zinazokwenda kwenye ubongo, uti wa mgongo, eneo linalozunguka uume, mwituko wa misuli, tishu za ufumwele (fibrous tissues), mishipa ya vena na ateri na pia iliyo karibu na corpora cavernosa.
Kudhurika kwa neva, ateri, misuli laini na tishu za ufumwele (fibrous tissues), mara nyingi hasa kwa kutokana na maradhi, matokeo yake ni kupungua nguvu za kiume.
Maradhi kama ya figo, kisukari, pombe, maradhi ya mishipa ya damu na maradhi ya neva, ni sababu ya kupungua nguvu za kiume kwa asilimia 70 ya matatizo yote ya kuishiwa nguvu za kiume.
Hivyo unaposema umepungukiwa nguvu za kiume, hii ina maana ndani ya mwili wako kuna kiungo au viungo kadhaa havifanyi kazi vizuri. Huenda figo haifanyi kazi vizuri au huenda ini lako halifanyi kazi vizuri au moyo hausukumi damu vizuri au tezidume (prostate gland) imevimba hawezi kukontrol shahawa vizuri. Hii ndiyo maana kitaalamu tunasema

KUPUNGUA NGUVU ZA KIUME SIYO UGONJWA NI DALILI YA UGONJWA.
Ni kwamba, kuna viungo zaidi ya 30 ndani ya mwili wa mwanaume vinavyofanya kazi za nguvu za kiume, hivyo inapokea dosari za kiutendaji katika moja ya kiungo au baadhi ya viungo, basi hapo kupungua nguvu za kiume ni jambo lisiloepukika kwa mwanaume yeyote yule hata kama ni mfalme wa nchi. Nini basi kinaweza kusababisha viungo hivyo kutofanya kazi vizuri?
Baadhi ya tabia zetu, magonjwa, vyakula tunavyokula, na mazingira tunayoishi huweza kusababisha utendaji mbovu wa viungo hivyo, na hivyo kusababisha tatizo la kupungua nguvu za kiume. Sababu za kupungua nguvu za kiume ni nyingi sana, ni zaidi ya 200. Hapa tuangalie baadhi yake:



PUNYETO (MASTURBATION)

Kupiga punyeto au kujichua (masturbation) ni kujisisimua kiungo cha tendo la ndoa kwa mkono (au kwa njia nyingine) kwa ajili ya kutoa manii ili kujiridhisha kimapenzi.
Kwa watu wengi hasa vijana, kuishiwa nguvu za kiume ni matokeo ya masturbation.
Majarida, magazeti na picha za video za uchi huongeza madhara kwa vijana na hivyo kushawishi punyeto.
Punyeto ina madhara mengi mno kiafya. Mtu yeyote anayepiga punyeto mwili huwa dhaifu, mapigo ya moyo huongezeka na kumbukumbuku zake huwa dhaifu. Mfumo wa usagaji chakula hudhoofishwa na kuwaka kwa mapafu hutokea. Mtu anaweza pia kupungukiwa damu.
Mtu ambaye amezoea masturbation anakuwa hana uwezo wa kuoa pindi anapofikia umri wa kuoa. Kama ataoa, mke wake atamchukia na wanaweza hata kuachana. Kama mwanamke atakuwa mwanamke mwema mwenye kumvumilia mumewe, hata hivyo atafadhaika sana kiakili.
Baadhi ya waathirika wa punyeto hudhani kwa kuwa walipiga zamani na sasa wameacha hawana athari! Punyeto huleta madhara kwa wakati huo na baadaye. Hata kama ulipiga punyeto siku moja, madhara yake yanaweza kuwa makubwa kinyume na unavyoweza kudhani.
Hata hivyo, hakuna idadi maalumu inayoweza kuchukuliwa kama ni ufanyaji masturbation mkubwa au wa kupindukia (iliyovuka kiwango). Idadi ya masturbation anayoweza kufanya mtu bila madhara hutegemea afya ya mtu huyo na kemia ya mwili wake.
Baadhi ya watu hufanya masturbation kwa muda mfupi katika kipindi fulani, mathalani mwezi mmoja tu au miwili. Na wengine wanaweza kufanya masturbation kwa muda mrefu kiasi cha mwaka mwaka mmoja au zaidi na hata huweza kufikia mara 2 hata mara 5 kwa siku, na wanaweza kufanya kila siku (non stop)!
Kwa hakika hii ni masturbation iliyovuka mipaka, ni lazima itadhikisha ini na kazi za mfumo wa neva na lazima imweke mtu katika uhanisi hata kama ni kijana wa miaka 18, na kwa baadhi ya watu hata ugumba! Wanaume wengi sana walio na umri chini ya miaka 40 wana tatizo la kuishiwa nguvu za kiume kutokana na kujichua (masturbation).
Ni wazi kwamba watu wengi wanapokuwa wanapiga punyeto, wanakuwa hawajui wanachokifanya, kama wangelijua basi wangeliichukia punyeto kama wanavyochukia ukoma!
Masturbation huleta mabadiliko makubwa katika mwili kama ambavyo nimeshagusia. Madhara ya mabadiliko haya ndani ya kemia ya mwili yanaweza kujidhihirisha yenyewe kama uchovu, kupoteza nywele, kupoteza kumbukumbu, kuona ukungu, maumivu ya korodani/kinena, kufika kileleni haraka, kutoka kwa shahawa zenyewe, kushindwa kusimamisha uume vizuri, kukosa uzazi, maumivu ya mgongo/kiuno n.k.
Naam! Hapa sasa tutazame madhara yanayoletwa na masturbation ndani ya mwili, tuchambue kipengele kimoja baada ya kingine kwa kina.


Uume kusimama kwa uregevu
Kama masturbation itafanywa sana kupindukia, huchochea kemikali iitwayo acetylcholine katika mfumo wa neva huria ubongo za parasimpathetiki (parasympathetic nerve). Hali hii inaweza kuzidisha sana kupita kiasi kiwango cha mchocheo, na matokeo yake itaweza kuzalisha sana kupita kiwango cha kawaida homoni zinazohusika na kujamiiana (sex hormones) na neurotransmitters kama vile acetylcholine, dopamine, serotonin na hivyo kusababisha mabadiliko ya kemia ndani ya mwili. Dopamine ni kemikali inayotengenezwa katika ubongo na iko katikati, na ni kipitisha ujumbe (neurotransmitter).

Dopamine huhusika sana na raha. Kichocheo ambacho huzalisha aina yoyote ya mwitikio chanya pia vilevile huchochea utoaji wa dopamine katika ubongo.
Uzalishaji huu mwingi wa kupita kiasi huenda moja kwa moja kudhoofisha mfumo wa viungo vinavyoshughulika na uzazi na tendo la ndoa. Na hatari yake kubwa ni kwamba, kama mtu hatatibiwa mapema, anaweza kuua nguvu za kiume kabisa na hata kujiletea ugumba.

Parasympathetic nerve ni neva yenye jukumu la kusimamisha uume, kama mtu atafanya masturbation ya kupindukia, atazalisha kemikali nyingi ndani ya mwili, na uzalishaji huo hudhoofisha utendaji wa neva hii kwa kuifanyisha kazi kupita kiasi, na hivyo kwa baadaye uume wa mpiga punyeto unaweza kuwa unasimama kwa uregevu. Mfano wake ni kama umeme huu tunaoutumia majumbani mwetu kwa kazi mbalimbali. Pengine tukitumia mfano wa umeme, mtu anaweza kuelewa kwa urahisi zaidi.

Ni kwamba, ndani ya miili yetu pia kuna umeme (bioelectricity). Unapofanya tendo la ndoa unazalisha umeme wa kawaida ndani ya mwili wako katika hali ya kawaida kwa sababu ni mwungano wa jinsia mbili tofauti, ni kama hasi na chanya. Lakini, unapofanya masturbation hali ni tofauti.

Katika masturbation unazalisha umeme/kemikali nyingi sana, kwa sababu ‘unafosi’ umeme kutengenezeka kwa nguvu kwa kupitia chanya tu, umeme huo unaenda kuua vitu vinavyofanyiwa kazi na umeme huo. Ni kama ambavyo tumekuwa tukiona mara kwa mara umeme unapozidi majumbani mwetu, vitu ambavyo vilivyokuwa vikitumia umeme huo kama friji, tv, na kadhalika huungua.

Katika miili yetu hali ni hivyo hivyo. Kwa hali hiyo, wapiga punyeto, watambue wanafanya jambo baya sana, watambue wanajiangamiza kwa mikono yao wenyewe.
Madhara ya kuregea kwa uume kutokana na masturbation, yanaweza kuanza kuonekana mapema au yanaweza kutokea baada ya muda mrefu, kutegemeana na afya ya mhusika na kemia ya mwili wake.
Kufika kileleni mapema

Kudhoofika kwa neva huria ubongo za parasimpathetiki (parasympathetic nerve) husababishwa na masturbation ya kupindukia. Kama ambavyo nimekwishaeleza katika sehemu iliyotangulia, neva hii ndiyo yenye jukumu la kusimamisha uume, pia vilevile neva hii ndiyo yenye jukumu la kufunga milango ya shahawa kwa muda wa kutosha wa kufurahia tendo la ndoa. Pindi neva hii inapokuwa dhaifu, maji ya shahawa hutoka hata kama mtu yuko usingizini, wakati wa ndoto za mapenzi au hata wakati wa msisimko mdogo sana.
Kwa nini mtu afike kileleni mapema kutokana na punyeto? Punyeto kama lilivyo tendo la ndoa, kama ambavyo tumeshaona huzalisha baadhi ya kemikali ndani ya ubongo (acetylcholine, serotonin, na dopamine) ambazo punde tu baadaye huleta raha ya akili na mwili.

Kemikali hizi ni nzuri kwetu kwa sababu hutolewa katika kiwango maalumu. Hatari inakuja kwamba, kama zitazalishwa kwa wingi sana, zina tabia ya kukaa muda mrefu sana ndani ya mwili na kuzalisha madhara ya kimwili na kisaikololojia kama vile kutokuwa makini katika jambo, kupungua uwezo wa kukumbuka mambo, matatizo ya kukosa usingizi na mwili kukosa nguvu (physical lethargy).

Pindi mtu anapopiga punyeto sana, huchochea seli zenye jukumu la uzalishaji wa homoni hizi. Seli hizi haziitiki tu kwa kuongeza utendaji wake wa kazi, bali pia idadi yake huongezeka kuliko kawaida, na hivyo mwili wa mpiga punyeto unakuwa na msisimko mkubwa sana, kiasi ambacho hata mwanamke anaweza kuvua nguo tu, na muathirika wa punyeto akajipizia mwenyewe!

Jambo jingine baya ni kwamba, uzalishaji mwingi wa homoni hizi moja kwa moja huathiri neva ya parasimpathetiki (Parasympathetic nerve) yenye jukumu muhimu la kufunga milango ya maji ya shahawa kiasi cha mwanaume kufurahia tendo la ndoa na kuridhika na mwenza wake.

Hivyo, neva hii inapoathirika, yaani inapokuwa regevu na ufikaji kileleni pia huathirika kwa kiwango kikubwa sana, kwa maana milango iko wazi, kufuli hakuna! Yaani neva inakuwa haina uwezo wa kufunga milango ya shahawa.

Madhara mengine makubwa na hatari yanayoletwa na mpiga punyeto ni kwamba, tendo hili kwa kiwango kikubwa sana hudhuru kiungo muhimu sana kwa mwanaume kinachoitwa tezi-dume au tezi-shahawa (prostate gland). Kiungo hiki kiko chini ya kibofu cha mkojo. Baadhi ya kazi zake kubwa ni kutengeneza maji ya shahawa na ‘kukontroo’ shahawa. Kiungo hiki ndicho jeuri ya mwanaume.

Kwa ufupi tu ni kwamba, prostate gland ndiye dreva; ndiye anayeamua kwamba hapa anafunga breki au hapana.
Tezi hii ndiyo inayoamua kuwa sasa unafika kileleni au hapana. Wapiga punyeto huzalisha umeme mwingi ambao umeme huu huifanyisha kazi sana tezi hii na hivyo kuitanusha sana, na hivyo kuvimba. Inapovimba, ugonjwa ambao kitaalamu tunauita,

Benign Prostate Hyperplasia (BPH),

mpiga punyeto anakuwa anapata tatizo la kufika kileleni haraka, na hata umri utapokwenda zaidi anaweza kupata tatizo la mkojo kiasi cha kuhitaji kufanyiwa upasuaji.

Pia, na kama mtu atafanya masturbation kabla ya kufikia umri wa miaka 21, ajue anajiua kabisa nguvu za kiume. Kwa sababu tezi hii katika wakati huu inakuwa katika ukuaji, inakoma kukua katika umri wa miaka 21.
Hivyo, mpiga punyeto kabla ya muda huo anakuwa anavuruga ukuaji wake na kwa hiyo kujiletea uhanisi hasa kufika kileleni haraka mnoo! Inapovimba tezi hii huwa inapata msisimko mkubwa sana na inakosa kabisa ‘kuntroo ya shahawa’ (ya udhibiti wa shahawa).

Jambo jingine linalosababisha mpiga punyeto afike haraka kileleni ni kudhoofisha misuli inayojulikana kama pelvic floor muscles, misuli hii ndiyo inayofanya kazi ya kufunga na kufungua kutoka kwa shahawa, hupokea amri kutoka katika mfumo wa neva.
Wapiga punyeto hudhoofisha misuli hiyo, na hivyo kuwafanya wafike kileleni haraka sana. Hii misuli ndiyo pia huwa inatumika kufunga mkojo, baadhi ya watu ambao huwa

wanadhoofika misuli hii kutokana na maradhi mbalimbali huwa pia wanapata matatizo ya kukojoa mara kwa mara.
Hizo ndizo sababu zinazofanya wapiga punyeto wafike haraka sana kileleni. Wao wenyewe ni mashahidi, kilio chao kikubwa ni kufika keleleni haraka sana, ni kuingia tu na kumwaga!

Utamkuta mtu ni kijana barobaro ambaye ukimwona unaamini akifanya mapenzi atachukua dakika 30 kufika kileleni, na hata zaidi hapo, na hata mke wake atamwamkia, “Shikamoo mume wangu!”

Yaani anapewa heshima ya kipekee hata kama ana umri mdogo zaidi ya mke wake.Lakini ajabu barobaro huyu atakawambia anafika kileleni ndani ya dakika 1 au 2 au 3!! Huu tayari ni uhanisi!

Hivyo mpiga punyeto aelewe kwamba anapofanya mchezo huo mchafu anaharibu milango yake ya shahawa, anadhuru tezidume, anadhuru misuli.
Wapiga punyeto wamekuwa wakijiuliza kwa nini baadaye wamepata tatizo la ufikaji haraka kileleni? Kwa ufupi sababu zao ni hizo, hivyo matibabu yanapaswa yaanzie katika sababu hizo. Wasikurupike tu kubugia dawa, wanahitaji wapate mtaalamu aliyebobea katika mfumo wa mkojo na mfumo wa uzazi wa mwanaume, siyo kununua dawa mitaani.

Vijana wanaosoma shule za kulala, na wanaopenda kutazama picha za ngono wana tabia hii sana ya kupiga punyeto, waelewe watakuja kukosa heshima ndani ya majumba yao punde muda tu watakapokuwa wako katika maisha ya ndoa. Waelewe watawatesa sana wake zao, kiasi hata hao wake zao kutoka ndani ya ndoa zao, ili wapate mahala pengine (kwa watu ambao hawajapiga punyeto) ili nao wastarehe na kufurahia tendo la ndoa.

Kuna msemo usemao, “Usipofyeka msitu, nyoka na wanyama wabaya wataingia.”
Naam! Kazi ni kwako sasa!
Kama wewe ni mpiga punyeto, ama uliwahi kupiga punyeto zamani, huu ni wakati wa kuchukua hatua haraka sana kuanza matibabu. Unapowahi matibabu unakuwa unatengeneza fursa pana ya kupona, kila mara nimekuwa nikisema, “Unapochelewa utakuta mwana si wako!”


2. MARADHI YA MISHIPA YA DAMU


Sababu kuu ya kushindwa kusimama uume ni kutokana na kunyanzi za ateri kwenye uume, kushindwa kufunguka na kuingiza damu, hivyo kusababisha uume kushindwa kusimama.

Uume kushindwa kusimama ni kudhihirika (kufichuka) kwamba mtu huyo ana tatizo katika mishipa yake ya damu. Hii humaanisha kwamba, kuwepo kwa tatizo katika mishipa ya damu ni moja ya chanzo cha tatizo.
Maradhi ya mishipa ya damu ni ugonjwa ambao utando hujijenga ndani ya mishipa yako ya ateri.

Utando huundwa na mafuta, calcium na vitu vingine vinavyopatikana katika damu. Utando huo huikaza na kuidhikisha mishipa yako ya ateri na kuifanya kuwa miembamba zaidi (yani kuwa na njia ndogo zaidi).

Maradhi ya mishipa ya damu, mafuta mengi, shinikizo la kupanda (hypertension), au kisukari hupunguza au huzuia mtiririko wa damu kwenda kwenye ubongo, moyo, na katika uume na hivyo kusababisha uume KUSHINDWA kusimama.

Maradhi haya, ambayo huchangia kwa asilimia 70 ya sababu za kupungua nguvu za kiume, husababisha kupungua kwa mnyumbuliko wa tishu, pia hupunguza kipenyo cha mshipa. Kama mshipa uliozuiwa ni mshipa wa moyo, itazalisha mshtuko wa moyo (heart attack). Kama mishipa ni ya kwenye ubongo, itazalisha kiharusi (kupooza).


SHINIKIZO LA DAMU LA KUPANDA (PRESHA YA KUPANDA)


Shinikizo la damu la kupanda (High Blood Pressure) kama halikutibiwa mapema kwa usahihi, huweza kuleta matatizo hatari ya kiafya ikiwa ni pamoja na mshtuko wa moyo, kiharusi (stroke), kushindwa kwa figo kufanya kazi (kidney failure), hata kifo n.k.

Baadhi ya watu wanaweza kuwa na presha ya kupanda kwa muda wa miaka mingi bila kuwa na dalili zozote hata kama kipimo kinaonyesha kupanda sana katika kiwango cha hatari. Hata kama huoni dalili zozote, kudhurika kwa mishipa ya damu, moyo, figo n.k, kutaendelea kimyakimya ndani ya mwili wako. Kama tayari una presha ya kupanda ni vizuri kupima mara kwa mara na ni faida kubwa kufanya matibabu mapema.
Shinikizo la damu la kupanda huathiri kwa kiwango kikubwa nguvu za kiume, kwa sababu hudhuru mzunguko wa damu na figo, vitu ambavyo ni muhimu sana katika nguvu za kiume.


SHINIKIZO LA DAMU LA KUSHUKA (PRESHA YA KUSHUKA)


Shinikizo la damu la kushuka ni hali isiyo ya kawaida ambapo msukumo wa damu wa mtu (msukumo wa damu dhidi ya kuta za mishipa ya damu wakati na baada ya pigo la moyo) ni chini zaidi kuliko kawaida, ambayo inaweza kusababisha dalili kama vile kizunguzungu.

Pindi msukumo wa damu unapokuwa chini, kuna utiririkaji wa damu usiotakiwa kwenda kwenye uume, ubongo na viungo vingine muhimu.


UNENE/UZITO MKUBWA


Unene ni hali ya mwili kuwa mnene na mzito mno. Kipimo chake ni uhusiano kati ya urefu wa mtu na uzito wake.

Kuwa mnene mno kunaleta hatari nyingi za kiafya na kusababisha magonjwa kama vile:
• Shinikizo la juu la damu.
• Ugonjwa wa kisukari.
• Ugonjwa wa moyo.
• Kupooza.
• Shida za kupumua.
• Matatizo ya viungo vya miguu na kwenye uti wa mgongo.
Watu wanaonenepa sana hufa mapema na kuwa na magonjwa mengi kuliko watu wasio wanene ambao hula kiasi kulingana na wanavyohitaji chakula.
Unene huwa unaambatana na mafuta mengi mwilini. Mafuta hayo wakati mwingine huzidi kwenye kuta za ndani za mishipa ya damu na hivyo kupunguza ukubwa wa mrija kiasi kwamba damu itapita kidogo na kwa shida.

Hii huchangia kupungua kwa nguvu za kiume kwa sababu kiasi cha damu kinachotakiwa kusimamisha uume kitakuwa kidogo sana. Wakati mwingine uume unaweza kusimama kidogo na kulala kabla shughuli haijakamilika.

Uume unaendeshwa kwa mfumo wa majimaji (hydraulic system). Damu inatakiwa iufikie uume ili itanuke.
Uzito mkubwa huvuruga uwiano wa homoni na hivyo uzalishaji wa homoni muhimu kwa ajili ya kusimamisha uume unakuwa hautoshelezi.
Ufumbuzi wa kwanza wa mtu mwenye mafuta mengi mwilini ni kufanya mazoezi na kupunguza uzito.


KITAMBI


Kitambi kinahusiana na hatari kubwa ya maradhi ya moyo, shinikizo la damu la kupanda, uzuiliaji wa insulini, kisukari. Kwa kuongezeka kiuno hadi kwenye nyonga hatari ya kifo huongezeka pia.

Sababu kubwa za kitambi ni urithi, mfumo mbaya wa lishe, msongo, ukosefu wa mazoezi, tatizo la uvunjajivunji wa kemikali mwilini. Kitambi hupunguza nguvu za kiume kwa kiwango kikubwa sana kwa njia zifuatazo:
• Mafuta yalio ndani ya tumbo hubadalisha homoni ya kiume ya testestorone kuwa homoni ya kike estrogen.
• Mafuta ya tumboni huharibu mzunguko wa damu na kudhuru kemikali ya nitric oxide ambayo husaidia kutanua mishipa ya damu kwa ajili ya damu kuingia uumeni.
• Mafuta yaliyo kwenye kitambi hudhuru misuli pelvic floor muscles kwa kuikunja kutokana na kuibebesha uzito mkubwa. Misuli hii ina kazi ya kusaidia kusimamisha uume vizuri na kuzuia shahawa kutoka mapema.
• Mafuta yaliyo katika tumbo hudhuru afya ya tezidume kwa kiwango kikubwa sana, tezi hii ndiyo jeuri ya mwanaume.
Kitambi kina madhara mengi sana kiafya na ni chanzo cha magonjwa mengi ikiwa ni pamoja na kisukari, shinikizo la damu la kupanda.


KISUKARI


Kisukari ni moja ya matatizo makubwa mno yenye kusababisha upungufu wa nguvu za kiume, kwa sababu kisukari huleta mabadiliko katika utiririshaji wa damu na kudhuru sehemu za mwisho za neva. Husababisha mishipa ya neva na ateri kudhurika na hivyo hudhuru uwezo wa ubongo kupitisha matakwa yake kwenda kwenye mwili hali ambayo pia huufanya uume kushindwa kusimama.

Kisukari ni ugonjwa unaoathiri mishipa ya fahamu na kufanya mishipa ya damu kutofanya kazi yake vizuri ili kuruhusu damu kujaa kwenye uume. Hii humfanya mgonjwa wa kisukari kushindwa kusimamisha uume hata kama ana hamu ya kufaya tendo hilo.

MARADHI YA MOYO


Maradhi ya mishipa ya damu, kama vile kukakamaa kwa mishipa ya ateri, au maradhi ya moyo husababisha kupungua kwa mtiririko wa damu na hivyo kuuondolea uume uwezo wa kupokea damu ya kutosha itakayosababisha uume usimame.

Kuishiwa nguvu za kiume hutokea sana kwa wagonjwa wa moyo. Mazoezi ya kawaida yanaweza kusaidia kwa wanaume wenye matatizo ya moyo.


SIGARA


Wanaume wanaovuta sigara wana hatari kubwa ya kuishiwa nguvu za kiume; na kadiri wanavyovuta sigara nyingi ndivyo hatari inavyokuwa kubwa zaidi. Nikotini iliyo ndani ya sigara huzuia damu kuingia kwenye uume na hivyo kusababisha kupungua nguvu za kiume.

Sigara huleta madhara kwenye mishipa ya ateri na hivyo (mishipa hiyo) hushindwa kutiririsha damu katika utaratibu wake wa kawaida, na pia hudhuru ateri zilizo katika uume na hivyo kupunguza mtiririko wa damu ambao ni muhimu katika kusimamisha uume.
Nikotini huifanya mishipa ya damu kubana, jambo ambalo ndiyo sababu ya kuishiwa nguvu za kiume kwa wavutaji wengi wa sigara.

Wanaume wanaovuta sigara kwa muda wa miaka 20 huziba kabisa mishipa ya ateri.
Pia, sigara hupunguza kiwango chako cha utungaji mimba. Hupunguza kiwango cha kufika kileleni. Sumu zilizo ndani ya sigara hudhuru shahawa ikiwa ni pamoja na kupunguza kiwango cha mbegu na kuifanya mbegu kuwa na umbo lisilo la kawaida.


MARADHI YA INI


Ini ni Mfumo wa Uchujaji, Kiwanda cha Kemikali, na Ghala.
Ini ni moja ya kiungo kikubwa ndani ya mwili, lina mchango mkubwa katika michakato mingi ya uhai ndani ya mwili, ikiwa ni pamoja na:
• Kuvunjavunja chakula kuwa kemikali zinazohitajika katika miili yetu.
• Kuzalisha nyongo (inayohitajika kwa ajili ya usagaji wa chakula).
• Kutunza na kudhibiti kiwango cha sukari, vitamini na madini.
• Kudumisha uwiano wa homoni.
• Kuondoa sumu kutoka ndani ya mirija ya damu, na zaidi.
Hii ndiyo maana pindi ini lako linapokwenda kombo, vitu vingi ndani ya mwili wako huathirika ikiwa ni pamoja na uume wako.


MARADHI YA NEVA NA UBONGO


Mfumo wako wa neva, ambao hujumuisha ubongo, uti wa mgongo, neva za ukingoni na neva zinazojiendesha, huratibu miondoko yote, fikra, na hisia ulizo nazo.

Mfumo wa neva ndiyo hufanya uhisi mazingira ya nje na ndani; na ndiyo unaowasilisha habari kati ya ubongo wako na uti wa mgongo na tishu zingine. Huratibu matendo ya hiari.

Mfumo wa neva huratibu na kurekebisha kazi zisizo za hiari kama kupumua, mapigo ya moyo, msukumo wa damu na halijoto la mwili.
Ubongo ni kituo cha mfumo wa neva, kama ilivyo microprocessor katika kompyuta. Uti wa mgongo na neva ni viunganishaji kama milango na waya katika kompyuta. Neva hubeba mapigo ya kemikali umeme kwenda na kutoka katika sehemu mbalimbali za mfumo wa neva; pia vilevile kati ya mfumo wa neva na tishu zingine na viungo.

Mfumo wa neva una mchango mkubwa sana katika zoezi zima la kusimamisha uume.
Pindi mwanamme anaposisimkwa kimapenzi kwa kushikwa, mshiko huo hukamatwa na neva ndani ya ateri zilizo ndani ya uume.

Kisha neva husababisha kemikali iitwayo nitric oxide kuruhusiwa kuingia katika ateri. Hii huifanya ateri kuwa kubwa (yaani kutanuka) na kujaa damu. Hivyo hii huufanya uume kujaa damu na kuwa mkubwa na mgumu.
Corpora cavernosa hugandamiza mishipa ya damu iitwayo vena ambayo huruhusu damu kutoka nje ya uume. Kwa kuwa damu ndogo ndiyo hutoka nje ya uume kupitia vena, damu nyingi hubaki ndani ya uume.


Wakati wa kusimama uume vali huzuia mkojo usiingie kwenye urethra kiasi kwamba ni majimaji ya shahawa ndiyo hupita tu. Hii ndiyo sababu ni vigumu kwa mwanaume kukojoa wakati uume umesimama ndani ya tendo la ndoa.

Mwanamme pia huamshwa kimapenzi bila ya kushikwa, kwa mfano, kama atamwona mwanamke ambaye yuko uchi, au anafikiria kufanya mapenzi na mwanamke. Katika hali hii, ubongo wake hutuma ujumbe kupitia uti wa mgongo kwenda kwenye uume. Ubongo pia unaweza kuzuia uume usisimame, hata kama mwanamme anashikwa kimapenzi.

Ugonjwa wa kukacha seli, ugonjwa wa kutetemeka, majeraha kwenye uti wa mgongo, kisukari na kiharusi huduhuru uwezo wa ubongo kuitikia msisimko wa mapenzi.
Matatizo hayo husababisha muingiliano katika kupitisha mpwito neva kati ya ubongo na uume, hivyo upungufu wa nguvu za kiume, ni matokeo yake.

Kupata majeraha kwenye uti wa mgongo au ubongo inaweza kusababisha kupungua nguvu za kiume.
Ukiwa na Tatizo la Upungufu wa Nguvu za Kiume unaweza kunitafuta mimi nitaweza kukusaidia kunipata mimi bonyeza hapa. Mawasiliano

1 comments:

  1. Kutana na mtaalamu wa mitishamba anatibu .kansa..ugumba uti sugu...uzazi..ini..mapafu ..kisukar ...tb..bp..nguvu zza kiume..kurefusha uume ..kuongeza hips na makalio..cd 4 za ukimwi..mpigie dr kupitia 0744903557 tanga

    ReplyDelete