Saturday 29 November 2014

WATOTO WALIOZALIWA MASIKA HUWAHI KUTAMBAA




Utafiti uliofanyika hivi karibuni nchini Israel unaonyesha kuwa watoto wanaozaliwa majira za masika huwahi kutambaa zaidi ikilinganishwa na wanaozaliwa msimu wa kiangazi.


Kwa mujibu wa ripoti ya utafiti huo, watoto waliozaliwa wakati wa masika huanza kutambaa wakiwa na wiki 30 wakati wanaozaliwa majira ya kiangazi hufikia hatua hiyo baada ya wiki 35.
Ripoti hiyo inaeleza kuwa mara nyingi watoto wanaozaliwa majira ya masika hufikisha wiki 30 wakati wa kiangazi ambacho huambatana na joto hali inayomsababisha mtoto kupenda kucheza chini.

Kulingana na matokeo hayo, jopo la wataalam walioshiriki kwenye utafiti huo limewataka wazazi kuwa makini katika kuangalia mienendo ya watoto wao na wakati mwingine kuwasaida wanapofikia hatua ya kutaka kutambaa.

0 comments:

Post a Comment