Monday, 24 November 2014

UWEZO WA AJABU WA JUISI YA KITUNGUU-2


leo tunaendelea kufafanua faida zake hasa kwa nywele za binadamu.
Jambo muhimu la kuzingatia wakati wa usiku ni muda wa kumaliza kula na kunywa juisi hiyo. Hakikisha unakunywa juisi yako angalau masaa mawili baada ya kula chakula chako cha mwisho jioni.
Kama tatizo lako ni kubwa, kunywa juisi hii asubuhi na jioni hadi utakapoona tatizo la kutoka damu wakati wa kujisaidia limetoweka.Kwa kawaida tatizo huweza kutoweka ndani ya siku tatu au saba tu.
Lakini tatizo lako kama ni sugu, unaweza kutumia kwa muda mrefu kidogo, lakini bila shaka litaisha. Watu wengi wametumia tiba hii rahisi kuondoa tatizo hilo bila kulazimika kufanyiwa upasuaji.
TAHADHARI
Kiasi unachotakiwa kunywa kwa mara moja kisizidi glasi moja ndogo. Utakapokunywa kwa mara ya kwanza utajisikia vibaya na kichefuchefu, hali hiyo ni ya kawaida, jikaze na baada ya muda utajisikia vizuri. Inashauriwa usinywe ukiwa umekunywa pombe au ukiwa ulilala na pombe kichwani, kwani lazima utatapika.
Dozi hii ni kwa ajili ya kutibu tatizo la ‘Hemorrhoids’ kama tulivyoeleza hapo awali. Hata hivyo wakati ukitibu tatizo hilo maalum, utakuwa pia unajitibu au kujipa kinga ya maradhi mengine kama utakavyojifunza kwenye makala haya baadaye.
Wiki ijayo tutakueleza namna ya kutumia juisi ya kitunguu kama tiba ya kutibu upara na kuimarisha nywele na kuondoa mabaka kwenye ngozi.
KUOTESHA NYWELE
Utafiti kadhaa wa kisayansi uliofanywa kuhusu kitunguu, pamoja na faida zingine zilizoelezewa hapo juu, umebaini pia kitunguu kina virutubisho vingi vyenye uwezo wa kusaidia ukuaji na uimarikaji wa nywele.
Nywele za ‘kipilipili’ zinaweza kuwa ndefu na zile zenye tabia ya kukatika zinaweza kuimarika kwa kutumia tu juisi ya kitunguu. Kwa hili huhitaji kutumia madawa ya nywele ya gharama kubwa na yenye kemikali hatari kwa ngozi yako. Aidha, kitunguu kinaweza kuotesha nywele hata kwenye upara.
JINSI YA KUTUMIA
Kama tulivyoelezea wiki iliyopita, andaa juisi yako ya kitunguu na kisha pakaa sehemu unayotaka kuotesha au kuimarisha nywele zako. Unaweza kujipaka juisi ya kitunguu kichwani kama unavyojipaka mafuta, ila hakikisha unapitisha vidole vyako kwenye shina la nywele, usipakae juu ya nywele tu.
Kwa wale wenye kuotesha nywele kwenye upara, wanaweza kujipaka juisi ya kitunguu moja kwa moja kwenye kipara kama mafuta au wanaweza kukata kitunguu katikati na kutumia kipande cha kitunguu kujisugua nacho kwenye upara.
Itapendeza zaidi kufanya zoezi hili usiku wakati wa kulala.
Hali kadhalika wenye matatizo ya ngozi, watumie juisi ya kitunguu kujipaka sehemu zilizoathirika kama upakavyo mafuta.
Kwa maeneo sugu, pakaa mchanganyiko wa juisi ya kitunguu na unga wa bizari, acha kwenye ngozi ukae kwa muda usiopungua saa moja kabla ya kuosha. Juisi hii hutibu magonjwa yote ya ngozi ikiwemo chunusi na vipele.

0 comments:

Post a Comment