Wednesday, 26 November 2014

TATIZO LA UKOSEFU WA USINGIZI NI DALILI YA MARADHI YA ALZHEIMER





Picha ya Kopyuta ikionyesha athari za Alzheimer

Tatizo la kukosa usingizi huenda likawa ishara ya kutambua mapema maradhi ya kupiswa na akili au ''Alzheimer'' kwa mujibu wa utafiti uliofanywa kwa kutumia panya ambaye ana maumbile yanayofananishwa na binadamu.

Vipande vya protini, kwa lugha ya kitaalamu (plaques) au utando kwenye ubongo yanadhaniwa kuwa sehemu nyeti inayosababisha maradhi haya.

Utafiti uliofanywa na kuchapishwa katika jarida la tafsiri ya matukio ya Sayansi, umeonyesha kuwa punde chembe chembe za utando ule ulipoanza kumea kwenye ubongo wa panya, usingizi ukaanza kuwa tatizo kwa viumbe hao.

Taasisi inayosimamia utafiti wa maradhi hayo, (Alzheimer's Research UK) imehimiza kuwa ikiwa uhusiano huo unaweza kuthibitishwa huenda ikawa muhimu kwa Madaktari.

Utafiti wa kutaka kugundua mapema kama mtu anaelea kukumbwa na maradhi ya Alzheimer inadhaniwa kuwa muhimu katika kutibu maradhi hayo.
Mgonjwa wa kupiswa na akili

Wagonjwa hawaonyeshi dalili kupitia hisia au kumbukumbu zao hadi baada ya mda mrefu wa maradhi kumkumba mgonjwa. Yanapofikia hapa sehemu za ubongo huwa zimeharibika kiasi

kwamba tiba inakua vugumu kupatikana au hata kushindwa kupatikana.
Ndiyo sababu wataalamu wanafanya juhudi za kuanza mapema kugundua kama mtu atapata maradhi haya, miaka kadhaa kabla ya dalili hizo kujitokeza.

Viwango vya protini ijulikanayo kama beta amyloid kimaumbile hupanda na kushuka miongoni mwa binadamu na pia panya katika kipindi cha saa 24. Hata hivyo ni ile protini ambayo husababisha utando usiofutika kwenye ubongo na maradhi ya Alzheimer.

Majaribio yaliyofanywa katika Chuo Kikuu cha Washington yameonyesha kuwa panya wanaotoka usiku kwa kawaida hulala kwa dakika 40 kwa kila saa mchana. Lakini ubongo ulipoanza kupatwa na uchafu panya hawa wakaanza kusinzia kwa dakika 30 pekee.

Mmojapo wa wataalamu, Prof David Holtzman, alisema: "endapo mapungufu katika usingizi huanza mapema kiasi hiki katika ugonjwa wa Alzheimer, mabadiliko hayo yanaweza kutupa ishara ya wepesi wa kuweza kuyatambua maradhi haya."
Utando kwenye ubongo

"ikiwa matatizo haya ya usingizi yapo, hatuelewi hasa yanachukua mfumo gani, kupungua kwa usingizi kikamilifu au ni tatizo la kushindwa kabisa kulala au ni kitu tofauti kabisa."

Hata hivyo, utafiti unaofanyika kwa kutumia panya mara nyingi hayafai kutumika kwa binadamu kwa sababu nyingi zinzosababisha kutatizika na usingizi.

Dr Marie Janson, kutoka shirika la kujitolea Alzheimer's Research UK, ametaka utafiti zaidi ufanywe kwa kuwapima binadamu kuona kama kuna uhusiano baina ya matatizo ya kukosa usingizi na ugonjwa wa Alzheimer.

Aliongezea kuwa: "tayari umekuepo utafiti unaounganisha mabadiliko katika usingizi huchangia katika matumizi ya ubongo kwa fikra, lakini matokeo haya yanaonyesha kuwa kuna uwezekano kwamba mapungufu katika usingizi pia inaweza kuwa ishara na onyo la maradhi ya kusahau

Related Posts:

  • FAHAMU AINA ZA KIHARUSI (STROKE)-2 WIKI iliyopita tulielezea ugonjwa wa kiharusi na aina zake na tukafafanua kwa nini unawapata watu. Endelea kuelimika. Iwapo mgonjwa ataathirika sehemu ya ubongo kwenye shingo kuelekea kwenye uti wa mgongo (brainst… Read More
  • VYAKULA VINAVYOONGOZA KUONGEZA AKILI KWENYE UBONGO BILA shaka ubongo ni miongoni mwa viungo muhimu vya binadamu lakini ni watu wachache sana wanaoutilia maanani. Ubongo ndiyo kiungo kinachohusika na utendaji kazi wote wa mwili na ndiyo unaowezesha mwili kuishi maisha ya … Read More
  • FAHAMU AINA KUU ZA KIHARUSI (STROKE) - 3 WIKI mbili katika safu hii tumekuwa tukijadili tatizo la kiharusi (stroke) na kufafanua aina za ugonjwa huu. Endelea kuelimika. Iwapo mgonjwa ataathirika sehemu ya ubongo kwenye shingo kuelekea kwenye uti wa mgongo (bra… Read More
  • JINSI YA KUBORESHA USINGIZI WAKO MATATIZO YA KUKOSA USINGIZI yamekuwapo tangu zamani. Leo mamilioni ya watu hawapati usingizi wa kutosha. Kulingana na mtaalamu wa usingizi kutoka Brazili Rubens Reimão, inakadiriwa kwamba asilimia 35 ya watu ulimwengu… Read More
  • TATIZO LA UKOSEFU WA USINGIZI NI DALILI YA MARADHI YA ALZHEIMER Picha ya Kopyuta ikionyesha athari za Alzheimer Tatizo la kukosa usingizi huenda likawa ishara ya kutambua mapema maradhi ya kupiswa na akili au ''Alzheimer'' kwa mujibu wa utafiti uliofanywa kwa kutumia panya … Read More

0 comments:

Post a Comment