Thursday, 9 October 2014

JUA UGONJWA WA GOITA,DALILI PAMOJA NA TIBA YAKE




Baada ya somo mwanafunzi ajue mambo yafuatayo:-
1. Maana ya upungufu wa madini joto mwilini
2. Dalili za upungufu wa madini joto mwilini
3. Sababu za kupata upungufu wa madini joto mwilini
4. Jinsi ya kuzuia upungufu wa madini joto mwilini na
5. Matibabu ya upungufu wa madini joto mwilini.
1. Maana ya upungufu wa madini joto mwilini.



Huu ni uvimbe usio wa kawaida katika kikoromeo(Thyroid Gland) ambao hutokea mbele ya shingo)



2. Dalili za upungufu wa madini joto mwilini (Goita)
i. Uvimbe mbele ya shingo
ii. Mama wajawazito kuharibu mimba
iii. Kudumaa mwili na akili
iv. Mtoto kufia tumboni
v. Kuzaliwa mtoto njiti (uzito pungufu au premature)
vi. Kutetemeka na kuwa na wasiwasi.
vii. Macho kutoka nje



3. Sababu za kupata upungufu wa madini joto mwilini.
i. Kupungua kwa IODINE katika chakula
ii. Lishe duni
4. Jinsi ya kuzuia upungufu wa madini joto mwilini
i. Kutumia chumvi yenye Iodine (ayodini) hasa ile ya baharini
ii. Kutumia vyakula vyenye Iodine(ayodini) kwa wingi kama vile dagaa, maziwa nk.
iii. Kutoa elimu ya afya kwa jamii kuhusu umuhimu wa lishe bora na
iv. Kumpeleka mgonjwa hospitali iwapo ameshaanza dalili



5. Matibabu ya upungufu wa madini joto mwilini
i. Mgonjwa ataagiziwa dawa ya Iodine na daktari
ii. Tumia dawa kama utakavyoagizwa na

iii. Operesheni itakayofanyika kama tezi imekuwa kubwa na athari zake zimeonekana 

Related Posts:

  • UGONJWA WA MAFINDOFINDO KWA WATOTO  ​ ​KWA UFUPI Dhana hii potofu imesababisha wazazi wengi kuwapiga marufuku watoto wao kutumia wakidhani ndiyo chanzo kikuu. Leo nitaelezea ugonjwa huo wa mafindofindo ama kwa kitaalamu&nb… Read More
  • USAFI WA KINYWA NA UTUNZAJI WA MENO leo tutazungumzia usafi wa kinywa na umuhumu wake na jinsi utunzaji wa sehemu hiyo ya mwili unavyoathiri afya ya mtu kwa ujumla. Karibuni. Afya ya kinywa ina umuhimu mkubwa zaidi ya unavyoweza kufikiria na kwa ujumla … Read More
  • MARADHI YA FIZI NA MENO Aina za maradhi ya fizi na dalili zake Kupiga mswaki na kutunza meno sio suala gumu na iwapo tutapiga mswaki ipaswavyo pamoja na kutumia nyuzi kusafisha katikati ya meno, tunaweza kuzua maradhi ya fizi na pia meno … Read More
  • JINSI YA KUJIKINGA NA KUONDOA HARUFU MBAYA MDOMONI! WATU wengi husumbuliwa na tatizo la kunuka mdomo bila hata kujijua hivyo kuwa kero kwa wenzao na wakati mwingine hujishushia hadhi mbele ya jamii. Mara nyingi ugonjwa wa kunuka mdomo (Halitosis) husababishwa na uchafu… Read More
  • KUTOKWA NA VIDONDA MDOMONI NA MATIBABU YAKE Vidonda mdomoni husababisha sana maumivu makali pamoja na kumfanya mtu asiweze kuongea vizuri na watu.Vidonda hivi husababishwa na kutafuta kwa muda mrefu hasa bigijii au kitu chochote, uvutaji wa sigara,maa… Read More

0 comments:

Post a Comment