Friday 31 October 2014

FAHAMU JINSI YA KUKABILIANA NA MINYOO ILETAYO MAGONJWA




Minyoo ni viumbe hai ambavyo husababisha madhara ya kiafya kwa mtu aliyeambukizwa.minyoo huishi na kukua katika utumbo ambamo hufyonza virutubisho ambavyo ni muhimu kwa lishe ya binadamu.aina ya minyoo inayosababisha kichocho huishi katika kibofu cha mkojo.

Minyoo kwenye utumbo huchangia kwa kiasi kikubwa katika kudhoofisha lishe ya binadamu,hupunguza uwezo wa mtu wa kufanya kazi,udumavu wa akili na madhara mengine. Minyoo ya tumbo inayomwathiri mwanadamu ni pamoja na minyoo mviringo.minyoo ya safura,minyoo mjeledi,ninyoo sindano,minyoo uzi na tegu.

Dalili za uambukizo wa minyoo ya kwenye utumbo ni:

1. Kuwashwa mwili na sehemu ya haja kubwa.
2. kukohoa kikohozi kikavu
3. kukosa hamu ya kula
4. kuumwa tumbo na wakati mwingine kuharisha.
5. Udhaifu wa mwili na kuckoka kwa mara kwa mara
6. Kuvimba tumbo.
7. Kutapika
8. Utumbo kutoka nje ya unyeo
9. Kutoa minyoo kwa njia ya haja kubwa, kutapika minyoo au minyoo kutoka puani.
10. Kizunguzungu
11. Kupauka kwa fizi, ulimi na utando wa macho.
12. Kuvimba miguu.

Aidha kuna athari zinazosababisbwa na minyoo kwenye utumbo kama vile udhaifu wa mwili, utumbo kuziba, kuumwa tumbo, kudumaa kiakili, utapiamlo, upungufu wa wekundu wa damu mwilini na kifo.

 Minyoo huambukizwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine kwa njia mbalimbali kama vile kula kinyesi cha mtu aliyeathirika kupitia chakula,maji, udongo au matunda, kutonawa mikono baada ya kutoka chuoni. Njia nyingine ni maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto aliye tumboni.

Ili kujilinda na minyoo tunashauriwa kudumisha usafi haswa usafi binafsi kwa maana ya kunawa mikono kwa sabuni mara baada ya matumizi ya choo na kabla ya kushika chakula, kuosha kikamilifu matunda, mboga za majani na vyakula, kupika nyama vizuri ili kuuwa minyoo inatokaa katika nyamaa, mama mjamzito kuhudhuria clinic na kupatiwa dawa za kujikinga yeye na mtoto dhidi ya minyoo . watoto chini ya miaka mitano kuhudhuria clinic ili kupatiwa dawa ya kujilinda na minyoo kikamilifu.

Tanzania bila minyoo inawezekana kama tutazingatia ushauri wa wataalamu wa afya.

0 comments:

Post a Comment