Saturday 27 September 2014

SABABU ZA TATIZO LA KUTOPATA MIMBA - 2


Mpenzi msomaji, naendelea kuelezea sababu za mwanamke kutoweza kupata ujauzito. Tuwe pamoja...
Wanaume wengi wanashindwa kumpa mimba mwanamke kutokana na kutumia dawa  hovyohovyo au kuwa na matatizo ya tezi za thyroid, kuwa na ugonjwa wa kansa na matumizi ya kahawa na matatizo mengine ya kimwili.
Pia matatizo ya utokaji mbegu (manii), maumbile yasiyo rasmi na muonekano wa mbegu za kiume, upungufu wa mbegu za kiume, mbegu kutokuwa imara, tezi la kende kupanda juu tumboni, tatizo la vichocheo vya testosterone kupungua mwilini na kuwa na maambukizi ya vijidudu ndani ya viungo vya uzazi vya mwanaume.
Mwanaume pia anaweza kuwa na matatizo ya kurithi kama tatizo la kupeleka mbegu vizuri ukeni kama upungufu wa nguvu za kiume (sexual essues), kumwaga nje mbegu za kiume, kuziba kwa mishipa ya uzazi ya mwanaume kutotengenezwa mbegu (no semen) na kadhalika.
Matatizo ya kimaisha kwa mwanaume kama vile mfadhaiko (stress) au msongo wa mawazo, utapiamlo, ulevi wa kupindukia na matumizi ya madawa ya kulevya, umri kuwa mkubwa zaidi ya miaka 70.
Matatizo ya mazingira mabaya kwa mwanaume kama matumizi ya dawa za kuua wadudu watambaao katika viungo vya uzazi vya mwanaume, kupata joto kupita kiasi kama kuendesha magari ya mizigo ambapo dereva hukaa kitini kwa zaidi ya saa 10 na kufanya sehemu aliyokalia kupata joto sana pia matumizi ya tumbaku na sigara kwa wingi.
Kuchanganua mtu mwenye tatizo la kutopata ujauzito huhitaji kwanza mama na baba wote kwenda hospitali kuonana na daktari ili apate maelezo sahihi na waweze kupata mafunzo sahihi.
Vipimo kwa upande wa wanawake
Kipimo cha upevushaji wa mayai kupima mirija  ya uzazi, upasuaji mdogo kwenye tumbo na kumulika ndani. ya mwili wake ultrasound ya kizazi na vinginevyo.
Vipimo kwa upande wa wanaume
Baada ya kuchukua historia  ya mgonjwa  kwa urefu  kinachofuata  ni vipimo vya kuangalia kama yupo kawaida  au kama kuna hitilafu. Vipimo hivyo  ni kumchunguza  mwanaume kwa ujumla  hali ya afya  yake kwa kumpima kuanzia kichwani hadi miguuni.
Kupima mbegu zake,  kupima vichocheo vyake vya uzazi, kupima na ultrasound kwenye korodani zake.
Ushauri Muda wa kufanya tendo la ndoa kabla ya upevukaji wa mayai huzingatiwa  kuhesabu vizuri  kwa kutumia kalenda  kuanzia siku  ya kwanza  ya kutoka hedhi  ambapo  mtu mwenye  mzunguuko mfupi ni siku 28 hivyo hutoa siku 14 na kubaki zingine 14 ambazo  ndiyo siku  ya kuweza  kuwa yai  limepevuka.
Kwa hiyo,  tunashauri kufanya tendo la ndoa kuanzia  siku ya nne hadi ya tano kabla siku ya kupevuka kwa yai.Mwanamke anashauriwa kulalia mgongo huku umeinua magoti baada ya kufanya tendo la ndoa  kwa muda wa dakika 20.
Kutotumia mafuta yoyote ya kulainisha  uke kwani  baadhi ya mafuta  huuwa mbegu za kiume.
Kuacha kuvuta sigara kwa mwanaume na mwanamke  kwani uchunguzi  huonyesha  kuwa uvutaji  wa sigara  unasababisha ugumba na utasa.
Kupunguza uzito kwa mwanamke na mwanaume na kutumia vidonge vya madini  ya foric acid kwa ushauriwa daktari kumeonyesha msaada mkubwa kwa akina mama wanaopata shida ya kupata mimba.
Upimaji wa mbegu za kiume
Mbegu za kiume baada ya kutolewa zinatakiwa kufikishwa maabara kabla ya dakika 30 kwa upimaji.
Mwanaume anashauriwa kukaa siku 3 bila kuwa amefanya tendo la ndoa na ndipo atoe mbegu zake. Ujazo au wingi wa mbegu kawaida ziwe zaidi ya milioni mbili. Kwa kawaida wingi wa mbegu ni zaidi ya milioni 25.
Mbegu zenye afya zinazoweza kuogelea vizuri na kukimbia zinafanya zaidi ya asilimia 40 kuwa na uwezo wa kutembea vizuri.Wakati wa kupimwa, wataalamu huangalia jinsi mbegu zinavyofanana umbo.
Vitu vingine tunavyoangalia  kwenye mbegu ni kama PH ya mbegu ambapo kawaida  ni 7.2 hadi 8.0. Ikiwa kwenye mbegu kuna chembechembe nyingi  nyeupe za damu na kipimo kinaonesha hivyo basi hali hiyo huashiria kuwa kuna maambukizi ya vijidudu kwenye hizo mbegu za kiume.


0 comments:

Post a Comment