Usijiogopeshe kwa vitu ambavyo hutokea kwa nadra sana.Njia bora ya kuyatengeneza mawazo yetu yanayofikiri sana juu ya hatari ambazo hutokea kwa nadra sana ni kwa kuwaza kuwa wewe hautakuwepo pale hatari hiyo itakapo tokea katika eneo hilo, na hivyo haitakuathiri.Kwanini uwaze kwamba wewe una bahati mbaya sana na vyote vibaya vitakapotokea vitakukuta wewe tu. Najua inawezekama kabisa lakini nafasi za kuwezekana huko ni ndogo sana. Mfano. Kwanini uwaze kuwa unapotembea msituni peke yako, mti unaweza kukuangukia. Au unapokuwa kwenye ndege au meli, ajali yaweza kutokea, au hata unapokuwa safarini kwa gari, jiulize mabasi mangapi yametoka kule unakotokea na kufika salama kule unakokwenda bila shida yoyote, wewe je huwezi kuwa mmoja wa waliokuwa salama?Kuna mambo mengi ya kuogopesha yanayotokea katika maisha yetu ya kila siku, na kama ukiogopa na kuhofu kila kitu na kutofuata ushauri unaotolewa hapa, basi kila siku utatembea na kuishi kwa hofu tu.Usiwaze sana juu ya matukio yasiyoweza kuepukikaYako matukio katika maisha ambayo kamwe hatuwezi kuyaepuka. Matukio haya yanakuja katika maisha yetu, yanapita na kusahaulika. Kitu cha muhimu ni kuishi maisha yako vema na kiusalama zaidi ili usijiweke katika hatari za kiafya na taratibu ukijiandaa kiuchumi na kijamii kwa uzee ulioko mbele yako.Pia usisahu kutenda mema na kuishi sawa sawa na imani yako inavyokutaka ili uweze kupata maisha mema tena baada ya haya ikiwa unaamini hivyo.Baada ya kufanya maamuzi haya usiweke sana mawazo yako kwenye mambo yanayohusiana na uzee, kustaafu au kifo. Acha mawazo au fikra hizo zielee zenyewe tu akilini mwako pasipo kuanza kuzichambua kwa kina.Amua nini utakifanya pale vile unavyo viwazia sana na kuvihofu vitakapotokeaKama unaona ni kazi ngumu kutowazia sana mawazo ya vile unavyovihofia, na unashindwa kujisahaulisha akilini mwako, basi pata muda wa kuvichambua kwa kina. Kwa asili, woga kututisha pale tunapojaribu kuwaza kuhusu mwisho au hatima ya baadhi ya mambo au matukio fulani, kwahivyo jaribu kufikiria nini utafanya pale ambapo hofu zako zitakapotokea. Kwakufanya hivi utaona kuwa pale vile unavyovihofia vinapotokea, basi maisha yataendelea kama kawaida, na mambo yatakuwa ya tofauti na vile yalivyo sasa.Kama unadhani kuna tahadhari ya kuchukua au maandalizi ya kufanya katika vile unavyovihofia basi fanya hivyo kwa umakini mkubwa na mengine yote umwachie Mungu. Baada ya kufanya hili utaona dhahiri kuwa hofu na woga ulionao haukutesi tena.Wacha kulilia maziwa yaliyokwisha kumwagikaNi kawaida kulia pale unapopoteza kile ulichokithamini au kukipenda, au pale kile ulichokiwekea jitihada kisipoleta matokeo uliyoyadhania. Hata hivyo, huna haja ya kujiumiza kichwa wala moyo, maana hutobadili chochote kwa yaliyokwisha kutokea. Usiweke mawazo sana katika vile ulivyopoteza au kuvipatia hasara. Ni kweli kwamba yamkini maisha yangekuwa bora zaidi kama kile au vile ulivyopoteza visingepotea, lakini pia hakuna mwenye uhakika na hili.
NAMNA YA KUISHUGHULIKIA NA KUISHINDA HOFU-4
Kilichotokea kimekwishatokea jitahidi sana kuboresha hali iliyopo sasa na ile iliyoko mbele yako siyo kusumbukia ile ambayo ingekuwako.
Acha kuilinganisha hofu sawa na jambo la muhimu
Unaweza kuwa unajidanganya kwamba kuwa na hofu ni sawa sawa na jambo lolote muhimu maishani. Ukweli ni kwamba hofu hupoteza nishati au nguvu ya mwili kwa kiasi kikubwa. Ingekuwa bora zaidi kuweka nguvu zako katika mipangilio ya wiki, mwezi na mwaka na siyo tu kuhofu.
Kamwe huwezi kuwa mtu mwenye tabia ya hofu na wakati huo huo ukawa mtendaji mzuri. Jaribu kuangalia wale wanaokuzunguka na utalihakikisha hili.
Wenye hofu pia ni ngumu kufanikiwa au kufikia malengo yao maishani. Kwahiyo wakati wowote utakapojikuta unahofu jikumbushe tu kwamba, kwa kuhofu haufanyi lolote la maana zaidi ya kupoteza nishati au nguvu yako ya mwili bure.
Amini kwamba tumepewa maisha haya ili tuyafurahie
Yathamini maisha yako kila siku, ukijua kwamba tumepwa ili tuyafurahie. Lazima kila siku kushukuru kwa mema mengi ambayo Mungu anatutendea, kwamaana kama ukiyaangalia mema yote haya huwezi kamwe kujiita mwenye bahati mbaya.
Kila siku uwe na mpangilio mzuri, ili kila kinachotokea katika siku yako kiwe kimepangiliwa sawa. Fanya mazoezi ya mwili kwa afya yako, soma vitabu mbalimbali vya maisha ili kuilisha akili yako, soma vitabu vya kiroho pia ili kuilisha roho yako. Pata nafasi yakuyatafakari na kuyatenda yale yote unayoyasoma.
Kula vyakula ambavyo vitausaidia mwili wako. Pata muda wa kushirikiana katika mambo ya kijamii kama vile mitoko ya maofisini, sehemu za ibada na katika familia.
Pata muda wa kuwa na mpenzi wako kama unaye na kama ni wa halali, pateni muda katika kuongea na kufurahia urafiki wenu.
Ongeza muda mzuri wa kuwa na watoto wako, zungumza nao mambo ya kwao na uwashirikishe mambo yakwako pia, furahi pamoja nao.
Katika maisha yako futa kwenye akili yako mtazamo wa kwamba maisha hujumuisha ni mjumuisho wa mikiki mikiki kama vile watu wa zimamoto walivyo. Kama unadhani kuwa maisha ni zima moto, basi dhumuni la kuishi kwako litakuwa kukaa macho kuangalia nini kitakacholeta moto ili ukizime.
Na kama unadhani kuwa maisha ni mlipuko wa matatizo basi dhumuni la kuishi kwako litakuwa kutega na kuangalia wapi hatari yaweza kutokea ili uizuie. Ondoka katika mitazamo hii michafu na uyatazame maisha kama zawadi ya kuifurahia.
Kama maisha ya raha yanakuponyoka sababu ya hofu zako, jiulize, ni lini hofu zako zitakwisha ili uanze kuyafurahia maisha?
Jibu ni kwamba, hofu hazitaisha kamwe kama hutaamua wewe mwenyewe kuzisimamisha. Utaishia kutumaini kuwa siku moja hofu itapotea kwa muujiza na utapata furaha.
Siku hiyo kamwe hutaiona kama hautafanya uamuzi wa makusudi wa kuondokana na hofu yako. Siku hiyo ni leo.
Kitu kingine cha muhimu ni kuondokana na zile hisia zako kuwa wewe hustahili kuyafurahia maisha.
Watu wengi waanahisia hizi. kama unahofu mara kwa mara basi waweza kuwa na hisia hizi pia. Hisia hizi zimejengwa kwenye msingi kwamba wewe hufai na huna thamani.
Kama unaamini hivi, pasipokujua utazifukuza nafasi zote za kukufanya uyafurahie maisha. Naomba nikwambie kwamba, wewe unafaa sana, unathamani kubwa, kwahiyo yafurahie maisha.
0 comments:
Post a Comment