Monday 8 September 2014

DAWA YA MARALIA SUGU




KWA WALE WENYE MALARIA SUGU NINATOA DAWA YANGU HII HAPA
Chukua majani manne ya Mpapai mabichi yaliyo komaa yenye shina na kikonyo(
ambayo yamekomaa) , chukua na vitunguu Swaumu punje zaidi za
ishirini na moja lakini zisipunguwe punje ishirini na moja.

1: Twanga majani yako ya mpapa kwenye kinu mpaka yakawa laini au
saga kwenye brenda
2: twanga punje zako za Vitunguu Swaumu

3; Chukua sufuria weka maji bilauri( glasi ) nne . weka
majani yako uliyoponda na uyachemshe mpaka utakapohisi
ukichuja unaweza kupata glass moja ya maji ambayo
yamechanganyika na majani yako ya Mpapai
4: baada ya kuchuja na kupata ule mchanganyiko wa glasi moja
bandika tena jikoni , ule mchanganyiko uliochuja na uweke
Vitunguu Swaumu vyako vilivyopondwa au kusagwa
5: Chemsha mpaka hadi pale utakapo ona ukichuja mchanganyiko
huo kwa mara ya pili utapata nusu glasi

Hivyo basi chuja huo mchanganyiko wa nusu glasi na kunywa
wote kwa mara moja. ( angalizo mchanganyiko huu ni mchungu
kuliko shubiri na una harufu kali sana yataka moyo kunywa.)

Ukiweza kunywa lazima kijasho Chembamba kitakutoka hata ukiwa na
Malaria kali inashuka na Homa inapungua ndani ya muda mfupi. unaweza kufanya hiyo dawa kwa muda wa siku 3 ukarudia njia hiyo hiyo kuengeneza dawa na kula.
ONYO: Mwenye mimba na Presha ya kushuka Tafadhali asitumie hii dawa.

0 comments:

Post a Comment