Wednesday 6 August 2014

UGONJWA WA ULAJI (EATING DISORDER)




Ugonjwa wa Ulaji (eating disorder)
Watu walioathiriwa na hali hii husumbuka sana kwa sababu ya tabia zao za ulaji. Wao pia husumbubuka kimawazo na kihisia kuhusu ulaji. Lishe isiyo na mpangilio humfanya mtu atamani kuwa mwenye mwili mdogo na vilevile huwa

na woga mwingi mno wa kunenepa. Ni muhimu mtu kupata ushauri na matibabu mapema vilivyo kwa sababu hali hii ina madhara mabaya ya kimwili na kimawazo.

 Aina za ulaji usio wa kawaida ni gani?

Aina mbili kali zaidi za hali hii ni

·         woga wa kula (anorexia nervosa) na

·         kujilazimu kutapika (bulimia nervosa).

 Woga wa kula (Anorexia)

Woga wa kula ni hali ya kuogopa sana kuwa mnene na kuwa na nia sana kuwa mwembamba.

Dalili za hali hii ni:

• Kupoteza angalau asili mia 15% ya uzito wa mwili kutokana na kukataa kula cha kutosha hata ikiwa mtu anahisi njaa.

• Kuwa na woga mwingi wa kunenepa na pia kupoteza uwezo wa kujimudu.

            • Kusumbuka kimawazo kuhusu mwili wa aliyeathiriwa akifikiri kuwa watu                                   wengine humwona ni kama amenenepa sana.

• Kufunya mazoezi ya mwili kupita kiasi kinachofaa.

• Ukosefu wa hedhi kwa wasichana.

Kujilazimu kutapika (Bulimia)

 Bulimia huwa ni hali ambayo mtu hula sana na mwishowe kujilazimu kutapika. Dalili zake ni:

            • Kula chakula kingi kilicho na calorie nyingi na wakati huu mtu anahisi hawezi kujiumudu na             hujidharau.

• Mtu hujilazimu kutapika ili kuondoa chakula kingi alichokula na kuzuia asinenepe. Badala ya au pamoja na kutapika, hutumia madawa au tembe za maji maji.


            • Mtu hujilazimu akule kiasi kichache cha chakula na hujichunga sana ili kujimudu asiongeze uzito inakuwa           muhimu sana kwa maisha yake.

Madhara ya anorexia na bulimia kwa mwili

Madhara ya kimwili ya woga wa kula na kujilazimu kutapika ni kali sana lakini hutibika ikiwa mtu hupata matibabu mapema. Ikiwa mtu hapati matibabu, woga wa kula na kujilazimu kutapika unaweza kuhatarisha maisha ya aliyeathiriwa.

Magonjwa mawili haya yakizidi yanaweza kusababisha:

• Huathiri figo.

• Huleta maambukizo kwenye mishipa ya mkojo na matumbo.

• Husababisha ukosefu wa maji mwilini, kinyesi kigumu na kuendesha.

• Huleta mshtuko, kifafa na shida ya misuli,

• Ukosefu wa hedhi au hedhi zinazokuja bila taratibu.

• Shida kwenye viungo vya mwili.

Madhara mengi ya anorexia yanahusiana na kudhoofika kwa mwili na:

• Shida ya kukosa hedhi wasichana.

• Kuhisi sana baridi, yabisi.

• Kuota kwa malaika zilizoinama mwilini.

• Kutofikiria kwa makini au kwa njia inayofaa.

 Kujilazimu kutapika husababisha:

• Kutokwa na madini ya meno kupitia kutapika.

• Mishipa ya mate iliyovimba.

• Kuwashwa kwa koromeo.

• Shida ndani ya  matumbo.

 Madhara ya kisaikologia na kihisia ni:

 • Upweke wa kujitakia kujitenga na kukataa kufanya urafiki na watu wengine.

• Huogopa atakataliwa na watu ikiwa watagundua ugonjwa wake.

• Hisia za kubadilikabadilika, mabadiliko ya nafsi, kutojiumudu hisia na huzuni.

 Nini husababisha ulaji usio wa kawaida?

 Sababu za kigenetiki

Kuna thibitisho kuwa wanawake walio na mama au dada aliye na woga wa kula huenda akaathiriwa na hali hii huonekana zaidi kuliko wale wanawake ambao hawana ndugu anayeathiriwa.

·         Sababu za kikemikali

Shida za usawa wa kemikali au homoni, haswa huanza na balehe katika miaka ya ujana, labda husika kusababisha hali hii ya lishe.

·         Sababu za kibinafsi

Kuna sababu nyingi za kibinafsi kuhusika na hali ya lishe isiyo na mpangilio kama:

• Mabadiliko maishani mwa mtu, kama miaka ya ujana inapoanza, kujifungua mtoto anapozaliwa au kifo cha mpendwa.

• Kutaka kufanya kila mambo kwa ukamilifu na kudhani kwamba kupendwa kwake kutategemea vile ambavyo ataweza kutimiza mambo makubwa.

• Kuogopa majukumu yanayotokana na kukomaa kiumri.

• Mawasiliano duni baina ya jamii au wazazi kuogopa kuwaachilia watoto kujitegemea zaidi wanapokomaa.

Matibabu gani yanapatikana?

 Matibabu ni pamoja na:

• Elimu ya lishe kusaidia kujifunza tena tabia bora za ulaji.

• Mbinu wa kisaikologia kusaidia watu wabadilishe mawazo yao, hisia na matendo yao kuhusu ulaji wa ghasia.

• Madawa ya kupunguza huzuni yanaweza kutumika kupunguza hisia ya huzuni na wasiwasi.

 Waone Wataalamu wa afya hawa ni pamoja na daktari maalum wa akili, wasaikologia, daktari maalum wa mwili, wataalamu wa ulaiji, wafanyakazi wa ustawi wa jamii, wataalamu wa shughuli na muuguzi.

0 comments:

Post a Comment