Thursday, 28 August 2014

UGONJWA WA SARATANI YA NGOZI (MELANOMA)-2



WIKI iliyopita tulieleza jinsi ugonjwa huu unavyomuingia mtu na matatizo yake.
 Tulieleza dalili lakini nyingine ni tezi za mwili za kwenye makwapa na kwenye nyonga huvimba, mgonjwa atatokwa na uvimbe kwenye ngozi, atapoteza uzito kwa kasi bila kujua sababu, atapata kikohozi kisichoisha, atapoteza fahamu au kupata kifafa,  ataumwa kichwa.
TIBA
Kuna tiba nyingi za kitabibu, zilizogawanyika katika makundi mbalimbali. Kuna zile za hospitali ambazo ni dawa na ni lazima zinunuliwe, lakini kuna tiba ambazo kwa ushauri wa daktari hata wewe unaweza kuziandaa bila kutumia gharama kubwa.
Moja ya tiba hizo ni kunywa maji ya moto ambayo yanatibu magonjwa mengi ikiwemo figo, kutoa sumu mwilini, kuyeyusha mafuta tumboni, kurahisisha mzunguko wa damu, kuondoa sumu kwenye ubongo na kusafisha haja ndogo.
Kunywa maji ya moto kila unapotaka kwenda kufanya kazi ya nguvu au mazoezi iwe kama kinga na inashauriwa kila siku mtu anywe glasi nane ili kutoa taka na kila kisichotakiwa kubaki mwilini, kupitia jasho au mkojo.
Ni vyema pia kunywa maji ya moto yenye ndimu au limao kabla ya kifungua kinywa ili kurahisisha mfumo wa mwili kwa siku nzima.
Maji yanarahisisha uyeyushaji wa chakula na mafuta mwilini, hivyo kutokana na umuhimu huo ni vyema kunywa maji  ya moto yatakayofanya kazi haraka na kwa ufanisi mkubwa bila kuchosha figo.
Faida nyingine ya kunywa maji ya moto kuwa ni kutoa sumu zilizopo kwenye mishipa ya fahamu na kuisaidia figo kufanya kazi kikamilifu, tofauti na maji baridi ambayo yanagandisha na kuilazimisha figo kuyeyusha kwanza na kisha kuchuja.
USHAURI
Unashauriwa kunywa maji moto kabla ya kufanya mazoezi kwani huko ni kujiandaa kwa ajili ya kuchuja jasho ambalo litatoa sumu. Maji ya moto yakifika tumboni yanaanza kufanya kazi moja kwa moja, kuliko yakiwa ya baridi yanaweza kusumbua kwa kuwa ni lazima yapate joto la mwili kwanza kabla ya kuanza kufanya kazi.
Unywaji wa maji ya moto kabla ya mazoezi ni mzuri kwani mtu anakuwa kama amekula chakula. Kunywa maji ya baridi bila kuweka kitu tumboni na kwenda kufanya mazoezi kunaweza kusababisha tumbo kuuma au maji kucheza wakati wa kukimbia kama unafanya mazoezi ya kukimbia.
Maji ni muhimu kwa mwili wako,  yakiwa ya moto ni bora zaidi, kwa kuwa yanatoa rangi ya njano ya mkojo na kuufanya uwe msafi na wenye rangi ang’avu. Ushauri ni kuwa ukiwa na alama yoyote mwilini inayokua kamuone daktari haraka.

Related Posts:

  • NJIA ZA KUONDOSHA HARUFU MBAYA MWILINI Kila mtu ana jasho au harufu ya kipekee mwilini na ndiyo maana kila mtu ana mahitaji ya kipekee katika kutunza mwili wake. Viungo vifuatavyo ndivyo hasa vinavyotoa harufu mbaya: Kinywa Kuna wakati kinywa hutoa harufu… Read More
  • MAMBO YA KUFANYA ILI USIPATE CHUNUSI Hakuna njia sahihi ya kujizuia ila unaweza kufanya yafuatayo;1.Osha taratibu sehemu unayodhani ina chunusi kwa maji safi na sabuni angalau mara mbili kila siku huku ukisugua taratibu ,usikwaruze kwa kucha au kitu choicho… Read More
  • JINSI YA KUONDOA MAKOVU YA CHUNUSI MARA nyingi chunusi zikitumbuliwa mbichi husababisha makovu yanayoleta weusi mbaya kwenye ngozi. Ukiachana na njia za gharama za kuondoa makovu hayo, kuna njia rahisi za kuondoa tatizo hilo:  1. Paka ‘bleach cream’ … Read More
  • FANYA MAMBO HAYA KUZUIA CHUNUSI NA MABAKA USONI Chunusi ni ugonjwa wa ngozi ambao hujit-okeza kama viuvimbe/vipele vidogo vidogo hasa sehemu za uso,kifuani na hata mgongoni.Vipele hivi hutokea wakati vishimo vya kupitisha jasho katika ngozi vinapozibwa kwa mafuta… Read More
  • NAMNA YA KUONDOA HARUFU MBAYA KWAPANI Hakikisha   unaoga kila siku ili kupunguza idadi ya bakteria kwapani kwani husababisha kuweka harufu mbaya kwenye mwili hasa majira ya joto kwa kuwa mara nyingi joto ndilo husababisha jasho na harufu kwapan… Read More

0 comments:

Post a Comment