Sunday 31 August 2014

TATIZO LA UTOKWAJI MAJIMAJI MACHAFU KATIKA VIA VYA UZAZI VYA MWANAMKE-3


WIKI iliyopita tulijadili vyanzo vya tatizo hili linalowakabili wanawake wengi ambavyo ni maambukizo/mashambulio katika ya fangusi aina ya candida au bakteria aina ya chlamidia kwenye njia ya uzazi ya mwanamke, ulaji mbovu, njia za kisasa za uzazi wa mpango (hasa vidonge) bila kujali ushauri wa mtaalamu na bila kujali usafi.
Nyingine ni kutokuwiana kwa homoni za mwanamke, uchafu wa mavazi na uchafu wa mwili hasa kwa mwanamke ambaye hajui jinsi ya kujisafisha katika via vyake vya uzazi ili kuondoa seli zilizokufa (dead cells), kushiriki tendo la ndoa bila kinga, kushiriki tendo la ngono kinyume na maumbile na baadae kuhamishia kwenye via nya uzazi.
Leo nitaendelea kwa kujadili madhara ya tatizo hili:
Madhara ya Tatizo la kutokwa na uchafu katika via vya uzazi (Vaginal discharge):-
Ugumba: Hii hutokea pale mashambulizi/maambukizi yanapofika kwenye mirija na kuleta uvimbe ambao huziba au kusababisha kutengenezwa kwa maji machafu mazito ambayo nayo huziba mirija na huua mimba kila inapotungwa.
Mwanamke kunuka/kutoa harufu mbaya wakati wote hata kama ameoga na kuvaa vizuri:  Huwa hali mbaya zaidi wakati wa kushiriki tendo la ndoa. Jambo hili husababisha mwanamke kuwa na aibu na kujitenga, kutengwa, kujiona hana thamani na unyonge.
Kupata maambukizi katika njia ya mkojo yaani U.T.I: Hii ni kwa sababu njia ya uzazi na ile ya mkojo zimekaribiana sana sehemu zinapoanzia kwenye via vya uzazi vya mwanamke. Tatizo hili la uchafu ukeni lisipotibiwa kwa uhahika na kuisha huchangia maambukizi katika njia ya mkojo kuwa sugu na yanayojirudiarudia kwa mwanamke.
Maumivu wakati wa kutoa haja ndogo, kwenda haja ndogo mara kwa mara, maumivu ya mgongo na kiuno na kutoa haja ndogo yenye rangi ya njano au kijivu ni baadhi ya dalili za U.T.I
Mimba kutunga nje ya mfuko wa uzazi/ uterus
Mashambulizi haya kwenye mirija hudhoofisha viumbe wanaoitwa cilia ambao wanamaumbile kama vijinyoya ambao wapo kwenye kuta za mirija ya uzazi wakiwa na kazi kubwa ya kusukuma yai la uzazi kupita bila tabu kuelekea kwenye mji wa mimba na hivyo yai halitofika kwenye mji wa mimba na mimba itatunga.
Kwenye mrija wa uzazi na kukua hapo, kitu ambacho humlazimu mwanamke kufanyiwa upasuaji kuondoa mrija ulioathirika na hivyo kubakiwa na mrija mmoja.

0 comments:

Post a Comment