Mwanamke au msichana aliyekuwa akipata siku zake kama kawaida hapo awali na baadaye ghafla kakosa siku zake kwa kipindi cha miezi 6 mfululizo, basi huchukuliwa kwamba ana ugonjwa au tatizo linalosabisha kero hiyo nyuma yake.
Inafahamika kwamba mwanamke au msichana yeyote aliyepevuka kikamilifu, hupata siku zake za kutokwa na damu isiyoganda katika njia ya uzazi mara moja kwa mwezi. Dalili hiyo inaashiria ukomavu katika viungo vya uzazi.
Hata hivyo, kuna wakati mwanamke au msichana anapatwa na tatizo la kutokuona siku zake, hii ni dalili ya kuwepo kwa tatizo katika mfumo wake wa uzazi.
Ifahamike kwamba kukosa siku kwa mwanamke kumegawanyika katika makundi mawili. Kundi la kwanza ni wale wanaokosa siku zao kwa kawaida bila ugonjwa na kundi la pili ni wale wanakosa siku zao kwa sababu ya ugonjwa.
Binti au msichana huchukuliwa amekosa siku zake bila ya ugonjwa pale anapofikisha umri wa miaka 16 bila kupevuka huku akioneka kukomaa kwa viungo vyake vya uzazi.
Mwanamke au msichana aliyekuwa akipata siku zake kama kawaida hapo awali na baadaye ghafla kakosa siku zake kwa kipindi cha miezi 6 mfululizo, basi huchukuliwa kwamba ana ugonjwa au tatizo linalosabisha kero hiyo nyuma yake.
Mambo yanayosabisha mwanamke au msichana kukosa siku zake bila kuwepo kwa ugonjwa (hali ya kawaida na inayokubalika kisayansi) ni pamoja na umri chini ya umri wa kupevuka au kubalehe, kuwa mjamzito, kipindi cha kunyonyesha mtoto na kumalizika kwa umri wa kuweza kupata mimba ( menopause).
Kuwepo kwa kundi hili ni kawaida na kuna sababu yake, hivyo mwanamke hatakiwi kuhofu chochote kwani hayo ni mabadiliko chanya katika mwili wake. Magonjwa au matatizo yanayosababisha mwanamke aliyepevuka au kubalehe kikamilifu, lakini hapati siku zake kama kawaida au ghafla ni mengi, lakini kwa uchache ni pamoja na tatizo katika mayai au vitunga mayai yake. Hili ni asilimia 40, tatizo katika ubongo wake asilimia 19, tatizo katika mfuko wa uzazi ni asilimia 5 huku magonjwa megineyo yakichangia kwa asilimia moja.
Ni vyema kwa mwanamke au binti anayepatwa na tatizo hili kumwona daktari ili uchungizi ufanyike na matibabu yatolewe.
Sunday, 24 August 2014
TATIZO LA MWANAMKE KUKOSA SIKU ZAKE ZA HEDHI
Related Posts:
KUPUNGUA NGUVU ZA KIUME NA MATIBABU YAKE PART-2 MATIBABU UPASUAJI NA BAADHI YA MATIBABU YA DAWAMatatizo yanayosababishwa na matibabu ya dawa na upasuaji, ni kwamba, neva na mishipa ya damu inayohusika na usimamaji wa uume zinaweza kudhuriwa na aina ya matibabu ya… Read More
JE WAJUWA FAIDA ZIPATIKANAZO KWA KIUMBE MDUDU MENDE? Mjue Mende 1.Ni mdudu anayeweza kuishi zaidi ya mwezi bila ya kula chakula chochote. Wana uwezo wa kuishi katika mazingira magumu. Aina moja kwa jina Eublaberus posticus wanaweza kuishi mwaka mmoja kwa kunywa maji pekee. … Read More
Oncologists Don’t Like Baking Soda Cancer Treatment Because It’s Too Effective and Too CheapOften the cancer patients agree to chemotherapy without knowing of its negative side effects. The chemo is very much toxic but still is the lead first treatment for cancer. The only reason that the chemo treatment is still pr… Read More
KUOTA NDEVU AU NYWELE KWA MWANAMKE, KWENYE SEHEMU AMBAZO SIO ZA KAWAIDA KWA JINSIA YA KIKE, HUJULIKANA ZAIDI KWA MAJINA MAWILI [1] HIRSUTISM AND [2] HYPERTRICHOSIS HIRSUTISM is defined as the excessive growth of thick dark hair in locations where hair growth in women usually is minimal or absent or is the growth of … Read More
TOFAUTI KATI YA DAWA ZA ASILI NA DAWA ZA KISASA TOFAUTI KATI YA DAWA ZA ASILI NA KISASA Kulingana na Wikipedia kemikali ni kitu chochote chenye muundo kamili kikemia na kinasifa inayokitambulisha. Hata vyanzo vingine vya taarifa huunga mkono hili. Kumbe vitu vingi sa… Read More
0 comments:
Post a Comment