Wednesday 20 August 2014

MUHIMU KUJUWA WAKATI UNA MIMBA

Wanawake wengi hujua wameshika mimba aghalabu wiki 3 baada kushika mimba. Mwili wenyewe utakuonyesha/utakutabiria kama:

Hedhi yako itakoma/itakuwa nyepesi
Utasikia uchefuchefu/utatapika (ugonjwa wa asubuhi – ‘morning sickness’ – na inaweza kutokea wakati wowote wa siku pia).
Matiti yako yataanza kuwasha, kufura au yataanza kuwa makubwa.


Chuchu (ncha ya titi) na sehemu zilizokaribiana zitaanza kuwa nyeusi na zizizoweza kuvumilia.
Itakubidi kwenda haja ndogo mara kwa mara.
Utasikia uchovu
Kusokotwa na tumbo

Kama umeona baadhi ya dalili hizo, unaweza kuwa na mimba. Pata jaribio/uchunguzi kipimo cha mimba ili kupata yakini! Unaweza pimwa bure katika kliniki iliyokaribu nawe au ununue kifaa vya kujipmia nyumbani kutoka duka la dawa. Daktari wako anaweza kukupima pia au atakuelekeza kwa mtaalamu kama hauna.

Umuhimu wa kunyonyeasha
Pindi tu baada ya kujifungua,kumung’unya wa kujirudia rudia wa mtoto hutoa oksitoksini kutoka kwa teziubongo wa mama.Homoni hii haiashirii tu matiti kumtolea mtoto maziwa (hii inajulikana kama tendohiari la utoaji wa maziwa ama “let-down), lakini wakati huo huo husababisha mkunyato katika mji wa mimba. Mkunyato unaotokea huzuia utokaji wa damiu uliozidi na husaidia mji wa mimba kurudia ukubwa wake wa kawaida.

Ikiwa mama atanyonyesha mtoto bila ya kutumia maziwa mbadala ama vyakula vingine kipindi chake cha kuingia mwezini kitacheleweshwa.Tofauti na akina mama ambao huwalisha watoto wao kwa kutumia chupa, ambao kwa 

kawaida huingia mwezini baada ya majuma sita hadi manane, akina mama wanaonyonyesha wanaweza kukaa bila ya kuingia mwezini kwa kipindi cha miezi kadhaa. Hali hii ina manufaa muhimu ya kuhifadhi chuma katika mwili wa mama na mara kwa mara hutoa nafasi asili baina ya uja uzito.

Kunyonyesha ni kuzuri kwa akina mama wapya na vile vile kwa watoto wao. Hakuna chupa za kufisha vijidudu,hakuna haja y a kununua maziwa ya mtoto,kupima na kuyachanganya.Inaweza kuwa rahisi kwa mama anayenyonyesha kupoteza uzani wa uja uzito vile vile kwani kunyonyesha kunatumia vizio vya joto. Kunyonyesha pia husisimua mji wa mimba kukunyata na kurudia ukubwa wake halisi. 

Mwanamke anayenyonyesha huzalimishwa kupumzika ambako anahitaji sana.Ni lazima akae chini na kupumzika kila baada ya masaa kadhaa ili anyonyeshe.Kunyonyesha wakati wa usiku ni rahisi pia. Ikiwa amelala chini, mama anaweza kulala huku bado ananyonyesha.

Kunyonyesha pia ni njia asili ya kuzuia mimba-hata ingawaje sio ya kutegemewa.Kunyonyesha mara kwa mara huzuia uzalishaji wa mayai na hivyo kupunguza uwezekano wa mama anayenyonyesha kuingia mwezini, kutoa mayai ama kupata uja uzito. Hakuna hakikisho hata hivyo. Mama ambao 

hawataki watoto wengi wanapaswa kutumia mbinu za kuzuia mimba hata ikiwa bado wananyonyesha. Kujidunga homoni na vipandikizi wakati wa kunyonyesha ni salama kama zilivyo mbinu za kinga za kuthibiti uzazi.Maelezo kwenye vidonge vya kuthibiti uzazi vinasema ya kwamba ikiwezekana mbinu nyingine ya kuzuia uja uzito inafaa kutumiwa hadi mtoto achishwe ziwa. 

Kunyonyesha pia hupunguza gharama.Hata ingawaje mwanamke anyenyonyesha huwa na hamu kubwa ya chakula na hula kalori zaidi, chakula chake cha ziada sio ghali ukilinganisha na kununua maziwa ya mtoto. Kunyonyesha hupunguza matumizi ya pesa ilhali hutoa chakula ambacho ni bora zaidi kwa mtoto.

Manufaa ya Kipindi Kirefu ya Kunyonyesha
Sasa imeanza kuwa bayana ya kwamba kunyonyesha humpatia mama zaidi ya manufaa ya kipindi kifupi katika kipindi cha hapo mwanzoni baada ya kujifungua.
Utafiti umeonyesha manufaa mengine ya kiafya ambayo mama anaweza kuyafurahia kwa kunyonyesha.Manufaa haya yanajumuisha afya bora, kupungua kwa hatari ya baadhi ya saratani na manufaa ya saikolojia.


Kitu kingine muhimu kinachotumiwa katika kuzalisha maziwa ni kalshiamu.Utafiiti wa hivi sasa unaonyesha ya kwamba baada ya kuachisha watoto ziwa,uzito wa mfupa wa mama anayenyonyesha hurudia ule wa kabla ya uja uzito ama huwa hata wa juu zaidi. Mwishowe,kunyonyesha kunaweza kusababisha mifupa yenye nguvu zaidi na hupunguza hatari ya ugonjwa wa mifupa (osteoporosis) “mifupa iliyokonda.”Utafiti wa hivi sasa umethibitisha ya kwamba wanawake ambao hawakunyonyesha wako katika hatari kubwa ya kuvunjika kwa nyonga baada ya kukoma hedhi.


Wanawake ambao hawanyonyeshi wameonekana katika utafiti mwingi kuwa katika hatari kubwa ya kupata saratani za uzazi. Saratani ya ovari na ile ya mji wa mimba zimepatikana kuwa za kawaida katika wanawake ambao hawakunyonyesha.
Hitimisho: Kunyonyesha hupunguza hatari ya matatu kati ya magonjwa mabaya sana katika wanawake-saratani za wanawake, ugonjwa wa moyo na ugonjwa wa mifupa-bila ya tishio lolote la kiafya.

Masuala ya Kisaikolojia Kwa Akina Mama Wanaonyonyesha
Kunyonyesha ni zaidi ya kutoa tu lishe na kumlinda mtoto dhidi ya magonjwa kupitia kwa maziwa ya mama.Kunyonyesha hutoa njia ya kipekee ya kuingiliana baina ya mama na mtoto, kukaribiana kwa papo hapo kwa ngozi –kwa-ngozi na malezi ambayo akina mama wanaotumia chupa wanapaswa kufanya jitihada ili wayarudufu.
Prolactin ambayo ni homoni inayotengeneza maziwa,huonekana kutoa utulivu maalumu kwa akina mama na kuwasaidia kupambana na mfadhaiko kwa njia iliyo bora.

0 comments:

Post a Comment