Saturday 26 July 2014

SABABU ZA MAUMIVU WAKATI WA TENDO LA NDOA

SABABU ZA MAUMIVU WAKATI WA TENDO LA NDOA

·         Upungufu wa lubrication(maji ya ulainishi) ndani ya uke unaweza kusababisha maumivu. Kwa kawaida, uke wa mwanamke unazalisha majimaji kulainisha ili uume uingie bila kusababisha maumivu. Zinaposhindikana njia za kitabibu na ushauri mwanamke anashauriwa kupaka lubricants zilizopendekezwa kiafya. Maji maji ya ukeni (Lubricants) kwa  kawaida huzalishwa katika uke wa mwanamke kila siku  lakini uzalishaji huongezeka kwa kiasi kikubwa wakati mwanamke anapopata hisia za kufanya ngono au anapotarajia kujamiiana.  Ukavu ukeni ni hali ambayo majimaji yanakua hayatoshi, na wakati mwingine mafuta bandia (kama tulivyoona hapo juu) hutumika kwa kulainisha uke wake. Bila lubrication ya kutosha, kujamiiana kunaweza kuleta uchungu kwa mwanamke. Uke una tezi inaitwa Bartholini huzalisha pia majimaji ya ukeni. Mbali na baadhi ya matatizo ya kiafya yanayoweza kusababisha mwanamke kuto zalisha maji ya kutosha ni pamoja na kutokua tayari kwa tendo la ndoa na sababu za kisaikolojia pia zinaweza kua chanzo cha tatizo la kuto zalisha maji ya kutosha

·         Maumivu ya kina ndani ya uke inaweza kuwa ishara ya matatizo kama vile ovarian cyst, yaani uvimbe mdogomdogo katika mfuko wa mayai(ovary) 

·          Maambukizi ya mfuko wa uzazi au mirija ya kupitishia mayai, endometriosisi 

·         Wakati mwingine maumivu husababishwa na vaginismus(mkazo wa misuli ya uke)- hali ambayo misuli ya uke inakaza.
  • Wakati mwingine, inaweza kuwa  sababu za kisaikolojia . Maumivu ya awali yanaweza kusababisha hofu ya maumivu ya mara kwa mara na hali hiyo ikawa vigumu kuondoka kichwani.

UTATA

*NI DEBATE KUHUSU UREFU WA UUME KUWEZA KUSABABISHA MAUMIVU KWA MWANAMKE WAKATI WA TENDO LA NDOA, NA KUHUSU UNENE WA UUME WATAALAMU WANASEMA HAKUNA UUME WENYE UNENE WA KUMUUMIZA MWANAMKE

 
*WENGINE WANASEMA "THERE IS NO OVERSIZE PENIS AND THERE IS NO UNDERSIZE VAGINA

0 comments:

Post a Comment