Friday, 18 July 2014

MADHARA YA KUPIGA PUNYETO (MASTRUBATION) JE KUNA FAIDA AU HASARA YA KUPIGA PUNYETO?



Ili tuweze kuongezeka inatubidi tuzaliane kama viumbe wengine, na hatuwezi tu kuzaliana bila ya kujamiiana, na hatuwezi kujamiiana bila ya kuwa na hisia zitakazotupelekea kufanya kitu kama hicho. Katika maumbile ya mwanadamu hupata hisia hizo anapofikia umri wa kubalehe na ndio hapo huanza kuona mambo mageni kiasi cha kumfanya ajione tofauti na wengine hata kama nao walishapitia hatua kama hiyo.

Katika hatua hii ndio mbegu za uzazi (Sperms) zinaanza kutengenezwa na kukomazwa, hali inayomfanya mtu kuwa na hisia za kutaka kuwa na mwenzake (Girlfriend) ili atimize haja zake. Kwa asilimia kubwa ya vijana wa sasa hujichua ili kuondoa hisia hizi pale wanapokosa wapenzi, na imeathiri vijana wengi sasa bila ya wao kujua.

Kitendo hiki cha kujichua kinachojulikana kama "Kupiga punyeto” in English "Masturbation” huleta madhara ya muda mrefu ambayo ni vigumu mtu kugundua. Hebu tuangalie baadhi ya madhara ya kitendo hiki:

  1. Upungufu wa nguvu za kiume.

Hili ni tatizo linalowakabili watu wengi sana na hili pia hutokana na watu hao kuwa na mchezo wa kupiga punyeto hapo awali au hata muda huu. Na hivyo hukosa nguvu za kiume na kuwafanya wakose heshima ndani ya ndoa.



  1. Kutofurahia tendo la ndoa.
Kumbuka kuwa unapopiga punyeto unatumia mkono ambao unapewa amri na ubongo ya kufanya kile ambacho nafsi itaridhika, hivyo lazima utatumia nguvu nyingi za mkono kwa kadiri ya matamanio ya nafsi yako yanavyohitaji hali itakayopelekea kutofurahia tendo la ndoa kwani hapo utakuwa hutumii mkono bali ni kiungo kingine ambacho hukiamrishi wewe kufanya vile utakavyo.





  1. Madhara ya ndani ya sehemu za siri.

Kitendo cha kupiga punyeto hutumia sabuni ambayo ina kemikali, hivyo kitendo cha kusugua sugua kwa kutumia sabuni huifanya ipenye ndani au kwenye vitundu vidogo vya ndani ya ngozi na kuweza kukusababishia madhara mbalimbali. Ni wachache sana ambao hawatumii sabuni lakini bado haina faida kwani huweza kupata athari kwa sababu zingine.




  1. Kupunguza uwezo wa kufikiri.

Wafanyao kitendo hiki hutumia nguvu nyingi za akili kuwaza kuwa yuko na fulani kumbe sio kweli, yeye yuko peke yake bafuni na sabuni yake tu. Hali hii huumiza sana akili kwani ni kitendo cha kila siku na kwa vijana wengine hufanya mara mbili au zaidi kwa siku kutegemea na hisia zake, hivyo akili huchona na uwezo wa kifikra unapungua kwa kiasi kikubwa sana.




  1. Kukosa nguvu katika magoti.

Kufanya sana kitendo hiki hupunguza mafuta yalio katika viungio vya magoti na kufanya magoti kukosa afya na nguvu.



Unaweza kujiuliza sasa kama ni kijana ufanyeje ili uepukane na hili? Na je? Utadhibiti vipi hisia zako? Ni rahisi sana fanya haya yafuatayo:

  1. Jiweke busy na masomo yako kwani ndiyo wakati wake huu na sio kufuata au kufikiria juu ya matamanio. Kumbka kuw amatamanio hayawezi kuja tu ikiwa utayapuuza na kujali mambo mengine ya muhimu kulingana na wakati wako.


  1. Fanya sana mazoezi ya kuuchosha mwili kama vile kukimbia, kuruka kamba, kucheza mpira, basketball, karate na mengineyo ambayo yatakuchosha na kukutoa jasho kila siku kwa mpangilo maalumu.


  1. Epuka kukaa peke yako bila kazi yoyote kwani kutakufanya ufikirie matamanio kwani ndio jambo linalotawala fikra za vijana.


  1. Acha kula hovyohovyo bila sababu maalum na hasa epuka sana kula vyakula vya mafuta mafuta kwani hivi hutengeneza mbegu za kiume kwa kasi kubwa sana.


  1. Tumia muda wako wa free kupumzisha akili yako kwa kulala.


  1. Jitahidi kutokukaa bafuni kwa muda mrefu bil aumuhimu wowote na epuk akujisugua au kujishika sana sehemu za siri wakati wa kuoga.

Jitahidi ubadilike na fahamu kwamba kufanya hivyo kukiendelea sana kwako itakuwa tena sio mazoea bali ni tabia na siku zote mazoea hujenga tabia, utajikuta huachi hata kama utampata wa kukutimizia haja zako (Mke) kwani hutoridhika naye kwa athari ya mkono wako.


Fahamu pia kuwa kutafuta msichana (Girlfriend) sio njia sahihi kwani ndiyo sababu ya kuharibu jamii kwa kuwaharibia maisha yao kwa kuwapa ujauzito wakiwa mashuleni, kusambaza maradhi na kuleta watoto wa mitaani (Street Children).

Njia sahihi ni kama tulizozitaja hapo juu. Soma kawa bidii, Jali muda wako na kuwa makini sana. Utapata kazi nzuri,utampata akupendaye mkaridhiana, mkaoana na kujenga familia iliyo bora kabisa ambayo hata mungu ataipenda na kuibariki.

0 comments:

Post a Comment