Friday, 11 July 2014

LISHE KWA MGONJWA WA KISUKARI





LEO tunaendelea tena kuangalia suala la lishe kwa wagonjwa na hapa tunamuangalia mgonjwa wa kisukari. Kama tulivyokwisha ona katika makala nyingine zilizopita, mgonjwa yeyote wa magonjwa hatari kama presha, moyo, saratani, kisukari n.k, ni lazima ajue vyakula anavyopaswa kula au kutokula.
Elimu ya lishe ni muhimu sana, kwani madhara ya ugonjwa huonekana haraka na hata kusababisha kifo upesi, iwapo mtu ataendelea kula bila kujijua vyakula vilevile vilivyosababisha tatizo la kiafya alilonalo.
Kwa ujumla, mgonjwa wa kisukari (Diabetic), hana mipaka mingi ya vyakula, anaweza kuendelea kula vyakula vingi kama kawaida iwapo atajua jinsi ya kula, kiasi gani na kwa wakati gani. Hata hivyo, kama ulaji wake ulikuwa hauzingatii ulaji sahihi, baada ya kuugua hana hiyari bali kufuata kanuni za ulaji sahihi.
Kanuni kuu ya ulaji anayopaswa kuzingatia mgonjwa wa kisukari ni kula kiasi bila kushiba sana, kula kwa muda uleule kila siku, na kula mchanganyiko wa matunda, mboga na nafaka zisizokobolewa. Hii ina maana kwamba mgonjwa anatakiwa asisikie njaa wala shibe muda wote wa siku.

KITU GANI UNAKULA?
Bila kujali kama una kisukari au la, afya bora iko mikononi mwako kwa kuwa na hiyari ya kuchagua unachokula. Lakini unapokuwa tayari mgonjwa, unakuwa huna hiyari tena ya kuacha kuzingatia ulaji sahihi, vinginevyo unakiita kifo haraka. Kimsingi, mgonjwa wa kisukari azingatie zaidi ulaji wa vyakula vitokanavyo na mimea, aache kula vyakula vya kusindika, vyenye sukari na mafuta mengi.
WAKATI GANI WA KULA?
Suala la kujali muda wa kula kwa mgonjwa wa kisukari ni la lazima, kwa sababu atatakiwa wakati wote kudumisha kiwango cha sukari mwilini mwake kwa kula kwa wakati uleule ili kuepuka kusikia njaa ambayo husababisha sukari kushuka kwa kasi.

KIASI GANI UNAKULA?
Vilevile suala la kula kiasi kwa mgonjwa wa kisukari si la hiyari tena, bali ni la lazima. Hata mtu akila vyakula bora vyenye virutubisho vya hali ya juu kiasi gani, kama akivila kupita kiasi huweza kusababisha unene ambao ni sababu moja wapo ya ugonjwa wa kisukari, hivyo ni muhimu kuzingatia kiasi.
Mgonjwa wa kisukari hahitaji kuwa na chakula maalumu, bali anatakiwa kutilia maanani ulaji wa mboga, matunda na nafaka zisizokobolewa. Lishe ya mgonjwa wa kisukari ni ya kawaida tu yenye vyakula vyenye virutubisho vingi na mafuta kidogo na kiasi kidogo cha wanga.

ZINGATIA
Mgonjwa wa kisukari anashauriwa kula matunda, lakini anakatazwa kunywa juisi za matunda. Halikadhalika, matunda kama ‘Apples’, ‘Peas’ na mengine ya jamii hiyo, ni bora yaliwe pamoja na maganda yake.
Miongoni mwa matunda bora kabisa kwa mgonjwa wa kisukari ni zababi mbivu, hizi zikiliwa kila siku mara tatu kwa siku, huweza kuwa tiba kabisa ya kisukari.
Halikadhalika majani ya embe nayo ni dawa ya kisukari. Loweka majani mabichi ya mwembe, kiasi cha kiganja kimoja (gramu 15), kwenye nusu lita ya maji usiku kucha, kisha asubuhi yakamue upate maji yake, kunywa kila siku asubuhi na unaweza kukidhibiti kisukari, hasa kile kinachopanda nyakati za asubuhi.

Related Posts:

  • FOODS THAT MAKE MEN BETTER IN THE BED Want to spice things up in the bedroom? Try any one of these 7 foods to fire up the libido Having a healthy sex life plays an important part of our wellbeing. Low libido in men is much more common than we are… Read More
  • NJIA SABA MUHIMU ZA KUZUIA U.T.I KWA WATOTO CHINI YA MIAKA MITANO Ugonjwa wa mfumo wa mkojo kitaalamu urinary tract infection(UTI) umekuwa ukisumbua watu wengi. Vimelea vinavyosababisha ugonjwa katika mfumo wa mkojo hukua na kusambaa endapo kinga ya mwili inakuwa ndogo hivyo makund… Read More
  • SABABU 18 ZA KUPUNGUZA UZITO sababu 18 zinazokulazimu upunguze uzito wako na uogope unene na zote ni hizi zifuatazo: 1. Unene unaongeza kiwango cha mafuta mwilini, ambayo huongeza uwezekano wa kupata kansa. 2. Unene unaongeza mafuta mwilini, … Read More
  • KANSA YA MATATITI: VITAMIN D NDIYO KINGA KUBWA Vitamin D, ambayo kwa kiasi kikubwa hupatikana kwa ngozi kupata mwanga wa jua, ina faida nyingi muhimu za kiafya mwilini na utafiti wa hivi karibuni umebaini kuwa vitamin hiyo ndiyo msingi mkubwa wa kuzuia magonjwa mbalimba… Read More
  • FOOD TO BOOST SPERM COUNT Low sperm count affects approximately one in 25 men. Lifestyle factors such as stress, obesity, and poor nutrition can impact sperm health. If you and your partner are planning for a baby, a nutritional overhaul is a … Read More

0 comments:

Post a Comment