Thursday, 17 July 2014

Je Saratani ya Tezi-Kibofu ni 'maradhi ya Zinaa?'



Celi za Saratani ya Tezi Kibofu
Huenda Saratani ya Tezi-Kibofu ni ugonjwa wa Zinaa unaosababishwa na ugonjwa wa zinaa ambao dalili zake sio wazi sana.
Hii ni kwa mujibu wa wanasanyansi nchini Marekani. Wanasema kwamba Saratani hiyo husababishwa na maradhi fulani ambayo huenezwa wakati wa kitendo cha ngono.

Ingawa baadhi ya Saratani husababishwa na maradhi fulani fulani, kitengo cha utafiti wa Saratani nchini Uingereza kinasema kuwa ni mapema mno kuongeza Saratani ya tezi kibofu kwa Saratani hizo.Lakini wataalamu wanasema kuwa ushahidi bado haupo kama kweli Saratani hiyo ni moja ya magonjwa ya zinaa na inasababishwa na magonjwa ya zinaa.

Wanasayansi waliofanya utafiti huo walichunguza celi za tezi kifobu cha binadamu katika maabara.
Waligundua kuwa maradhi ya zinaa yaitwayo, 'Trichomoniasis' yalichochea ongezeko la Saratani hiyo.
Hata hivyo mfumo wa maisha pia unachangia ongezezeko la visa vya magonjwa ya Saratani.
Ugonjwa wa 'Trichomoniasis' unaaminika kuwaathiri watu milioni 275 duniani na moja ya maradhi maarufu ya Zinaa ambayo hayasababishwi na Virusi
'Dalili za Trichomoniasis'
Seli zilizoambukizwa Saratani
Kawaida, mtu hatapata dalili za ugonjwa huo na inawezekana asijue kama anaugua ugonjwa huo.
Wanaume huhisi kujikuna sana ndani ya uume wao , kupata hisia za kuchomeka wakati wanapokwenda haja ndogo au kuvuja majimaji meupe kutoka kwa uume wao.
Wanawake pia wana hisia tu sawa na hizo katika sehemu zao za isiri pamoja na kuwa na harufu mbaya.
Utafiti huu wa hivi karibuni sio wa kwanza kuhusisha ugonjwa wa 'Trichomoniasis' na Saratani ya Tezi kibofu.
Utafiti uliofanywa mwaka 2009 ulipata kuwa robo ya wanaume walio na Saratani hio walikuwa na dalili za ugonjwa wa Trichomoniasis na wanaume hawa pia walikuwa na uvimbe ambao ulikuwa umekomaa mno.
'Hoja ya Uchunguzi zaidi'
Uchunguzi huo pia unaonyesha njia ambazo ugonjwa huo wa zinaa unawaweka wanaume katika hatari ya kupata Saratani ya tezi kibofu.
Profesa Patricia Johnson na watafiti wenzake, waligundua kuwa viini vinavyosababisha ugonjwa wa 'Trichomonas vaginalis' - huvuja proteni ambayo husababisha Saratani ya Tezi Kibofu kuzuka.
Mtaalamu wa afya, Nicola Smith,anasema uchunguzi huu unaonyesha tu njia ambazo ugonjwa wa zinaa wa Trichomonas vaginalis unazidisha uwezo wa mtu kuugua Saratani ya Tezi Kibofu na kuchochea seli kukuwa kwa kasi.
"Lakini uchunguzi huu ulifanywa tu katika maabara na matokeo ya awali kwa wagonjwa yalikosa kuonyesha uhusiano kati ya ugonjwa huo na Saratani ya Tezi Kibofu,'' alisema Bi Nicola

Kwa kauli hii wanasema kuwa uchunguzi zaidi unahitajika ili kuabini hasa kinacho sababisha Saratani ya Tezi kibofu kwani ugonjwa wa Trichomoniasis husababisha tu mazinigira kwa ugonjwa huo kukomaa ila sio chanzo cha ugonjwa wenyewe.

Related Posts:

  • 10 Unexpected Side Effects Of Peppermint Tea Peppermint—the word conjures up images of bubble gums, right? But, peppermint is also used to provide flavor to various other products. Some of them are toothpaste and tea. It is an active ingredient in various medicinal a… Read More
  • 10 Surprising Side Effects Of Watermelon Come summers and we can find watermelons everywhere! The perfect summer fruit, watermelons with high water content, make for great thirst quenchers. Watermelons are not just tasty and refreshing but are healthy too! They c… Read More
  • 5 Side Effects Of Garlic You Should Be Aware Of Allium sativum, commonly known as garlic is a member of the onion genus species, Allium. It falls into the broad category of onions, shallots, leak and chive and is usually of a pungent nature in smell and taste. Originati… Read More
  • 15 Harmful Side Effects Of Aspirin You Must Be Aware Of We have all heard of ‘Aspirin’! It is one of the most commonly used drugs. But, most of us are unaware of the purpose it serves and the side effects of its overdose.Aspirin, also known as acetylsalicylic acid, is a salicyla… Read More
  • 10 Harmful Side Effects Of Ginseng Tea Ginseng is an ancient herb, which offers remedies for many diseases. It is also known as the king of all herbs. It protects our body and also helps our body fight innumerable diseases. Ginseng is an adaptogen, which is cap… Read More

0 comments:

Post a Comment