Wataalamu wa afya wanasema fenesi huongeza ufanisi wa mfumo wa kinga mwilini na kusaidia kuongeza kinga dhidi ya kifua, mafua na kikohozi. Hii ni kwa sababu ya kuwa na vitamini za aina mbalimbali.
Fenesi ni miongoni mwa matunda ya msimu yenye umbo la kipekee na ladha tamu ya aina yake. Tunda hili linatajwa kuwa na faida lukuki kiafya kwa mwili wa mwanadamu. Kula gramu 100 tu ya fenesi huweza kuupatia mwili nguvu ya kalori 95.
Tunda hili lina nyama laini iliyojaa sukari aina ya fructose na sacrose inayoweza kuupatia mwili nguvu na kuuhuisha kwa haraka.
Fenesi limejaa ufumweli au fibre, sifa inayosaidia kulainisha choo.
Tunda hili lina virutubisho kadha wa kadha vyenye faida kubwa mwilini. Baadhi ya virutubisho hivyo ni vitamini A, C, B complex, vitamin B6, folic acid, niacin, riboflavin na madini za aina mbalimbali kama vile potassium, magenesium, manganese na chuma. Katika tunda la fenesi kuna protini, mafuta, wanga na antioxidants. Fenesi pia linatajwa kuwa chanzo kizuri cha nishati kisichokuwa na mafuta. Si hayo tu, bali pia kwa kuwa na virutubisho vyenye uwezo wa kuondosha sumu mwilini.
Ttunda hilo linaweza kuukinga mwili dhidi ya saratani na magonjwa mengine
Pia kuongeza uwezo wa kuona.
Kiasi kikubwa cha madini ya potassium kinachopatikana katika fenesi hulifanya tunda hili liwe na uwezo pia wa kuimarisha mifupa na afya ya ngozi.
Wataalamu wa afya wanasema fenesi huongeza ufanisi wa mfumo wa kinga mwilini na kusaidia kuongeza kinga dhidi ya kifua, mafua na kikohozi. Hii ni kwa sababu ya kuwa na vitamini za aina mbalimbali. Faida nyingine ni kurekebisha msukumo wa damu na pia husaidia kurahisisha mmeng'enyo wa chakula tumboni pamoja na kuukinga mwili dhidi ya magonjwa ya moyo na kupooza. Sio vibaya kuelewa kuwa inasadikika kwamba tunda hili lina uwezo wa kuukinga mwili dhidi ya ugonjwa wa pumu na kupunguza makali ya ugonjwa huo. Si hivyo tu, bali fenesi lina vitamini muhimu zinazohitajika kwa ajili ya utengenezaji wa damu mwilini
FAIDA 10 ZA KULA MATANGO NA MATIKITI MAJI
Ulaji wa matango na matikiti maji husaidia kuboresha kiwango cha maji ambayo huitajika mwilini, hii ni kutokana na matango kuwa na kiwango kikubwa cha maji ambayo husaidia kuondoa taka mwili pamoja na sumu mbalimbali amb…Read More
MAPARACHICHI NA MAPAPAI: WAFALME WA MATUNDA -2
Ukipita maduka ya Uzunguni utakuta vyakula mbalimbali vinauzwa toka Afrika. Matunda haya yanayothaminiwa sana Majuu, huuzwa bei aghali sana.
Hapa London ambapo kila aina ya chakula ulimwenguni hupatikana bei za matunda…Read More
UYOGA: KINGA BORA DHIDI YA SARATANI
VIRUTUBISHO
maalum vinavyopatikana kwenye uyoga, vimevuta hisia za watafiti kwa zaidi ya miaka 20 sasa ili kupata uhakika kwamba mboga hii ina
uwezo mkubwa wa kutoa kinga kwa mwili wa mwanadamu dhidi ya ugo…Read More
TIKITI MAJI (WATERMELON) NA FAIDA ZAKE
Licha ya 92% ya tikiti maji kuwa ni maji, bado zile 8% zilizobaki zina faida kubwa sana kiafya jambo linaloonekana kutofahamika kwa wengi.Baadhi ya vyakula vimekuwa vikifurahisha pale vinapoliwa, tikiti maji ni miongoni m…Read More
FAIDA YA TUNDA LA MKOMAMANGA KITIBA
Dr. Clifford B. Majani
Mkomamanga (Punica granatum)ni mmea ambao asili yake ni katika nchi za Mashariki ya Kati (Middle East) na umetajwa sana katika vitabu vya kale vya historia ya eneo hilo. Kwa mujibu w…Read More
0 comments:
Post a Comment